Tetesi: Uongo juu ya JKT

Aise hao vijana wa mabasi ya njano tokea wanaanza kindergarten wanaamshwa sa kumi alfajir kujitayarisha ili kuwah hayo mabasi ya njano...kwao kuamka sa tisa usiku sidhani ka ni jambo jipya...
 
Aise hao vijana wa mabasi ya njano tokea wanaanza kindergarten wanaamshwa sa kumi alfajir kujitayarisha ili kuwah hayo mabasi ya njano...kwao kuamka sa tisa usiku sidhani ka ni jambo jipya...
TAtizo sio kuamka inshu ni ulaini...
 
ephen_ njoo umsikilize mwenzio huku.
Mkuu ephen_ njoo uone maneno kuntu huku toka kwa bwana nanga
Mkuu! Watu tunatofautiana kuzikabili changamoto
Mimi hata leo niambiwe nirudi jkt Sirudi Ng'oo
Lakini wengine wanatamani hadi wanalia kurudi jeshini

Nakubaliana na mleta mada kwenye suala la โ€ŠMisosi! Jeshini wanajua kutulisha vitu vinavyoeleweka nakumbuka nyama za kule zilivyo mapande hadi raha
 
Uko sahihi mkuu
 
Mkuu sehem ya kuamka saa tisa
Ukiitwa unakuja mbio na kurudi mbio na hapo umefafanua vema kuwa Kila mda ni "kipindi"hapo hakuna bata nimekulia TMA master jeshi ni kipengele
Sahihi mkuu
 
Yah mara nyingi huwa hivyo unakuta mtu afya mbovu. Mfano hapo DRC kuna vichwa vinaitwa kaibiles hao jamaa ni SF ya nchi ya Guatemala (commando) walienda ku train askari wa SF ya FARDC hao jamaa kimsingi nawakubali sana kwenye swala la misitu mikubwa ni balaa.
Sasa moja kati ya training yao wakati wanaelekea mwishoni mwa kozi kuna zoezi hufanyika hivi watahiniwa lazima wafanye doria kupitia brashi iliyojaa miiba wakiwa wamevaa chupi, kubiringika kwenye miiba ili kuupa mwili maumivu, na kutumia siku mbili kwenye maji hadi shingoni bila kulala kwenye joto kali la kitropiki. Hatua hii inaitwa El Infierno kikwao yani HELL ("Kuzimu").

Ukiwa na afya mbovu hata hapo hufiki.

Noma sana homboy.
 
Balaa๐Ÿ“Œ
 
Sasa umekanusha nini na wewe umeandika nini???

Kulala masaa 3 ni starehe kwako??

Hakunq faraja kwenye mateso, acha kuhalalisha ujinga hapa.

Kwenda jeshini inapaswa iwe hiari kwa anaetaka, sio mambo ya kulazimishana.
 
Waridi wangu ephen alishaeleza kila kitu kwa hiyo vijana wanaotaka kwenda JKT huwa nawaambia wasome uzi wa shemeji na wifi yao ephen kupata mwanga kidogo. na siyo wanakwenda wamebeba matranka makubwa na mazito utafikiri wanafunzi wanaoripoti kidato cha kwanza shule ya bweni.
 
Jeshini kule nilikua D coy .
Kuna wana walikua wanajiita kitengo TANAPA yaani hao mda wa kuamka kabla hawaja hesabiwa wanasepa polini huko hawarudi mpaka foleni ya usiku..

Bwawani ilikua mbali kidogo ukizingatia na baridi la asubuhi daaah..
Kule bwawani kulikua na kitengo bustani yaani hao mda wote wanashida bwawani.

Tukimaliza kazi ya kuchota maji tunakuja ku foleni uwanjani hapo sasa kipindi cha uzalendo kila mtu anapangiwa majukumu kutokana na kitengo chake .. yote yote kitengo kilichokuwa kinaogopwa ni shamba aiseeee ..

Tulipo kuwa kurutu ndo kasheshe ilianza.. yaani kula mpaka mpige rout na unakuta rout ni ndefu aiseee yaani huko ni kufata ticket ya chai au chakula...

Kipindi cha kurutu ni kipindi kigumu sana maana hapo ndio hujulikana nani kitunguu nani nyanya...

Kuna mambo nikikumbuka aiseee kule kuna maisha ya hovyo sana sometimes...

Kuna kunyonya mafuta
-Pushap za X
-Kushona.
-Kunya maji chupa kama mbili zile A lita moja ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ
-Viroba kama 400 hivi

Siku ya intro na siku ya ujanja wa msituni ndo nusu watu wakate moto....
 
WAzi afande
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