Unywaji wa maziwa Tanzania ni anasa au ni kwa afya bora

Unywaji wa maziwa Tanzania ni anasa au ni kwa afya bora

mwaswast

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
12,780
Reaction score
6,480
tmsowoya@mwananchi.co.tz
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
“Sikumbuki lini ilikuwa mara ya mwisho familia yangu kunywa maziwa kwa sababu ni gharama na siwezi kumudu bei yake, kuliko kununua maziwa, ni bora ninunue mboga za majani watoto wale.”
Hivi ndivyo mkazi wa Tabata Kisiwani, jijini Dar es Salaam Benitho John alivyozungumzia unywaji wa maziwa.
Kwake jambo hilo ni kama anasa na haoni umuhimu wake mwilini. Sio Benitho peke yake anyedhania hivyo, ukweli ni kwamba baadhi ya watu wanapuuzia na hawaoni umuhimu wa kunywa maziwa hata kama yapo karibu nao.
Wakati leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya unywaji wa maziwa, wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa maziwa yanakazi nyingi mwilini ikiwano ya kuifanya ngozi kuwa nyororo, kuimarisha meno na mifupa kutokana na vitamin zilizopo.
Takwimu za Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (Fao) za mwaka 2014, Kenya inaongoza Afrika kwa uzalishaji wa maziwa ya ng’ombe wakati Tanzania ikishika nafasi ya tisa.
Shirika la Afya Duaniani (WHO), linapendekeza kila mtu anywe angalau lita 200 za maziwa kwa mwaka ingawa wastani kwa dunia ni lita 108.
Kiwango cha unywaji wa maziwa kwa Tanzania kwa kila mtu ni chini ya lita 50 kwa mwaka wakati Kenya ikifikia lita 130.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zinazokabiliwa na changamoto ya kuwa na watoto wenye udumavu, ugojwa ambao unachangiwa kwa kiwango kikubwa na lishe duni wanazozipata watoto walio chini ya miaka mitano.
Sababu kubwa inayofanya watoto hao kudumaa ni ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Maziwa yana virutubisho vyote muhimu kwa ujenzi wa afya ya binadamu kwani yana protini ya daraja la kwanza, mafuta, madini, vitamin na sukari ya asili ya lactose na maji.
Jambo hilo linailazimisha Kampuni ya Asas Dairies Ltd kuingia kwenye kampeni ya kuhamasisha unywaji wa maziwa kwa shule za msingi za Manispaa ya Iringa.
“Tunataka walau unywaji wa maziwa ufikie asilimia 60, watu waone umuhimu wa kunywa maziwa kwa sababu ni muhimu kwa afya zao,” anasema mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo, Ahmed Salim Abri.
Salim Abri anasema lengo ni kupanda mbegu ya unywaji wa maziwa kwa wanafunzi ili hata wanapokuwa nyumbani wawahamasishe wazazi kununua maziwa.
“Katika kampeni hii tumetenga lita 120,000 za maziwa zikiwa na thamani ya Sh60 milioni ili katika wiki hii ya unywaji wa maziwa kila mtoto apate,” anasema.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mshikamano, Haiba Roy anasema kuna haja ya kuanzisha kampeni ya unywaji maziwa shuleni kila siku, ili kuwasaidia kiafya wanafunzi wengi wakiwamo wanaokwenda shule wakiwa hawajapata mlo wowote toka nyumbani kwao.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mtwivilla, Florian Kilumile anasema uamuzi wa kampuni hiyo kufanya kampeni ya unywaji maziwa unapaswa kuungwa mkono na wadau wengine ikiwamo Serikali, ili kuwakumbusha wazazi kujenga utamaduni wa kununua maziwa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto.
Baadhi ya wanafunzi wanakiri kuwa wengi wao hawajawahi kunywa maziwa wakiwa nyumbani.
“Nyumbani huwa sinywi maziwa kabisa kwa sababu wazazi hawaoni umuhimu huo ila wakielimishwa wanaweza kuanza kununua hata mara mbili kwa wiki,” anasema mwanafunzi Juma Salehe.
Salim Abri anasema inawezekana kila familia kutenga bajeti kidogo ili kuhakikisha inapata maziwa kutokana na umuhimu wake.
