Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana mkuu Kuna kitu nimemkumbuka jeshiniMbn umeanza nakicheko mkuu😁
ephen_ njoo umsikilize mwenzio huku.
Mkuu! Watu tunatofautiana kuzikabili changamotoMkuu ephen_ njoo uone maneno kuntu huku toka kwa bwana nanga
Uko sahihi mkuuMkuu! Watu tunatofautiana kuzikabili changamoto
Mimi hata leo niambiwe nirudi jkt Sirudi Ng'oo
Lakini wengine wanatamani hadi wanalia kurudi jeshini
Nakubaliana na mleta mada kwenye suala la Misosi! Jeshini wanajua kutulisha vitu vinavyoeleweka nakumbuka nyama za kule zilivyo mapande hadi raha
Mkuu sehem ya kuamka saa tisaSio bata kiivyo mkuu jeshini ni jeshini,jeshini sio sehemu ya watu walaini
Yah mara nyingi huwa hivyo unakuta mtu afya mbovu. Mfano hapo DRC kuna vichwa vinaitwa kaibiles hao jamaa ni SF ya nchi ya Guatemala (commando) walienda ku train askari wa SF ya FARDC hao jamaa kimsingi nawakubali sana kwenye swala la misitu mikubwa ni balaa.Tatizo watu wanadanganyana sasa mtaani kuhusu jeshini.
✅️mfano wakat nipo kambi X kuna watu wawili walifariki
Nilivyorudi mtaani watu walikua wanacomplain sana kwamba watu wamekufa wakati wanafanya mazoezi means mazoezi yalikua magumu kupitiliza
✅️wakati mi nipo kwenye hiyo kambi X watu hao ambao walifariki nawafahamu na walikua ni wagonjwa wa kudumu na wote vifo vyao vilisababishwa na afya zao
Balaa📌Yah mara nyingi huwa hivyo unakuta mtu afya mbovu. Mfano hapo DRC kuna vichwa vinaitwa kaibiles hao jamaa ni SF ya nchi ya Guatemala (commando) walienda ku train askari wa SF ya FARDC hao jamaa kimsingi nawakubali sana kwenye swala la misitu mikubwa ni balaa.
Sasa moja kati ya training yao wakati wanaelekea mwishoni mwa kozi kuna zoezi hufanyika hivi watahiniwa lazima wafanye doria kupitia brashi iliyojaa miiba wakiwa wamevaa chupi, kubiringika kwenye miiba ili kuupa mwili maumivu, na kutumia siku mbili kwenye maji hadi shingoni bila kulala kwenye joto kali la kitropiki. Hatua hii inaitwa El Infierno kikwao yani HELL ("Kuzimu").
Ukiwa na afya mbovu hata hapo hufiki.
Noma sana homboy.
Aliyenzisha huu uzi ni SHOGA.Kama jeshini ni bata basi Kuna namna jeshi limepoteza umakini ila jeshini haipaswi kuwa bata
Jeshini kule nilikua D coy .Habari wana Jf
nisiwachoshe tuende moja kwa moja kwenye uzi.
katika mitaa yetu tunayoishi kumekua na tetesi nyingi zinazosambaa zikihusisha na kuelezea maisha ya jeshini(JKT) na kuonekana ni tishio kwa vijana ambao wanatarajia kwenda jeshini.
Utafiti ambao nimefanikiwa kuufanya katika kipindi kifupi mtaani nimefanikiwa kugundua kwamba wengi wao wanaosambaza taarifa hizo asilimia 80 wakati asilimia 20 ni watu ambao wameenda jeshini na kama ilivyo sifa ya fasihi simulizi ya kukosa uhalisia kutokana na kuongeza na kupunguza taarifa hizo
. Mfano wa uzushi huo ni kama;
📌kula kwa kuhesabiana dakika
Ambapo kijana atatakiwa kula kwa haraka ndani ya muda ambao amepangiwa,muda huo ni kama vile dakika 5 au 10
📌mafunzo ya jeshini(jkt) ni magumu kiasi kupelekea vifo vya vijana
📌jeshini ni sehemu ya mateso na sio mafunzo kama wasemavyo
Huo ni baadhi ya uzushi kuhusu maisha ya jeshini pia kama mdau wa Jf naamini utakua umekutana na uzushi na tetesi nyingi zaidi kuhusu maisha ya jeshini ukiachana na machache ya hapo juu
✅️niendelee kwa kuelezea kwa ufupi maisha ambayo niliexperience nikiwa jeshin.
