Unywaji wa maziwa ya ng'ombe hauna tija na afya yako (African and Asian)

Unywaji wa maziwa ya ng'ombe hauna tija na afya yako (African and Asian)

Hupunguza. Tena sio kwa kila mtu ni kwa baadhi ya watu tu. Na tatizo hilo laweza kuwa la muda tu au kwa maisha yote.
Kiasi cha 68% ya watu wazima (adults) duniani huweza kujikuta wana changamoto hiyo ya upungufu wa Uwezo wa ku-digest aina ya sukari iitwayo Lactose ipatikanayo kwenye maziwa. Hili ni kutokana na mwili wa mhusika kupungukiwa na uwezo wa kuzalisha aina ya kimeng'enya (Enzyme) iitwayo Lactase.
Watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha enyme ya Lactase lakini kadri wanavyokua (grow-up) uwezo huo nao hupungua -wengine hupungua kiasi kikubwa mno na hao ndo wenye tatizo la Lactose intolerance ukubwani lakini wengine huendelea kuwa na uwezo huo hata wakiwa wakubwa adults. Kwa mantiki hiyo watu wazima (adults) hutofautiana kwa viwango tofauti na pia eneo mtu alikokulia e.g. huku kwa wafugaji ni nadra sana au ni mara chache sana kukutana na tatizo hilo.
Asante sana kwa elimu mkuu🙏🏽.
 
Yeah; If it is documented and written "Seems to be"..... it means that the issue is subject for further investigations.
Kwa mantiki hiyo huo utafiti bado haujakamilika i.e haujafika mwisho. Unaendelea. Tusubiri hatima italeta jawabu gani.
Masuala ya "A" is linked to "B" inatafsiriwa
1. In maths: "A" ina mahusiano na "B" = Relations
2. In biology(Genetics): "A" inatokana na "B" i.e. "A" amerithi kutoka "B" au "B" amerithi kutoka "A" = A & B ni ndugu. Kuna asilimia (100%)ya Muunganiko/ Mfanano/ Uingilianaji
 
Habari wakuu, Kama kichwa habari kinavyo eleza ya kuwa waafrika na waasia hawawezi kunufaika kiafya kwa kunywa maziwa.
Kwa utafiti uliofanywa na chuo kikuu Cha Cornell kimegundua ya kuwa watu wengi -- kama asilimia 60 na hasa wale wenye asili ya Asia na Afrika -- wanaacha kuzalisha lactase, kimeng'enya kinachohitajika kusaga maziwa, kwani kimsingi ni watu ambao mababu zao walitoka sehemu ambazo mifugo ya maziwa inaweza kufugwa kwa usalama na kiuchumi, kama vile huko Uropa, ambao wamekuza uwezo wa kusaga maziwa na hapa wakiangalia wakigusia adhari hizo za ki-DNA zimetokea kabla ya 1900.

Ingawa watoto wote wa mamalia hunywa maziwa ya mama zao, wanadamu ndio mamalia pekee ambao hunywa maziwa wakiwa watu wazima.

Ila watu wa asili ya kaskazini mwa Ulaya, Wana uwezo wa kuzalisha kimeng'enyo hivyo uwapa sababu ya kunywa maziwa katika maisha yao.

Ni ukweli usiopingika ya kuwa Kila kiumbe kimepewa utaratibu wake wa kula mfano ndege wanatofautiana kwenye vyakula hivyo hivyo kwa wanyama walao majani nk seuze kwa binadamu hivyo kutokana na georgrafia na sababu nyingine za kimaumbile kama rangi, nywele, vimo, nk kwanini isiwe kwenye vyakula pia.
Kuna utafiti uliofanywa nchini Marekani imebaini yakuwa kutokana fast foods kuwa ndio mlo unaliwa na wengi ila imeonekana kuwaadhiri zaidi watu wenye asili ya Afrika na Asia zaidi ndio wanoongoza kwa magonjwa yatokanayo ni kuongezeka uzito wa mwili kupita kiasi.

Source: The Cornell university and many other​
Kabisa ndio maana wale wenzetu wa matoke samaki na maharage wanazalisha maji mengi kwenye lile jambo letu lile;;;;😜anyway,,,,,nisha acha uhuni
 
Elites wanajua chakula ni biological weapon, ni ujasusi watu Wana control population. Na wasio jua maana wanapiga kelele hii ni ajabu.
 
Shida naiona ni kwamba tunasubiri aliyetengeneza mfumo aje atuambie ni kweli sio nzuri, na hapa tumegusa uwezo wa mwili wetu kumeng'enya vipi kuhusu ufugaji wakisasa na dawa na sindano zinzotumika kuchochea uzalishaji.
Chemical hizo zinamadhara Gani kwa mlaji? Ni ipi tofauti ya maziwa ya mama na ya wanyama wengine (wachanga), kwa nini wauzaji wa maziwa ya unga wamelazimishwa kuandika ukweli ya kuwa maziwa ya mama ni Bora kuliko ya maziwa yao tena akisisitiza kua mtoto chini ya miezi sita apewe maziwa ya mama, licha yakuandika kwa maandishi madogo chini kabisa. Ila yanasomeka. Pengine tunasubiri watuandikie kwenye lable kama sigara kwa ni hatari kwa afya Yako.
 
Back
Top Bottom