Mr Sir1
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 1,749
- 7,945
Kuna tabia mpya Traffic wameanzisha barabara ya Nyerere baada ya Quality Center ikiwa unaelekea mjini wanaweka utepe kwenye uelekeo wa Service Road ilipo bank ya Absa karibu na Lifemate Furniture.
Hata ikiwa dhamira yao ni kuzuia watu wanaeonda mjini wasichepuke, lakini haileti maana kwa sehemu walipoweka utepe maana kuna ofisi nyingi kwenye hiyo service road, kupelekea mtu anaetaka kwenda katika moja wapo wa hizo ofisi kukosa pa kuingilia.
Na hii imekuwa mradi kwao maana kuna baadhi ya watu wanatoa hongo na wanawaruhusu kupita.
Hata kama ni kula kwa urefu wa kamba zao, lakini wafikirie na wengine pia.