Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Muendelezo wa unyanyasaji wa viongozi wa upinzani hasa kuanzia zama za Magufuli na sasa wakati huu wa Rais Samia, una impact moja: kuwafanya wapinzani kuwa jasiri huku msingi mkuu wa huo ujasiri ni kuona au kuamini kuwa kwa sasa hawana tena cha kupoteza kwani kama ni kuteswa, wameshateswa sana, na kama ni kuuwawa, wenzao wengi wameshauawawa sasa kwanini wao wawe tena hofu.
Hali waliofikishwa viongozi wa upinzani na wanachama na mashabiki wa upinzani, ni sawa na hatu ambayo mtu hufikia kufanya maamuzi magumu ya kujinyonga baada ya kuona kuna mambo yamemuelemea/yanamtesa na sasa haoni tena faida ya kuishi na anakuwa amejenga ujasiri wa kujiua. Hii ndio hatua wapinzani wa nchi hii wamefikishwa na tawala hizi za kimabavu.
SATIVA na Mdude ni ushahidi mzuri wa hichi nachesema. Hata Godbless Lema kupitia video aliojirekodi kaweka wazi kuwa safari hii hatakimbia tena nje ya nchi na hata sms inayodaiwa kuwa ni ya Lissu akimwambia OCD kuwa yuko teyari watoe roho yake, ni ushahidi mwingine wa hiki nachokisema.
Pia soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
Hivyo, kama watawala wanafikiria kutumia dola dhidi ya wapinzani ndio kutawafanya wawe waoga au warudi nyuma, ukweli ni kwamba, wanawajengea ujasiri kupitia shida na hayo mateso wanayowapa na kuwafanya wafikie "the point of no return" katika mapambano na kuona ni bora kufia vitani kuliko kuendelea kunyanyaswa' Hata wapelstina hii ndio spirit yao japo hawana jeshi kama la wayahudi ila wanapambana bila kujali wao ndio wanakufa kwa wingi zaidi.
Kwa msingi huo, halii hii ya wao kuona hawana tena cha kupoteza ndio itawafanya wajitokeza tena bila woga mbele ya askari waliosambazwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaama. Na tunakoelekea, itafika hatua wananchi hawataogopa wala kutishika tena na uwepo wa askari mitaani.
Ndio maana kuna wakati unaweza kuona swala au nyati anajitokeza kupambana na Simba. Mfano ni pale swala au nyati anapoona maisha yake hayana maana tena baada ya Simba kuwa ameua au kujeruhi kitoto chake au mmoja wao katika kundi.
That is nature, and that is also the nature of human being if not all animals on this planet.