Unyama: Diwani wa CHADEMA Mbeya Mjini anusurika kuuawa na watu wasiojulikana, apigwa panga la utosi, hakuna uchunguzi

Unyama: Diwani wa CHADEMA Mbeya Mjini anusurika kuuawa na watu wasiojulikana, apigwa panga la utosi, hakuna uchunguzi

Serkali inawajibika kulinda raia wake kwa namna zote bila kujali hisia zao kisiasa.
Lkn pia sio kila shambulizi ni serkali, je ujambazi siku hizi haupo?
Je serkali sasa hivi inatumia mapanga na marungu ?
Tuajadili mambo kwa wigo mpana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila CDM tumezidi uzwa zwa…. wanaotupiga hivi tunawajua, wengi wao tunaishi nao mtaani, tunalalamikaa alafu yanaisha, kesho, keshokutwa wanatandika mwingine tunalalamika tuuu yanaishaa, ilifeke mahali tuukatae huu mchezo, kwani nini
Pole sana mkuu kwa uchungu
 
Kichwa kinasema panga la utosi picha inaonyesha kwenye paji la uso sasa tushike lipi
unataka tukuwekee picha zote , halafu mara nyingi nakuona uko upande wa shetani , je wewe ni miongoni mwa wauaji ? simama uhesabiwe
 
Viombo vya dola waifanyie kazi na waje na majibu mujarabu, ili kuondoa ukakasi baina ya raia na vyomb vya dola.
 
Yani we jamaa bhana,kila baya unahusisha na siasa,tupe basi uthibitisho/maelezo ya kina kuliko ulivoandika kidogo hivyo. Kama wana matatizo yao binafsi je? Au ni wahuni walitaka kumpora kitu.

macson
 
View attachment 1348474
Hapa ndio mahali ambapo Nchi yetu na siasa zetu zilipofikia.

Tunamshukuru Mungu kwa kumlinda Mh Ibra dhidi ya wahalifu wanaolindwa ambao walimvamia alipotoka kwenye mgahawa kuelekea nyumbani kwake .

Mungu ibariki Chadema

=====

Ibrahim John Mwampwani diwani wa kata ya Isyesye Jijini Mbeya, amevamiwa saa nne na watu wanne wenye Mapanga na kukatwa sehemu za kichwani. Ameshonwa nyuzi 6, Alikuwa anatoka kwenye Shughuli zake za biashara.
Kuna watu watakuja kuhoji kwann hakuwahi kurudi nyunbani. Nina imani uchunguzi unaendelea kuwabaini wahusika.
 
Inachotakiwa ni kudhibiti kauli tu midomoni mwetu,inaleta shida sana,we ukimwambia MTU utaona harafu MTU huyo kesho apate matatizo watu watakuhisi wewe, hata kama siyo wewe, tuchunge ndimi zetu na kunena mabaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lile jeneza CHADEMA lililo onyeshwa na Tulia lilikuwa na maana gani??
Mdude Chadema alifanywaje au huelewi??
CHADEMA wanasababu ya kuwahisi CCM kwa sababu wanahamasisha mauwaji kwa wapinzani, Bulembo alihamasisha wakashangilia wote kama mataaila, hukuona bungeni??
 
Kwahiyo hii ndio kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya Tulia kubeba Jeneza lenye msalaba Mbeya ?
 
Yani we jamaa bhana,kila baya unahusisha na siasa,tupe basi uthibitisho/maelezo ya kina kuliko ulivoandika kidogo hivyo. Kama wana matatizo yao binafsi je? Au ni wahuni walitaka kumpora kitu.

macson
umewahi kusikia diwani wa ccm kacharangwa mapanga ?
 
Viombo vya dola waifanyie kazi na waje na majibu mujarabu, ili kuondoa ukakasi baina ya raia na vyomb vya dola.
uliwahi kusikia polisi wa Tanzania wakihangaika na majanga ya Chadema ?
 
jf ndio sehemu yenye upotoshaji mkubwa

Diwani wa kata hiyo namjua vizuri na siku ya tukio bahati nzuri nilkuwa mbeya

huyu alikuw na mke wake mdogo wametoka kwenye biashara yao ya cafe ndo wanarudi kwao then wakavamiwa na kibaka kwa lengo la kupokonya mauzo

kibaka alikata na panga mke wake akaachia pochi iliyokuwa na elfu 70.
jamaa akiwa anatak kumuokoa mkewe ndo akampiga panga hapo usoni

kwahyo msipotoshe umma kuwa kavamiwa na ccm no ni vibaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kwa Lisu ulisema haya haya, naomba hili pia lije kukutokea wewe au familia yako.
watanzania mnakoelekea siyo kuzuri kwa kuzani kuwa viongozi wa chadema ni malaika hawana makosa katika jamii huyu kapigwa panga lakini kabla hata ya uchunguzi unakuja na uzi kuwa ccm ndiyo wamempiga je unauhakika gani? je kama alikuwa na visasi na watu wengine utajuaje acheni ujinga mnaotaka kuujaza kwa watu yatawarudia nyienyie je alikuwa kwenye kutano wa siasa? unajuaje kama humo kwenye mgahawa kama kazurumu mtu akawa anamfuatilia?acheni kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi chadema mnasubiria kutendewa haya mpaka lini??? Mimi ningekuwa diwani au mbunge wa chadema ningeachia ngazi. Mana kila siku sisi tu ndiyo tunapigwa na hakuna hatua zozote kama chama tunazochuka, tunabaki kusubiria fisiemu watusaidie kuwakamata hao wanaotufanyia ubaya, this is pathetic.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila CDM tumezidi uzwa zwa…. wanaotupiga hivi tunawajua, wengi wao tunaishi nao mtaani, tunalalamikaa alafu yanaisha, kesho, keshokutwa wanatandika mwingine tunalalamika tuuu yanaishaa, ilifeke mahali tuukatae huu mchezo, kwani nini
Atua zichukuliwe na chadema waache uzwazwa. Kama Mbowe hana mikakati ya kuendesha operation ya kumaliza hili jambo apishe kwa muda. Watu wake kila siku wanatandikwa na yeye yuko kimya. Itafika siku hakuna hata mtu mmoja atakaye kubali kugombea nafasi yoyote kwa tiketi ya chadema kwani ataogopa kukutwa na mambo kama haya. CHADEMA CHUKUENI HATUA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom