Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Nimekuambia ana ratibu mzunguko wa jua na mwezi ,kinachotokea kwa binadamu ambacho hata wewe hujui kesho yako.

Sijaona hoja yako mpaka sasa zaidi ya 😂😂kubisha...Toa hoja zako maana najua hauna.
Adui mkubwa sio ujinga (lack of knowledge)
Ispokuwa ni illusion of knowledge.

Hiyo ni mbaya sana.

Anayeratibu jua na mwezi ni nani?

Bado utataja Mungu ambaye ni wa kufikirika na ndiyo tunaomba uthibitisho wake kama yupo kweli.

You are making circular fallacy.

Yani kwamba madai yako ndiyo yanakuwa uthibitisho.

What a shame!
 
Sasa hujui huoni kama ni kazi kumuelewesha mpumbavu (yaani hujui halafu hutaki kujua).

Hamna unachojua zaidi ya kufuata mkumbo ..Huu sio mtihani tunatumia akili na uhalisia wa maisha.

Je hiki kinajibu kile nlichokuuliza zaid ya Ad hominem tu.

Nmekuuliza,
wew unayejua unaweza kunieleza chanzo cha binadamu kwa kunipa hizo facts!?
 



Uwezi kuwa na akili za kufika mbali kama huwezi kufirikia ,lazima ujiulize maswala hao wanagunduzi wote kweny tafiti zao walianza kwa kujiuliza maswali ndio wakaanza kufanya tafiti.


Kwa vile hauna hoja sioni tatizo😂😂😂....jua kwa nn lina ratiba kila siku na hakuna anayezunguka hiyo ratiba kila siku.... Binadamu alianzaje maisha hapa duniani? Je dunia ina miaka mingapi mpaka sasa ukiachana na hii 2023?
 
Je hiki kinajibu kile nlichokuuliza zaid ya Ad hominem tu.

Nmekuuliza,
wew unayejua unaweza kunieleza chanzo cha binadamu kwa kunipa hizo facts!?
😂😂Kwa nn wwe hauna majibu na hutaki kuelewa?

Nimekuuliza haujawahi kujibu hata mara moja .!
 
Nimecheka saaana. Wee jamaa umetafakari sana haya mambo kwa kina. The way ulivyoandika sasa.....
 
Niliongelea dhana ya Mungu in general, au wewe unadhani dunia hii ina mungu wako tu?

Kwamba Allah kaombwa na Ibils abaki ili ampoteze binadamu na Allah akamkubali baki ili awapoteze ...... shida inaanzia hapa(kwanini amkubalie? Was it necessary?)

Kwanza kabisa akamrubuni Adam na Hawwa wakamkosea Allah matokeo yake Allah akawaondoa bustani ya kula bata akawaleta duniani kula shuruba kama maradhi magonjwa majanga nk(tunashurubika hata ambao hatukuwepo)
Matokeo yake mengine sasa ukichukulia dini moja wapo iwe sahihi utapata 80% ya watu wote duniani shetani atakuwa kawapotosha
Na ukichukulia hio dini ambayo ipo sahihi labda islam bado watakao kuwa wanafuata sahihi ni asilimia ndogo zaidi

Hii inafanya zaidi 90% ya watu wote duniani Ibils aliyemuomba Allah kuturubuni atakua katurubuni

Kwahiyo 99% ya watu wote duniani tutakwenda kuchomwa moto wa milele kwasababu tu Allah katuletea Iblis atupotoshe [emoji23][emoji23][emoji23]

Halafu bado unaambiwa Mungu anatupenda kama tunavyo penda mbona ya jicho letu

Kwa msingi huu Allah kwangu ni jitu fulani katili limemuumba binadamu ili ateseke duniani na majanga na kesho ahera motoni
 
Liko wapi jibu la swali langu hapo.!?

Umeanza kuinadi qurani yako tu kuipigia upatu badala ya kunijibu

Kwamba ukiifata qurani hutakumbwa na tetemeko, kifo, magonjwa, kuonewa n. K

Kwa sifa zake huyo Mungu inaonesha kabisa alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kutokea kabisa.

Kitendo cha kuumba huu ulimwengu wa namna hii (unaoruhusu mabaya) unafanya kuharibu sifa yake ya upendo wote ama ujuzi wote.

Kwanini Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kaumba ulimwengu huu wenye kuruhusu mabaya!?
 
