Uchaguzi 2020 Uoga: 2020 Mwaka wa uchaguzi umefika lakini CCM yaendelea kuzuia Mikutano ya hadhara, Msajili wa Vyama aufyata

Uchaguzi 2020 Uoga: 2020 Mwaka wa uchaguzi umefika lakini CCM yaendelea kuzuia Mikutano ya hadhara, Msajili wa Vyama aufyata

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ili kuhalalisha uvunjifu wa Katiba ya nchi, Mwenyekiti wa CCM ndugu Magufuli alinukuliwa akitoa marufuku ya shughuli za kisiasa kwa kisingizio dhaifu cha kuleta maendeleo na kwamba wenye hamu ya kufanya siasa wasubiri mwaka wa uchaguzi 2020, Polisi wakadaka amri hiyo haramu kama kifanyavyo kidaka tonge kwenye chakula , wanasiasa waliojaribu kupinga amri hiyo haramu wakakamatwa, wakapigwa, wakateswa na baadaye kuswekwa lupango na kisha kufunguliwa kesi za kizushi na kufungwa jela, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya kusini Mh Suleiman Methew ni miongoni mwa wanasiasa waliofungwa kwa vile walifanya mikutano kinyume cha katazo la Magufuli (Majina ya Polisi wote waliotumika tunayo)

Kama wasemavyo Wahenga, Usiku wa deni hauchelewi kwisha, basi ndicho kilichotokea, 2020 imefika na bado waliosema tuisubiri wanaogopa kuruhusu mikutano ya hadhara, wanaomba siku zirudi nyuma lakini haiwezekani, hawajui cha kufanya na wamekwama, kile kilichoitwa kuzuia siasa ili kuleta maendeleo hakipo, bali ifahamike kwamba badala ya maendeleo hali ya kiuchumi imekuwa mbaya zaidi, hakuna ajira kwa miaka yote minne, wala hakuna nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wachache wasiozidi laki 6 wa serikali, hali ni mbaya hata kuliko kabla ya zuio la mikutano.

Hata hivyo wananchi wametambua kwamba kukataza siasa haikuwa sababu ya maendeleo bali ulikuwa uoga wa Mwenyekiti wa CCM ambaye alikuwa hana ajenda ya kuwaambia wananchi baada ya kuingia ikulu Kibahati .

Itaendelea...
 
Hivi asiporuhusu hadi wiki moja kabla ya uchaguzi kufanyika kutatokea nini?

Swali hili linaweza likaonekana kama la kipuuzi; lakini kiuhakika, ningependa kujua jibu lake ni nini.
Siyo swali la kipuuzi, ni swali la kufikirisha.
Ni vigumu kuvuka mto kabla hujaufikia lakini siyo vibaya kupanga mikakati ya namna ya kuuvuka huo mto mara utakapoufikia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom