Tetesi: Uongo juu ya JKT

Tetesi: Uongo juu ya JKT

Khaaa mkuu umepita huko nini...
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Mnashangaa mbona tunaanza kupimwa kisa intro... Kumbe kichoenda kutokea hapo ni zaidi ya matatizo...
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Noma mkuu___ mselema,syllas(pt),meja_oromi,bosco, balaa😁😁
 
Noma mkuu___ mselema,syllas(pt),meja_oromi,bosco, balaa😁😁
Mselemu... D coy
Ochu...
Bugau
Oromi

Bosco jamaa wa shambani.... Ahahaha shamba mkakatiii manina walaaaaaahiiii

Oya ile bwawani sa 9 daaah kule nachi hapana aiseee
 
Mselemu... D coy
Ochu...
Bugau
Oromi

Bosco jamaa wa shambani.... Ahahaha shamba mkakatiii manina walaaaaaahiiii

Oya ile bwawani sa 9 daaah kule nachi hapana aiseee
Watu wa B COY walikua wanakula bata sana kuliko wote😁
 
Watu wa B COY walikua wanakula bata sana kuliko wote😁
Khaaa yaani nini B coy wale bata kuliko nani
......

Kwanza mi kule ningehama aiseee wale jamaa wanasifa sana aiseeeee B coy achana nao aiseeee
 
Habari wana Jf
nisiwachoshe tuende moja kwa moja kwenye uzi.
katika mitaa yetu tunayoishi kumekua na tetesi nyingi zinazosambaa zikihusisha na kuelezea maisha ya jeshini(JKT) na kuonekana ni tishio kwa vijana ambao wanatarajia kwenda jeshini.
Utafiti ambao nimefanikiwa kuufanya katika kipindi kifupi mtaani nimefanikiwa kugundua kwamba wengi wao wanaosambaza taarifa hizo asilimia 80 wakati asilimia 20 ni watu ambao wameenda jeshini na kama ilivyo sifa ya fasihi simulizi ya kukosa uhalisia kutokana na kuongeza na kupunguza taarifa hizo

. Mfano wa uzushi huo ni kama;
πŸ“Œkula kwa kuhesabiana dakika
Ambapo kijana atatakiwa kula kwa haraka ndani ya muda ambao amepangiwa,muda huo ni kama vile dakika 5 au 10

πŸ“Œmafunzo ya jeshini(jkt) ni magumu kiasi kupelekea vifo vya vijana

πŸ“Œjeshini ni sehemu ya mateso na sio mafunzo kama wasemavyo

Huo ni baadhi ya uzushi kuhusu maisha ya jeshini pia kama mdau wa Jf naamini utakua umekutana na uzushi na tetesi nyingi zaidi kuhusu maisha ya jeshini ukiachana na machache ya hapo juu

βœ…οΈniendelee kwa kuelezea kwa ufupi maisha ambayo niliexperience nikiwa jeshin.
Mnamo mwaka 2022 nilifanikiwa kwenda kambi X ya jeshi ya jkt kwa ajiri ya mafunzo

ilikua mnamo saa 12 niliwasilini kambini hapo,nilikutana na vijana wenzangu ambao wamewasili kambini hapo wakiwa wamekaa chini wakisubiri muda waongezeke na wengine ambao tunawasili ili tuweze kuondoka kwa pamoja
Baada ya kama nusu saa tuliambiwa tusimame na kutembea single line tayari kwenda kuacha vitu vyetu na rasmi kuanza maisha ya kambiani hapo wengi wetu walikua wamevaa full track suit na vipara
Tulifika maeneo ya mbwenini ambapo jeshini tunaita anga tulikabidhiwa vitanda vjzuri tukalala hadi asubuhi


Katika kipindi hicho unakua na cheo cha uzalendo maisha yalikua simple sana zaidi zaidi ni kukimbia kimbia na kuimba nyimbo za hamasa maarufu kama chenja

. πŸ’₯MUDA WA KULALA
Wakati tupo wazalendo muda wa kulala haukua constant kutokana na mfumo uliopo kwa maana tulikua tukihesabu namba na kuitwa majina ndipo unaenda kulala,siku zingine tulikua tunalala saa nne ,nyingine saa tano zingine saa tatu na nusu

πŸ’₯ MUDA WA KUAMKA
muda wa kuamka ulikua saa tisa alfajiri tunafoleni tunahesabiwa namba tunaenda kwenye majukumu kama vile kufanya usafi maeneo ya kambi na wengine kwenda bwawani kwa ajiri ya maji ya bustani,sasa hapa wengi wao wanaanza kuona maisha magumu kutokana na muda ambao wamezoea kuamka wakiwa kwao na hapa wengi wao wale wa MABASI YA NJANO😁 utawaona wanalalamika zaidi kutokana na ulaini walionano
πŸ’₯MUDA WA CHAI
muda wa chai ni pale watu washafanya shughuri tofaut tofauti kama vile walioenda shamba na kazi zingine wanarudi kikosini na kujumuika wote kwa ajiri ya chai ilikua ni saa nne kamili,unapatiwa mkate na chai ambayo tulikua tunakunywa kwa ndani ya saa moja na sio kwa dakika kama wasemavyo walimwengu.
Baada ya chai tunafoleni tena then wanatugawa kwa vitengo mfano shamba ,ujenzi na usafi na ingine zaidi kwa idadi