Mnamo mwaka 2022 nilifanikiwa kwenda kambi X ya jeshi ya jkt kwa ajiri ya mafunzo
ilikua mnamo saa 12 niliwasilini kambini hapo,nilikutana na vijana wenzangu ambao wamewasili kambini hapo wakiwa wamekaa chini wakisubiri muda waongezeke na wengine ambao tunawasili ili tuweze kuondoka kwa pamoja
Baada ya kama nusu saa tuliambiwa tusimame na kutembea single line tayari kwenda kuacha vitu vyetu na rasmi kuanza maisha ya kambiani hapo wengi wetu walikua wamevaa full track suit na vipara
Tulifika maeneo ya mbwenini ambapo jeshini tunaita anga tulikabidhiwa vitanda vjzuri tukalala hadi asubuhi
Katika kipindi hicho unakua na cheo cha uzalendo maisha yalikua simple sana zaidi zaidi ni kukimbia kimbia na kuimba nyimbo za hamasa maarufu kama chenja
. 💥MUDA WA KULALA
Wakati tupo wazalendo muda wa kulala haukua constant kutokana na mfumo uliopo kwa maana tulikua tukihesabu namba na kuitwa majina ndipo unaenda kulala,siku zingine tulikua tunalala saa nne ,nyingine saa tano zingine saa tatu na nusu
💥 MUDA WA KUAMKA
muda wa kuamka ulikua saa tisa alfajiri tunafoleni tunahesabiwa namba tunaenda kwenye majukumu kama vile kufanya usafi maeneo ya kambi na wengine kwenda bwawani kwa ajiri ya maji ya bustani,sasa hapa wengi wao wanaanza kuona maisha magumu kutokana na muda ambao wamezoea kuamka wakiwa kwao na hapa wengi wao wale wa MABASI YA NJANO😁 utawaona wanalalamika zaidi kutokana na ulaini walionano
💥MUDA WA CHAI
muda wa chai ni pale watu washafanya shughuri tofaut tofauti kama vile walioenda shamba na kazi zingine wanarudi kikosini na kujumuika wote kwa ajiri ya chai ilikua ni saa nne kamili,unapatiwa mkate na chai ambayo tulikua tunakunywa kwa ndani ya saa moja na sio kwa dakika kama wasemavyo walimwengu.
Baada ya chai tunafoleni tena then wanatugawa kwa vitengo mfano shamba ,ujenzi na usafi na ingine zaidi kwa idadi
💥 CHAKULA CHA MCHANA
Ilikua ni saa saba kamili,wakati huo watu wote waliokua kwenye vitengo wanarudi wanakusanyika kwa ajiri ya chakula cha mchana,tulikua tunakula ugali,maharage na mboga zingine,pia nyama ilikua mara tatu kwa wiki.
Kama ilivyo jeshi"JESHINI KILA KITU NI KIPINDI PIA KULA NAKO NI KIPINDI,KULA NI LAZIMA HAUTAKIWI KUKUTWA NJE YA ENEO LA CHAKULA MUDA WA KULA" ,Baada ya kumaliza kula tunakusanyika tena na kuendelea na shughuri ndogo ndogo
Hapo muda wako wa kupumzika ni wakati wa kula na kulala sasa kama ilivyojesshi. "JESHINI SIO NYUMBANI" hapa sas magari ya njano wanalialia maisha magumu😁,jeshini kuna muda ulikua unapewa upumzike ukiwa kitengoni ukiwa umemaliza kazi kwa wakati maarufu kama "kula tano"
💥CHAKULA CHA USIKU
TUlikua tunakula saa 12 hadi saa moja,wakati wa kula ukifika kazi zote zinasitishwa.
Chakula kilikua wali maharage na chai kila siku pia kulikua na pilau na nyama baada ya hapo tunafoleni kwa ajir ya kuita majina tayar kwa kulala
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
Kuna watu walikua wanatoroka kwa kuona maisha magumu has MABASI YA NJANO ni walaini sana
💥 BAADA YA KUFUNGUA KOZI
hapa unakua unepandishwa cheo na kuitwa KURUTI na sio mzapendo tena hapa sas kulala ni saa 6 kuamka saa tisa
Hapa ndo kunamazoezi madogo madogo ya jeshi
Hapa wengi hutoroka hasa walain
Kutoroka kupo unaweza kutoroka ukarudi jiona ni wewe tu hapa kuna kitu tunaita "SIFA WEPESI" ukiwa mzito kila kitu utashiriki ila ukiwa mwepesi unatoroka hadi siku ya posho😁 unahisi kuna mazoezi
Jeshini ni kwa kiasina sio kama wasemavyo mwalimwengu 📌🔨🔨
WAzi afandeJeshini kule nilikua D coy .
Kuna wana walikua wanajiita kitengo TANAPA yaani hao mda wa kuamka kabla hawaja hesabiwa wanasepa polini huko hawarudi mpaka foleni ya usiku..
Bwawani ilikua mbali kidogo ukizingatia na baridi la asubuhi daaah..
Kule bwawani kulikua na kitengo bustani yaani hao mda wote wanashida bwawani.
Tukimaliza kazi ya kuchota maji tunakuja ku foleni uwanjani hapo sasa kipindi cha uzalendo kila mtu anapangiwa majukumu kutokana na kitengo chake .. yote yote kitengo kilichokuwa kinaogopwa ni shamba aiseeee ..
Tulipo kuwa kurutu ndo kasheshe ilianza.. yaani kula mpaka mpige rout na unakuta rout ni ndefu aiseee yaani huko ni kufata ticket ya chai au chakula...
Kipindi cha kurutu ni kipindi kigumu sana maana hapo ndio hujulikana nani kitunguu nani nyanya...
Kuna mambo nikikumbuka aiseee kule kuna maisha ya hovyo sana sometimes...
Kuna kunyonya mafuta
-Pushap za X
-Kushona.
-Kunya maji chupa kama mbili zile A lita moja 😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌
-Viroba kama 400 hivi
Siku ya intro na siku ya ujanja wa msituni ndo nusu watu wakate moto....