Sio tu kwa Iringa, zaidi ya watoto 2,000 wa shule za awali na msingi wenye umri wa hadi kufikia miaka tisa mkoani Njombe, wamenza kunufaika na mpango wa unywaji wa maziwa bure katika siku zote za shule kama mbinu ya kuimarisha afya na kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto.
Idadi hiyo ni miongoni mwa watoto 10,000 watakaofikiwa na programu hiyo katika mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na Mbeya wakati mradi huo unatekelezwa na shirika la kimataifa la Heifer kupitia moja ya miradi yake.
Meneja wa mradi wa uendelezaji wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD II) Tanzania, Mark Tsoxo anasema mpango wa unywaji maziwa shuleni unalenga kukuza utamaduni wa kunywa maziwa miongoni mwa watoto na kutengeneza mahitaji imara kwa ajili ya maziwa.
Katibu wa Tanzania Women Power (TPW), jijini Dar es Salaam Joyce Madenge ambaye pia ni mwalimu, anasema mpango wa maziwa shuleni unaweza kusaidia kujenga afya hasa za watoto wanaokosa fursa ya kuyapata.
Umuhimu wa maziwa mwilini
Mtaalamu wa Lishe kutoka Jukwaa la Lishe nchini (Panita), Debora Essau anasema umuhimu wa maziwa mwilini ni mkubwa hasa kutokana na virutubisho vilivyopo.
Anasema maziwa yanaweza kumfanya mtu kuwa na meno imara yanayong’aa, ngozi nyororo na ng’avu pia na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini.
Deborah anasema maziwa yana madini ya Calcium yenye kazi kubwa ya kujenga mifupa na meno.
“Kwa hiyo uimara wa meno na mifupa hutegemea pia unywaji wa maziwa, ni vizuri familia kujiwekea mkakati wa kila mtu kupata maziwa,” anasema.
Anasema maziwa pia yana vitamini ‘D’ kwa wingi ambayo inaweza kupatikana kwa kuota jua hasa wakati wa asubuhi.
Wataalamu wa afya wanasema upungufu wa vitamini hii unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya kuanzia udhaifu wa mifupa, matatizo ya nywele na hata udhaifu wa misuli.
Debora anasema mbali na vitamin hiyo, unywaji wa maziwa yana protini ambayo pia husaidia kujenga mwili.
“Kumbuka hiki ni kimiminika na kama unvyojua, unapokunywa kimiminika unalainisha choo hivyo unywaji wa maziwa unaweza kuufanya mwili kuwa na nguvu kwa kupata uhakika wa choo,” anasema.
Utafiti mmoja uliowahi kufanywa nchini Marekan ulieleza kuwa unywaji wa maziwa hasa yanayotokana na wanyama unaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa utafiti huo vitamin D inayopatikana kwenye maziwa husaidia utengenezwaji wa kichocheo cha Serotonin kinachohusisha masuala ya ‘mood’.
Unaweza kupata hamu ya kula, kulala na wakati mwingine unywaji wa maziwa unaweza kupunguza uchovu na kumpa mtu raha.
Deborah anasema maziwa mazuri zaidi ni yale yatokanayo na wanyama kwani yana protini inayopatikana kwa kiwango cha hali ya juu.
“Maziwa pia hutupatia sukari japo kwa kiasi kidogo hivyo nisisitize tu kwamba ni muhimu kila mmoja kuzingatia unywaji wa maziwa katika milo ya kila siku,” anasema.
Mtaalamu mwingine wa lishe Matrida Kassanga anasema unywaji huo wa maziwa haupaswi kupita kiasi.
“Kunywa maziwa kiwango kile kinachotakiwa mwilini, usinywe maziwa mengi hasa krimu kwa sababu unywaji huo unaweza kukusababisha uzito kupita kiasi,” anasema.
Salim Abri anasema kwa sababu maziwa hayawezi kudumu muda mrefu yasiposindikwa ipasavyo, kampuni hiyo itaanza matumizi ya teknolojia ya UHT kutengeneza aina mbalimbali za maziwa.
“Teknolojia hii ya Ultra High Temperature inawezesha maziwa yanayosindikwa kukaa kwa muda mrefu, hadi miezi sita bila kuharibika hata yakiwekwa katika maeneo yasio na mashine za kuyapooza,” alisema.
Anasema sio tu maziwa fresh hata yale ya mtindi yanazo faida nyingi kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu

Unywaji wa maziwa Tanzania ni anasa au ni kwa afya bora
 
Tunaambiwa ni land of milk and honey.😀😀😀
Aah wapi! Ndio sababu kuu ya malnutrition in Tanzania among young children due to lack of a balanced diet . Hawa Watu wa mihogo 24/7 bora tumbo ijae.
 
