Japo mie ninaamini mungu yupo,lkn nikiri wazi kabisa kuwa wewe ni mtu mwenye akili sana,una uweze mkubwa sana wa kujenga hoja na kushawishi.
Nashukuru sana mkuu kwa kutambua hilo, Na umekuwa muelewa.
Watu wengine huwa hawawezi kukubali ila wanataka ubishi tu.
Na waki ishiwa hoja huanza kutumia matusi, kejeli na kuni shambulia kwa lugha zisizofaa.
Siku zote, Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika,
Na kitu kikisha fahamika na kuthibitishika kipo, Hakuna haja tena ya imani kutambua uwepo wa kitu hicho.
Nikupe mfano mdogo,
Mwanafunzi anaye fanya mtihani, kabla ya matokeo kutoka anakuwa hana uhakika wa ufaulu wake utakuwaje, ila anakuwa Ana "imani" ya kwamba atafaulu, Lakini kwa vile hana uhakika vizuri hajui atafaulu kwa kiwango kipi, Pia vile vile anaweza akafeli au akafaulu kwa kiwango tofauti na matarajio ya "Imani" yake kwa vile Hana uhakika.
(Ni imani yake tu)
Lakini matokeo ya mtihani yakishatoka, Imani hiyo ya kuamini kwamba "Atafaulu au atafeli" ina ondoka na kuwa ukweli na uthibitisho wa kwamba mwanafunzi huyu "Amefaulu au Amefeli" kwa uthibitisho wa kuonekana kwenye cheti chake cha matokeo au karatasi ya mtihani aliyo jibia.
Na hapa mwanafunzi huyu anakuwa Hana "imani" tena ya kwamba "amefaulu au amefeli" kwa vile ana uthibitisho wa uhakika wa jibu moja tu, kwamba kweli amefaulu au amefeli kwa kuangalia vyeti vyake au matokeo yake ya mtihani yaliyo toka.
Imani ile ya kusema kwamba nitafaulu au nitafeli inakuwa haipo.
Hivyo msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika juu ya jambo fulani,
Ukweli Hauendani na imani.
ukweli una endana na kujua, uwepo wa uthibitisho, facts, evidences na Logic.
Yani kwenye imani hata 1+1 jibu linaweza kuwa tisa kwa imani, kwa vile ni imani tu.
Ila kwenye ukweli 1+1 jibu lazima liwe 2.