Unyanyasaji wa wanawake wanaohudumu katika kumbi za starehe (Baa)

Unyanyasaji wa wanawake wanaohudumu katika kumbi za starehe (Baa)

Willima

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
26
Reaction score
39
Masuala ya kijinsia yanajumuisha nyanja na masuala yote yanayohusiana na Maisha na hali ya mwanamke na mwanaume katika jamii, jinsi wanavyohusiana, na tofauti zao katika upatikanaji na matumizi ya rasilimali, shuguli zao, na jinsi wanavyo itikia mabadiliko mbalimbali katika jamii. Jinsia ni aina mbalimbali za sifa zinazohusu mwanamke na mwanaume na tofauti zao kulingana na miundo ya kijamii inayo zingatia majukumu ya kila jinsia.

Jinsia ni ya umuhimu mkumbwa katika kufafanua uwezo na fursa ambazo baadhi ya Watu wanao na baadhi ya Watu hawana kaika jamii fulani. Pia kutafsiri na kutathmini jinsia za Watu wengine huathiri ushirmikiano baina ya jinsia katika jamii na maeneo mbalimbali ya kikazi, huu unyanyapaaji wa jinsia hususani jinsia ya kike katika maeneo ya kazi huathiri maemdeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

Unyanyasaji wa wanawake wanaofanya kazi ya kuhudumu bar umekithiri, suala hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara, wahudumu wengi wa Baa hususani wanawake wamekuwa wakikabiliana na matatizo mbalimbali kutoka kwa wateja wao hasa wa jinsia ya kiume, matatizo hayo ni kama kupokea maneno machafu kutoka kwa wateja wao na pia kushikwa kushikwa katika maeneo mabaya ya miili yao.

Hizi ni kero kubwa sana ambazo huvumiliwa na wahudumu wakike wa Baa, kwakuwa wanahitaji kipato na hawana njia nyingine ya kuwaingizia pesa ili waweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Unyanyasaji huu hupelekea wanawake wengi kukata tamta ya kuendelea kufanya kazi hiyo hivyo husababisha wengi kuacha kazi na hali hii hurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

Wanawake wanaofanya kazi ya kuhudumu Baa waheshimiwe kwani nao wanatafuta riziki kama watu wanao fanya shughuli zingine.

Kuheshimu kazi ya mtu mwingine ni morali tosha kwa mtu anayefanya kazi hiyo, heshimu kazi ya mwingine ili umjenge katika kazi hiyo na ili kuleta maendekeo katika jamii.
 
Masuala ya kijinsia yanajumuisha nyanja na masuala yote yanayohusiana na Maisha na hali ya mwanamke na mwanaume katika jamii, jinsi wanavyo husiana, na tofauti zao katika upatikanaji na matumizi ya rasilimali, shuguli zao, na jinsi wanavyo itikia mabadiliko mbalimbali katika jamii. Jinsia ni aina mbalimbali za sifa zinazohusu mwanamke na mwanaume na tofauti zao kulingana na miundo ya kijamii inayo zingatia majukumu ya kila jinsia.

Jinsia ni yaumuhimu mkumbwa katika kufafanua uwezo na fursa ambazo baadhi ya Watu wanao na baadhi ya Watu hawana kaika jamii fulani. Pia kutafsiri na kutathmini jinsia za Watu wengine huathiri ushirmikiano baina ya jinsia katika jamii na maeneo mbalimbali ya kikazi, huu unyanyapaaji wa jinsia hususani jinsia ya kike katika maeneo ya kazi huathiri maemdeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

Unyanyasaji wa wanawake wanao fanya kazi ya kuhudumu bar umekithiri, suala hili limekua likijitokeza mara kwa mara, wahudumu wengi wa Baa hususani wanawake wamekua wakikabiliana na matatizo mbalimbali kutoka kwa wateja wao hasa wa jinsia ya kiume, matatizo hayo nikama kupokea maneno machafu kutoka kwa wateja wao na pia kushikwa kushikwa katika maeneo mabaya ya miili yao.

Hizi ni kero kubwa sana ambazo huvumiliwa na wahudumu wakike wa Baa, kwakua wanahitaji kipato na hawana njia nyingine ya kuwaingizia pesa ili waweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Unyanyasaji huu hupelekea wanawake wengi kukata tamta ya kuendelea kufanya kazi hiyo hivyo husababisha wengi kuacha kazi na hali hii hurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

Wanawake wanao fanya kazi ya kuhudumu Baa waheshimiwe kwani nao wanatafuta riziki kama watu wanao fanya shughuli zingine. Kuheshimu kazi ya mtu mwingine ni morali tosha kwa mtu anayefanya kazi hiyo, heshimu kazi ya mwingine ili umjenge katika kazi hiyo na ili kuleta maendekeo katika jamii.
kwani wamekulalamikia
huu ni utafiti au ni observations zako
 
Lingekua ni tatizo bar zingekua na upungufu wa wahudumu wa kike
Wahudumu wanavumilia, kwasababu kwa wengi wao ndio njia pekee ya kuwaingizia kipato kwakua wengi wao hawana uwezo wa kupata njia nyingine ya kuingiza kipato kwasababu pia ya kutokua na elimu ya kutosha ambayo itawawezesha kupata kazi nyingine au njia nyingine ya kuwaingizia kipato kwahiyo inawa walazimu
 
wakikabiliana na matatizo mbalimbali kutoka kwa wateja wao hasa wa jinsia ya kiume
Wewe hujui lolote kuhusu iyo biashara ya bar. Mwenye bar anatoa platform tu, hao unaowakandia ndo waajili na walipaji wenyewe wakuu. chukua hiyo.
 
Ni wazo zuri lakini kama na wao wangezingatia uvaaji wa mavazi ya kimaadili yasio na ushawishi wowote sina imani kama wangefanyiwa vitendo hivo kwa wingi
 
kwani wamekulalamikia
huu ni utafiti au ni observations zako
Hakuna alie nilalamikia lakini ni vitu vinavyo jitokeza sana kwa wahudumu wa jinsia ya kike na hali hii huwa kama maonevu kwa wahudumu hao na kwakua hawana utetezi na namna yakufanya kuzuia vitendo hivyo huwa wanakaa kimwya ili waweze kulinda kazi zao.So kuheshimu kazi ya mtu mwingine ni muhimu kama vile unavyotaka kazi yako iheshimiwe.
 
Ungeanza na wamiliki wa bar wanao walaza zaidi ya watano geto moja na kuwalipa elfu hamsini.
Hayo yasikufanye wewe kudharau kazi ya huyo muhudumu, hiyo ni hali tu ya maisha ambayo hutokea na pia hupita, chamuhimu hapa ni kumheshimu huyu muhudumu, na yeye anahitaji heshima katika kazi yake kama wewe kazi yako inavyo heshimiwa
 
Itabidi tutumie sheria za mashariki, wanawake wajirembe wakae uwani maana wao ni maua na wakitoka watoke na msindikizaji 😁😁
Wanawake pia wanaweza kufanya kazi tu kama wanaume, chamuhihu ni kuheshimu kazi wanazo zifanya.
 
Upo sahihi kabisa,asilimia kubwa ya wadada wanaofanya hizi kazi za bar wengi wanafanya kwasababu hawana option nyingine ya kuwaingizia kipato,kwahiyo tunapokuwa tunalipa kodi tujaribu kuwaheshimu
 
Ni wazo zuri lakini kama na wao wangezingatia uvaaji wa mavazi ya kimaadili yasio na ushawishi wowote sina imani kama wangefanyiwa vitendo hivo kwa wingi
Ninaamini kila kazi inauvaaji wake, na pia matukio haya huwa hayashawishiwi na mavazi ya mtu bali ni akili ya anae muona na ile namna anyo mchukulia muhudumu uyo kama angekua anamheshimu hawezi kupata wazo la kumzalilisha kwa amna yoyote ile. Sio kwamba ni wanawake wanao hudumu baa tu ndio wanao vaa nguo za kushawishi, unaweza kutana tu mwanamke barabarani ambae hajavaa nguo ya kumsitiri lakini ni vigumu kumzalilisha kwakuwa humjui. Hivyo ninaamini ni namna mtu ameijenga akili yake juu ya muhudumu uyo
 
Ni wazo zuri lakini kama na wao wangezingatia uvaaji wa mavazi ya kimaadili yasio na ushawishi wowote sina imani kama wangefanyiwa vitendo hivo kwa wingi
Ninaamini kila kazi inauvaaji wake, na pia matukio haya huwa hayashawishiwi na mavazi ya mtu bali ni akili ya anae muona na ile namna anyo mchukulia muhudumu uyo kama angekua anamheshimu hawezi kupata wazo la kumzalilisha kwa amna yoyote ile. Sio kwamba ni wanawake wanao hudumu baa tu ndio wanao vaa nguo za kushawishi, unaweza kutana tu mwanamke barabarani ambae hajavaa nguo ya kumsitiri lakini ni vigumu kumzalilisha kwakuwa humjui. Hivyo ninaamini ni namna mtu ameijenga akili yake juu ya muhudumu huyo
 
WANAWAKE WAMEUMBWA KWA AJILI YETU, SAWA TUTAWAHESHIMU
 
yaani unafananisha kazi ya kuwahudumia walevi na kazi ya kuuza mchele ama nyanya?be serious dude!
 
kwani wamekulalamikia
huu ni utafiti au ni observations zako
Kwenye qualitative research..one of methodology ya kukusanya data ni observation...hivyo mleta mada atakua ameamu kutumia njia hiyo kufanya utafiti..swali kumuuliza je ni overt au covert observation.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom