Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Kwanza Allah ndio ameumba ndimi za watu, katika surat al Insaan amegusia hilo, ya kuwa ameumba mataifa na makabila mbali mbali lengo tupate kujuana.

Kwahiyo Allah ndie ameumba lugha na mataifa, na haongei Kiarabu, bali Allah akituma mjumbe sehemu anampa ujumbe kwa lugha yakez ndio maana Ibrahim aliongea kwa lugha yao, Musa, Yesu na kadhalika Mtume aliongea au kupewa ujumbe kwa lugha ya Kiarabu sababu alianza kuzungumza na watu wake kwa lugha hiyo, vipi Mtume awe Muarabu halafu apewe ujumbe kwa Kisukuma na watu wake wanaongea Kiarabu ?

Allah anaeleweka kwa lugha zote, ndio maana tunamuomba na kumsoma. Lakini lugha sio kikwazo kama ukiamua kujifunza, na ukianalgalia lugha ya Kiarabu ni tofauti na lugha nyinginezo bali husemwa lugha hii ni ya watu wote na ushahidi uko wazi, ukisoma Historia ya fani za Kiarabu utakuta wasomi wa kubwa wa lugha hii Ulimwenguni kote si Waarabu kiasalia, lakini tafuta lugha nyingine hilo hulikuti. Tukiongelea katika mlango huo hakuna lugha kuishinda Kiarabu.

Kujua Kiarabu ni lazima kama ukitaka kujua Dini hii, sababu imekuja kwa lugha ya Kiarabu. Lakini hakuna aliye zaliwa anajua, hata wewe Leo hii umezaliwa hujui kusoma Wala kuandika lakini umesomeshwa na ukajua. Sasa kwanini hili hulisemi ? Leo hii ulienda Saudia utakuta Waafrika wanawasomesha Waarabu Kiarabu,maana yake nini ? Hii ni elimu Haina wenyewe ukitaka kujua unajua ukizembea ni wewe na uzembe wako.

Hajashindwa kufanya hivyo, bali angetaka sote tumuamini tunge kumaini kama ilivyo nukuliwa hivyo katika Qur'aan, ila amefanya haya na kuweka hali wezekano za kujua ambayo wewe unayadai ukitaka. Mola wetu hapendi watu wazembe.
Kwa nini Quran hiyo isifanyiwe tasfiri (translation) kwa lugha zote duniani ili iweze kueleweka na watu wote?

Kama "Allah" huyo ni Mungu wa binadamu wote, Alishindwaje kuleta Quran hiyo katika lugha zote au Quran hiyo kuweza kufanyiwa tasfiri ili kila mtu aelewe maandiko hayo kiurahisi.

"Allah" huyo, Anajua kabisa watu wapo kwa lugha tofauti lakini Quran hiyo ninyi waislamu mnadai, Haiwezi kufanyiwa tafsiri kwa lugha nyingine tofauti na kiarabu.

Huyo "Allah" kama alitaka tuijue Quran kwa lugha ya kiarabu, Alishindwaje kutuumba binadamu wote ulimwenguni kote, Tuzungumze kwa Kiarabu tu?

Ili iwe rahisi mafundisho yake ya Quran hiyo kueleweka kwa watu wote ulimwengu mzima?
 
Kwanini unaandika uongo ? Mara ngapi nimewakosoa kuhusu logic na mkashindwa kutetea utoto wenu ?

Nakupa kazi hapa, kati ya maneno na logic kipi kilianza ?
Umekosoa lini kuhusu logic zaidi ulijionesha kuwa hujui nini maana ya logic.?

Yaani hata maswali yako na misimamo yako huwa ni illogical,

Nawewe nakuuliza kuwa kati ya dunia na gravity kipi kilianza!?

Kingine njoo uthibitishe ukweli wa logic katika kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu, zaidi ya kucheza na maneno na kuikimbia hoja.

Msingi wa logic ni akili, akili ambayo ni dhaifu na ina ukomo vipi utumie akili pekee kukufokisha katika ukweli ?

