mboperatransy
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 314
- 1,274
Mwizi aliniibia simu yangu asubuhi, jioni akakamatwa kaiba Tv, akapigwa sana, akaletwa hospitali, nikiwa ninamshona majeraha aliyepigwa, na mwananchi mmoja akatoa simu yangu iliyoibwa asubuhi akasema na simu yake hii hapa huyu mwizi.
Jamani iliniuma lakini kwa kuwa ni kazi na wito, nikaendelea kutoa huduma. Na badae nikachukua simu yangu.
Tokea pale yule mwizi alipotoka jela baada ya miaka 3 akaja kuniomba msamaha na sasa hivi ndio mjumbe wa mtaa wetu
Amebadilika kabisa. Hawa watu hubadilika.