πŸ’₯ CHAKULA CHA MCHANA
Ilikua ni saa saba kamili,wakati huo watu wote waliokua kwenye vitengo wanarudi wanakusanyika kwa ajiri ya chakula cha mchana,tulikua tunakula ugali,maharage na mboga zingine,pia nyama ilikua mara tatu kwa wiki.
Kama ilivyo jeshi"JESHINI KILA KITU NI KIPINDI PIA KULA NAKO NI KIPINDI,KULA NI LAZIMA HAUTAKIWI KUKUTWA NJE YA ENEO LA CHAKULA MUDA WA KULA" ,Baada ya kumaliza kula tunakusanyika tena na kuendelea na shughuri ndogo ndogo
Hapo muda wako wa kupumzika ni wakati wa kula na kulala sasa kama ilivyojesshi. "JESHINI SIO NYUMBANI" hapa sas magari ya njano wanalialia maisha magumu😁,jeshini kuna muda ulikua unapewa upumzike ukiwa kitengoni ukiwa umemaliza kazi kwa wakati maarufu kama "kula tano"

πŸ’₯CHAKULA CHA USIKU
TUlikua tunakula saa 12 hadi saa moja,wakati wa kula ukifika kazi zote zinasitishwa.
Chakula kilikua wali maharage na chai kila siku pia kulikua na pilau na nyama baada ya hapo tunafoleni kwa ajir ya kuita majina tayar kwa kulala

πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
Kuna watu walikua wanatoroka kwa kuona maisha magumu has MABASI YA NJANO ni walaini sana
πŸ’₯ BAADA YA KUFUNGUA KOZI
hapa unakua unepandishwa cheo na kuitwa KURUTI na sio mzapendo tena hapa sas kulala ni saa 6 kuamka saa tisa
Hapa ndo kunamazoezi madogo madogo ya jeshi
Hapa wengi hutoroka hasa walain

Kutoroka kupo unaweza kutoroka ukarudi jiona ni wewe tu hapa kuna kitu tunaita "SIFA WEPESI" ukiwa mzito kila kitu utashiriki ila ukiwa mwepesi unatoroka hadi siku ya posho😁 unahisi kuna mazoezi



Jeshini ni kwa kiasina sio kama wasemavyo mwalimwengu πŸ“ŒπŸ”¨πŸ”¨
Wewe ulipita jkt ya wapi hiyo ambako hawakufa watu, sisi kufa wamekufa sana watu labda jkt ya mama
 
Wewe ulipita jkt ya wapi hiyo ambako hawakufa watu, sisi kufa wamekufa sana watu labda jkt ya mama
Vifo vinasababishwa na sababu tofaut tofauti kama vile magonjwa , hata pale jkt kuna watu ambao wamekufa nawaham kabisa wanachangamoto ya afya ambaoo ilipelekea kuwekwa kwenye kundi maaalum la wagonjwa ambao walikua hawafanyi mazoezi magumu kama wengine
 
Nilikua kitengo maalumu wakatcwa kurud nlizamia kwa wagonjwa wa kudumu
 
Kambi hutofautiana.

Kambi nilioenda mimi ilikuwa ukifika getini unakimbizwa na risasi.
Yaani MP wameshikilia mijegeja aina ya SMG afu wanakupimia, mbio zako tu.

Ilikuwa haina uzalendo, ukifika unatritiwa kama komando. Yaani pushapu 15k za kuanzia huku mgongoni kuna gunia la mahindi la kilo 50.
 
Kambi hutofautiana.

Kambi nilioenda mimi ilikuwa ukifika getini unakimbizwa na risasi.
Yaani MP wameshikilia mijegeja aina ya SMG afu wanakupimia, mbio zako tu.

Ilikuwa haina uzalendo, ukifika unatritiwa kama komando. Yaani pushapu 15k za kuanzia huku mgongoni kuna gunia la mahindi la kilo 50.
Aaahh acha bana bwana shetani πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Nilikua kikosi x... walivunjika vijana 12 wenye ulemavu walikua watatu ilipelekea mp mmoja, coplo wawili na private kadhaa kutawanywa vikosi vingine kile kikosi kazi cha wale masoja ni zaidi ya special force

Kuna dogo mmoja wa kigoma alidoji akadakwa juu ya mzambarau πŸ˜‚πŸ˜‚, demo yake afande alipanda akajitupa na tumbo hadi chini halafu serviceman arudie vile vile 😫, dogo alivunjika asee mkono sema alipona

JKT ya intake ya 2014 kurudi nyuma ilikuwa zaidi ya vita
 
Back
Top Bottom