Shida yenu hizi elimu mlizichukua kiushabiki ndio maana zinawafanya muwe wajinga na msio weza kufikiria nje ya mawazo ya waasisi wa logic zenu.
Uthibitisho wenye kuonesha logical contradiction katika dhana ya uwepo wa Mungu ni kama ifuatavyo.

Test no 1

Chukulia mfano
"Theist anaposema kuwa
1. * Kila kitu lazima kiwe na chanzo
2.* ulimwengu na vyote vilivyomo vina chanzo havikutokea bila mtengenezaji
3.* Chanzo hicho ni Mungu.

Je Mungu katengenezwa na nani/chanzo chake ni nini

4.* Mungu hana chanzo!!!

Hivyo tyar mzungumzaji kajipinga yeye mwenyewe.
Hoja Nambari 4 imepinga hoja nambari 1.

Hivyo hakuna logical consistency hapo, zaidi ni kwamba anakuwa analazimisha ujinga.

Na hapo unajua kuwa Mungu huyo analazimishwa tu.

Test no 2.

Sifa ambazo anapewa Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote halafu akaumba ulimwengu huu wenye kuruhusu mabaya

1. * Mungu muweza wa yote.

Asingeshindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kwa namna yeyote ile ili viumbe wake waishi kwa amani na furaha.

Lakini tunashuhudia mabaya hayo.
Uwepo wa mabaya hayo unadhihirisha kuwa Mungu si mwema hata kidogo.

2.* Mungu mjuzi wa yote

Kaumba huu ulimwengu ili kujaribu watu wake, yaani awapime kwamba wale watakaofaulu (wema) waende peponi, na wale watakaofeli (waovu) waende motoni.

Inamaanisha Mungu huyo si mjuzi wa yote, kwamaana hakuwa na haja ya kutest vitu ilihali anafahamu Destin ya viumbe vyake.

3. *Mungu mwenye upendo wote

Kwa ujuzi wake inaonekana kabisa aliumba kuzimu kabla hata ya viumbe wenyewe.

Then kumbe Mungu huyo si mwenye upendo wote.

==Uwepo wa majanga mazito kama matetemeko na vimbunga vikali kama Tsunami,

Majanga hayo yanaleta taabu sana na kusababisha ndugu kutenganishwa na vifo, ikiwemo watoto wachanga wasiojua kitu.

Hii inapinga dhana ya kwamba Mungu huyo ni wa haki na mwenye upendo wote.

Hizo ni baadhi tu nmejaribu kukuonesha jinsi dhana hiyo inavyojipinga yenyewe.

Na kujipinga huko kunathibitisha kuwa Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hawezekani kuwepo katika ulimwengu wenye kuruhusu mabaya!!!
 
Kama Mungu yupo na alitaka tumwabudu yeye, Alishindwaje kutuumba binadamu wote tukiwa na ufahamu wa kutambua yeye yupo?

Na kutu ondolea ufahamu wa kutomtambua yeye hayupo?

Tuka mwabudu kwa dini moja na Kitabu kimoja tu, Kinacho eleweka kwa binadamu wote wa Lugha zote ulimwenguni, Pasipo utata na utofauti wa ki maudhui?

Kama Mungu Yupo, Kwa nini ajifiche na kutuachia mtafaruku mkubwa na utata wa kutambua uwepo wake?

Yani ni sawa na kucheza mchezo wa kujificha (Kombolela) na kutafuta kisicho kuwepo.

Ndicho kinacho fanyika kumtafuta Mungu huyo.
FB_IMG_1694529280169.jpg
 
Hahaha

Jamaa anakushushia na lawama kabisa.

Tatizo unaweza kukuta mtu kaishi kwenye echo chamber, internet aliyonayo haitumii kumtoa humo apate concepts mpya, then anakutana na atheistic comments za kiranga humu jf for the first time, hapo lazima akuone stranger na baba wa atheism duniani 😂😂😂
Kuna watu hawaamini kabisa kwamba inawezekana akawepo mtu haamini katika uwepo wa Mungu, yani katika akili zao, hicho kitu hakiwezekani.