Kuna vitu muhimu kuliko maziwa, WHO wanasema inatakiwa kila mtu anywe lita 200 za maziwa kwa mwaka.

Hawajui maziwa ya Tanzania unaweza kunywa lita 200 kumbe lita 3 tu ndio zilikuwa sawa nyingine ni Maji ya mchele.
 
Bongo unaweza kutembea mbali sana ndio upate chai nzuri ya maziwa, nilikua nafikiria ni mambo ya Pwani, nilshangaa hata mikoani wako hivyo.
..............and the way they have a lot of land. Kenya tukipewa hiyo nchi yao tunaweza kusupply dunia nzima maziwa.
 
Maziwa sio jambo la kila mtu, kuna watu wengi hawapendi kunywa maziwa, na wengine wakinywa allergy zina wasumbua. Kukosa pesa ya kunywa maziwa sio swala la ajabu maama hata Kenya kuna watu hawawezi kununuwa maziwa. Mbona Kenya samaki ni shida kupata mpaka mnaagiza kutoka nje wakati mna bahari, mito na maziwa yanawazunguka?

Kenya yearly fish consumption per capita = 4.5kg.


Tanzania yearly fish consumption per capita = 20kg.
 
Ni kama chakula kilivyo hadimu kwenu!
Hadimu ndio chakula gani?
Maziwa sio jambo la kila mtu, kuna watu wengi hawapendi kunywa maziwa, na wengine wakinywa allergy zina wasumbua. Kukosa pesa ya kunywa maziwa sio swala la ajabu maama hata Kenya kuna watu hawawezi kununuwa maziwa. Mbona Kenya samaki ni shida kupata mpaka mnaagiza kutoka nje wakati mna bahari, mito na maziwa yanawazunguka?

Kenya yearly fish consumption per capita = 4.5kg.


Tanzania yearly fish consumption per capita = 20kg.
Lake Victoria, Tanganyika, Lake Malawi, River great Ruaha, Rufiji, Mara, Ruvuma, malagarasi Kagera and a 1424 km long coastline got lots of Fish unlike Arid Kenya.
 
Maziwa sio jambo la kila mtu, kuna watu wengi hawapendi kunywa maziwa, na wengine wakinywa allergy zina wasumbua. Kukosa pesa ya kunywa maziwa sio swala la ajabu maama hata Kenya kuna watu hawawezi kununuwa maziwa. Mbona Kenya samaki ni shida kupata mpaka mnaagiza kutoka nje wakati mna bahari, mito na maziwa yanawazunguka?

Kenya yearly fish consumption per capita = 4.5kg.


Tanzania yearly fish consumption per capita = 20kg.
Bring evidences here dude.. Alergy ni excuse kubwa sana pesa ndio Hanna...aty maziwa ni luxurious
 
Right now nakunywa pombe yangu mdogo mdogo ...Tanzania kukunyw maziwa nikama kukunywa hiki ki mzinga.
IMG_20180106_191208.jpeg
 
Maziwa hayanitiii mzuka kuyanywa,utakuta nakunywa soda nyingi kwa mwezi kuliko hata kikombe cha maziwa..labda siku niiamue hua natengeneza masala chai ile chain ya kihindi iliyojaa viungo na maziwa
 
Hadimu ndio chakula gani?

Lake Victoria, Tanganyika, Lake Malawi, River great Ruaha, Rufiji, Mara, Ruvuma, malagarasi Kagera and a 1424 km long coastline got lots of Fish unlike Arid Kenya.
Malawi landlock country, consume more fish than Kenya. In fact they used to eat 14kg, 3x more than Kenya before it drop 5.4kg.
 
Maziwa hayanitiii mzuka kuyanywa,utakuta nakunywa soda nyingi kwa mwezi kuliko hata kikombe cha maziwa..labda siku niiamue hua natengeneza masala chai ile chain ya kihindi iliyojaa viungo na maziwa

mkuu achana na soda kunywa maziwa kwa afya bora
 
Back
Top Bottom