Basi unathibitishaje Mungu ni Allah na sio Yahweh
 
🤣okay tufanye hivi twende kwa facts me nachoka kubishana na watu wanaojikosha
 

Attachments

  • Screenshot_20230912-110451.png
    42.5 KB · Views: 4
Kwa imani yangu naamini Mungu yupo ila sio huyu tuloletewa na wazungu/ warabu
Sabu ata mababu zetu kabla ya wazungu na warabu kuja walikua na Mungu wao walomwabudu na kumfanyia matambiko pale wanapokua na mattzo ama furaha
 
Japo mie ninaamini mungu yupo,lkn nikiri wazi kabisa kuwa wewe ni mtu mwenye akili sana,una uweze mkubwa sana wa kujenga hoja na kushawishi.
 
Hizo hisia ulizopata ndizo Mungu aliekuumba anazo na kukuzidi, ndio maana akaweka uwezo wa "kuji-resert" hiyo kansa inaisha(healing miracle), ila naamini kwa kilicho moyon mwako hutoweza kufikia hiyo level ya "resert"...
Kama ww ni mwanaume na una watoto..kile unachowaelekeza wanao unahisi kimekujia tuu kichwani hakuna origin yake?kwann umlinde bint yake asipigwe p wakat bint za wenzio unawapgsha "mijeled" bila huruma?kwasababu bint yko una-link nae ya kiroho na kimwili ndio maana roho inakuuma asifanyiwe unachofanyia wengine-the same kwa Mungu dhidi ya wanadamu aliowaumba kwa sura na mfano wake+small spirit portion ya pumzi yake.....wanadamu tunapata matatizo na hahitaji kutushikia fimbo kwakua ameshatoa maelekezo na mafundisho yote ya kukulinda, the same kwa kwa bint yako umemfundisha hiki do's hiki dont's akitoka hapo akaenda huko "mamende" wakampiga "mijeled" akarud na mimba what would you do? Kwani si ulishamfundisha kuishi njia unayoona ni sahihi..?? Au karud kapgwa tu "mjeled" utajua?ukimuuliza atasema? The same kwa Mungu hana haja ya kurudia kwakua elimu yote ametoa, na option ya msamaha katoa..bint yko mkaid na mwingine mnyenyekevu unawa-treat sawa?

Utofauti wako wewe na Mungu ni ROHO (origin of spirit) wewe kakuongezea mwili wa kutenda na maamuzi binafsi..siku ukifa(mwili kutengana na spirit) hayo maamuzi na mawazo ya kung'amua na kujiuliza "Mungu ni scam" yanatoweka kwakua utakua unaona visivyoonekana...(ndio maana mchawi anaogopa maswala ya ibada za dini..)
 
Nakupa kazi hapa uje uonyeshe ya kuwa Mtume hakuwa anashushiwa maagizo.
Bado tunazunguka pale pale kama Allah hayupo basi hata hayo maagizo hayakushuka

Allah HAYUPO

Kuna concept of Russel inasema

Kama niki kwambia kuna kibuyu kidogo cha Kinyiramba kinazunguka kwenye orbit ya jua
Ni kidogo sana kiasi kwamba huwezi kukiona kwa macho wala kwa mtambo wowote ule utaniamini?
The fact is hutaniamini hata kama hauna huwezo wa kuthibitisha

Concept hii inaonyesha mambo mawili

Mosi, Wajibu wa kuthibitisha anao aliyedai uwepo wa kitu

Pili, Mtu akikwambia habari za mashaka mwitikio wa kwanza ni kutokuamini na sio kuamini
Kwahiyo kutokuamini ni msingi wa kwanza hadi kuwepo uthibitisho

PROVE IT
 
Mimi sijaona
Naomba ufanye hivyo [emoji120]
Naanzia hapa, uwepo wa Mola muumba unathibitishwa kwa njia hizi.

1. Akili
2. Mazingira
3. Ufunuo.

Naanzia na ufunuo, kwa maana Qur'an.

Anasema Allah mtukufu, kuwapa "Challenge" wakana Mungu, sababu walikuwepo tangu zama za mitume.

33. Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!

34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (At-Tur : 33-35)

Maswali hayo mawili yanaonyesha hii Dunia yupo aliye iumba.
 

Mkuu mfano unatoa ni MFU

Mimi nazungumzia watoto wachanga wanazaliwa na saratani maisha yao yote wataishi kwa tabu na dhiki ya mionzi na chemotherapy
Most of them will never make to adulthood
Hawa wamemkosea nini Mungu?

Usinifananishe na mungu
Ningekuwa nina uwezo wa kimungu ningemuepusha mwanangu na balaa yote regardless na atakayo nifanyia
 
Skia si hatuna shida na wewe wishful thinking yako ya kuwa na sky daddy invincible anayekupenda na kukulinda...Ila ndo Usiforce waarabu na wayahudi kuleta miungu Yao na tufate sheria zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…