Kwa sababu ya udogo wa mawazo yao.
 
Haya maelezo hayana mantiki.

Kwamba utaratibu, watakaofeli wataenda motoni(tyari hapo Mungu si mwenye upendo wote).

Na kama kaumba kiumbe halafu akakipa mtihani means anataka kukipima/kukijaribu kufeli ama kufaulu (maana yake Mungu si mjuzi wa yote).

Halafu hapo hapo unasema kwamba anajua nani atafaulu na yupi atafeli...

Huoni jinsi maelezo yako yanakosa mantiki.
Safi kabisa, uje tena kusema ya kuwa mantiki ni jambo la msingi. Nitakuuliza swali kwanini umefikia hitimisho la juu ya kuwa watu kuingia motoni ni kwamba Allah Hana upendo wowote ?

Nilipokosoa Mantiki kama fani pweke, sababu najua logic, logic ina udhaifu wa kuchukua mambo juu juu. Huwezi kujiuliza kwanini watu wameingia motoni ? Ni baada ya nini na nini ?

Mpaka watu wanaingia motoni ni mchakato wa matendo, nia, na kufata mafundisho. Ukiona watu wanaingia motoni ujue huo ni mchakato, ni kwamba walifikishiwa ujumbe wakaukataa, hawakufanya toba muda ambao nafasi ya kufanya hivyo ilikuwepo, walikuwa na uwezo wa kufanya mema hawakufanya bali walikuwa na uwezo wa kutofanya uovu wakazembea.

Sasa kwa kutumia logic yenu kwa jambo kamilifu kama hilo onyesha wapi Lina makosa na halina mantiki kwa maana ya kuleta maana.

Allah akisema ya kuwa atatupa mitihani na hili liko wazi, akupime utasubiri au utakufuru, muda ambao tayari ameshakupa na njia ya kufaulu mtihani huo. Hapa anaonyesha upendo wa hali ya juu alio nao kwa waja wake.

Naam, anajua hayo sababu yeye ni Mjuzi wa kila kitu. Lakini kujua kwake yeye hakukuzuii wewe kufanya unalo taka, sababu ametupa uhuru huo.

Usiseme yanakosa mantiki kwa kuhitimisha juu juu na kutoangalia mchakato mzima.

Sasa nataka uje hapa uonyeshe kutokuwa na maana kwa maneno haya.
 
Nime challenge hoja zako za ushahidi wa uwepo wa Mungu
Badala ya kutetea umekimbilia ku quote mengineyo
Sahihi kabisa, kwenye huja challenge chochote ndio maana nimekuja kwenye hitimisho lako ambalo limetokana na uliyo yaandika huko juu, kwa maana sijapunguza Wala kuzidisha.

Sasa ili nionekane nimefanya hivyo una vyo dai, kosoa hiki nilicho kiandika.

Mwanzo ulisema hivyo hivyo kwamba hoja zako za kwenye post # 1 hazijajibiwa, sio kwamba hazijajibiwa ni nyepesi kiasi ambacho mnatupa uvivu kuwajibu sababu kwanza mnakuwa mmeegemea katika uongo, kwahiyo mnatupa kazi ya kukosoa uongo wenu kisha kukosoa hoja zenu. Hii ni kazi mara mbili.

Lakini kiuhalisia hamna hoja sababu mnae mzungumzia hamumjui bali mmemsikia tu.
 
Kwa nini Quran hiyo isifanyiwe tasfiri (translation) kwa lugha zote duniani ili iweze kueleweka na watu wote?

Kama "Allah" huyo ni Mungu wa binadamu wote, Alishindwaje kuleta Quran hiyo katika lugha zote au Quran hiyo kuweza kufanyiwa tasfiri ili kila mtu aelewe maandiko hayo kiurahisi.

"Allah" huyo, Anajua kabisa watu wapo kwa lugha tofauti lakini Quran hiyo ninyi waislamu mnadai, Haiwezi kufanyiwa tafsiri kwa lugha nyingine tofauti na kiarabu.

Huyo "Allah" kama alitaka tuijue Quran kwa lugha ya kiarabu, Alishindwaje kutuumba binadamu wote ulimwenguni kote, Tuzungumze kwa Kiarabu tu?

Ili iwe rahisi mafundisho yake ya Quran hiyo kueleweka kwa watu wote ulimwengu mzima?
Translation ziko nyingi na watu wanaendelea kufanya hivyo, ila ukitaka ukifaidi kitu kisome katika lugha yake ya asili, ndio maana watu wanajifunza na kujua lugha husika.

Kijana usirudie hoja, Allah bali Amesema katika Qur'an angetaka kuwafanya watu wote wamuamini angefanya hivyo, sio tu katika hili la Kiarabu kwake rahisi sana, lakini katika taratibu zake alizo weka na kwa hekima zake, amejalia kufanya juhudi katika kila jambo. Lazima ufanye ujuhudi katika jambo. Ndio maana hata sisi Wabantu tunafanya juhudi katika kujifunza Kiarabu na tunakijua, kwahiyo hakuna udhuru katika hilo.

Wapi tumedai ya kuwa haiwezi kufanyiwa tafsiri kwa lugha nyingine ? Soma tarjama ya Sheikh Abdallah Salehe al Farsy, hii ni ya Kiswahili, soma ya Ali Muhsin Barwan hii ya Kiswahili, Sasa usiwe unaandika uongo.

Hakushindws kufanya hivyo, bali ndani yetu ametuumba na kutupa uwezo wa kujua ndio maana watu wanajua na wanaendelea kujua. Huu ni utaratibu alio uweka yeye.

Wewe leo hii ukiamua kujua Kiarabu unalijua, kama ambavyo unafanya juhudi katika kuyakua mambo mengine na ukayajua, ni maamuzi tu, kila kitu kipo.
 
Umekosoa lini kuhusu logic zaidi ulijionesha kuwa hujui nini maana ya logic.?

Yaani hata maswali yako na misimamo yako huwa ni illogical,

Nawewe nakuuliza kuwa kati ya dunia na gravity kipi kilianza!?
Sasa usinirudishe katika nukta ambayo niliitolea maelezo ya kina na kutosha nawisho wake ukatokomea.

Kuwa Illogical hiyo ni kwa mujibu wa mtazamo wa logic kama fani kwayo imetengenezewa misingi, ila kiuhalisia si kweli.

Logic (Mantiki) kama fani, ni elimu kwayo humsaidia mtu kutokukosea katika kujenga hoja. Msingi wa logic ni akili, ambayo mtu alikaa akaweka misingi hiyo. Asili yake ni kwa kina Aristoto.

Sasa sijui unataka tuongelee logic gani ?

Jibu kwanza swali nililo kuuliza, kati ya logic. maneno kipi kilianza ?

Swali lako ulilo uliza si swali sahihi, Sasa sijui umefanya makusudi au hujui kama umekosea kuuliza swali hilo. Tumalize hilo kisha nakuja kuonyesha uongo wa swali hilo.
 
Translation ziko nyingi na watu wanaendelea kufanya hivyo, ila ukitaka ukifaidi kitu kisome katika lugha yake ya asili, ndio maana watu wanajifunza na kujua lugha husika.

Kijana usirudie hoja, Allah bali Amesema katika Qur'an angetaka kuwafanya watu wote wamuamini angefanya hivyo, sio tu katika hili la Kiarabu kwake rahisi sana, lakini katika taratibu zake alizo weka na kwa hekima zake, amejalia kufanya juhudi katika kila jambo. Lazima ufanye ujuhudi katika jambo. Ndio maana hata sisi Wabantu tunafanya juhudi katika kujifunza Kiarabu na tunakijua, kwahiyo hakuna udhuru katika hilo.

Wapi tumedai ya kuwa haiwezi kufanyiwa tafsiri kwa lugha nyingine ? Soma tarjama ya Sheikh Abdallah Salehe al Farsy, hii ni ya Kiswahili, soma ya Ali Muhsin Barwan hii ya Kiswahili, Sasa usiwe unaandika uongo.

Hakushindws kufanya hivyo, bali ndani yetu ametuumba na kutupa uwezo wa kujua ndio maana watu wanajua na wanaendelea kujua. Huu ni utaratibu alio uweka yeye.

Wewe leo hii ukiamua kujua Kiarabu unalijua, kama ambavyo unafanya juhudi katika kuyakua mambo mengine na ukayajua, ni maamuzi tu, kila kitu kipo.
Kama Quran ni kitabu cha huyo "Allah" Kwa nini kinafanyiwa Tafsiri (translation) na wanadamu?

je "Allah" huyo aliwapa mamlaka ya kufanya tafsiri ya kitabu chake cha Quran kwa lugha zingine?

Je mna idhini na ruhusa yake huyo "Allah" kufanya tafsiri ya kitabu chake?

Kama mna idhini na ruhusa hiyo ya kufanya translation ya Quran kwa niaba ya Allah wenu,

Je "Allah" huyo Hakujua kwamba anapaswa kuleta "Quran" hiyo katika lugha zote za binadamu wote ulimwenguni.

Yani alifanya kazi nusu ya kuleta kitabu( Quran)kwa lugha moja, wakati anajua binadamu wana lugha nyingi, kisha kazi ya kutafsiri "Quran" hiyo akawa achia nyie mmalizie?

"Allah" huyo ana ji contradict tena yeye mwenyewe...😄😄
 
Uwezi kuwa na akili za kufika mbali kama huwezi kufirikia ,lazima ujiulize maswala hao wanagunduzi wote kweny tafiti zao walianza kwa kujiuliza maswali ndio wakaanza kufanya tafiti.

Kwa vile hauna hoja sioni tatizo😂😂
Wewe umelenga kipi katika mjadala tulio nao?

Hoja yako iko wapi?

jua kwa nn lina ratiba kila siku na hakuna anayezunguka hiyo ratiba kila siku.... Binadamu alianzaje maisha hapa duniani? Je dunia ina miaka mingapi mpaka sasa ukiachana na hii 2023?
Kutokujua kitu, inathibitisha tu kuwa huna knowledge ya kitu hicho, na sio kwamba Mungu yupo.

Hata kama sifahamu mambo haya haithibitishi kivyovyote vile habari za Mungu huyo.

Watu waliamua kutunga jibu jepesi ili kuwafanya kuwa comfortable tu.

Na ndiyo maana huwezi kuthibitisha kama Mungu yupo, zaidi utatumia madai hayo hayo kwamba umethibitisha!!.

Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo nje ya hadithi na mawazo ya waamini tu.

Na unaweza kupinga jibu la Mungu kwasababu linakosa logic.

Yani ni sawa na mtu akuambie kuwa Square root ya namba 5 ni 15.

Hapo hainihitaji mimi kujua square root ya namba 5 kukataa kuwa namba 15 si square root ya namba 5.

Kwasababu najua square root ya 5 lazima iwe ndogo kuliko 5.

Sawa kabisa na dhana ya Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ambae aliumba ulimwengu huu wenye kuruhusu mabaya!
 
Mungu yupo hata utoe mifano ambayo haipo ila ukweli Mungu yupo mratibu wa mambo yote...
 
Kuongelea kwako dhana ya Mungu kwa ujumla no ujinga na uvivu wa kufikiri sababu lazima ukosee kama ulivyo kosea hapa. Huwezi kumuongelea Ng'ombe kuwa ni Mungu wakati Mungu ili awe Mungu lazima awe na sifa zake anuani.

Hapo ulitakiwa ujue unajadiliana na mtu wa aina gani kisha ujenge hoja kwa mtizamo wake. Ulipaswa ujadiliane na Mimi kwa mujibu wa Mungu ninae muamini Mimi, na ukijadliana na Mhindu hali kadhalika.

Amemkubalia sababu amemuomba, na angetaka asinge mkubalia bali amefanya hivyo kwa hekima na kuwatahini waja wake. Lakini hakutuacha hivi hivi alitutahadharisha juu ya Shetani, maana ukishawishiwa na Shetani ujue hiyo ni hiari yako. Kwa maana hiyo chochote utakacho kihoji hapo hakiwezi kuwa na nguvu, sababu ya uwepo wa Uhuru wa kuchagua.

Naam, lakini Adamu na Hawa walipewa onyo na ndio maana Allah akawatoa, maana yake walizembea wenyewe. Duniani unapata vyote, huwezi kuishi katika huzuni maisha yako yote au katika raha, bali duniani ni mapito ndio maana Kuna kufa, Kuna kufufuliwa na kuna kulipwa.

Aya zako za mwisho hakuna hoja uliyo iweka hapo zaidi ya malalamiko, hata wakiwa zaidi ya hizo asilimia ulizo zitaja, ukweli unabaki pale pale ya kuwa wamepotezwa kwa kutaka wenyewe kupotezwa.
Okay kulikuwa na uwezekano wa kutoletea huyo shetani? If so, why hajafanya hivyo...plus unajua dhana ya shetani ni rahisi Sana kudisprove...watu wameona Mungu wao mzuri hawezi kupewa lawama za mabaya so wamemtengenezea jambazi apigane na sterling wao...it's utter childishness
 
Sahihi kabisa, baada ya kuona hilo, huwa tunaenda mbali na kujadili ukweli wa hicho kinachodaiwa au kusemwa.

Mfano katika hayo maswali niliyo yaweka, Kuna uongo gani ? Jifunzeni kujadili hoja na si kukimbia hoja.

Kwamba je Dunia imeumbwa na sisi ? Au Dunia imetokana pasi na chochote ? Kumbuka haya yamenukuliwa natu ambaye hajui kusoma Wala kuandika. Kwa mwenye akili lazima atakiri ya kuwa hili si la kawaida.

Kujibu kwako maswali hayo na kutokujibu kwake kunaonyesha ya kuwa Mola yupo na Dunia hii imeumbwa.

Kuendelea kwa nchi sio lengo la sisi kuumbwa na hakimfanyi mtu awe sahihi, sababu Mola wetu huwa anawaruzuku mpaka watu waovu bali mpaka wanao mtukana na kumkana.

Jaribu kujenga hoja kijana.
Dunia tufanye imeumbwa, why does it have to be an Arabic god Allah....why asiwe Zeus, why asiwe brahma, why asiwe Yahweh, why asiwe Odin, Hilo ndo swali langu....coz kila dini inakimbilia kusema bana Mungu wetu kaumba kila kitu so muabudu or else, or else wat...🤣wat evidence do u have...
 
Hii sio kweli, bali hiki ni kichaka ambacho huwa mnajifichia wakana Mungu na hii inaonyesha ya kuwa mnapinga mambo ambayo hamna elimu nayo.

Mara nyingi anae kanusha ndio hutangulizwa sababu hudhaniwa ya kuwa ana elimu zaidi juu ya jambo hilo, na mara chache anaye kiri hutangulizwa.

Sisi tunakiri ya kuwa Mola yupo kwa sababu nyingi sana, zipo sababu za kiakili, za kimazongira na ufunuo. Sasa wewe ambaye unakuja na kusema ya kuwa "Mungu hayupo" unapewa nafasi kubwa ya kuthibitisha sababu unakuwa unaenda kinyume na Uhalisia, yaani unapingana na akili, unapingana na mazingira na unapingana na ufunuo.

Sasa hakuna mlango wa nyinyi kutoka katika kuwajibika kuthibitisha juu ya kutokuwepo kwa Mola.

Twende kazi.
Hamna evidence...is as simple as that...🤣
 
Back
Top Bottom