Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Kwa nini Quran hiyo isifanyiwe tasfiri (translation) kwa lugha zote duniani ili iweze kueleweka na watu wote?Kwanza Allah ndio ameumba ndimi za watu, katika surat al Insaan amegusia hilo, ya kuwa ameumba mataifa na makabila mbali mbali lengo tupate kujuana.
Kwahiyo Allah ndie ameumba lugha na mataifa, na haongei Kiarabu, bali Allah akituma mjumbe sehemu anampa ujumbe kwa lugha yakez ndio maana Ibrahim aliongea kwa lugha yao, Musa, Yesu na kadhalika Mtume aliongea au kupewa ujumbe kwa lugha ya Kiarabu sababu alianza kuzungumza na watu wake kwa lugha hiyo, vipi Mtume awe Muarabu halafu apewe ujumbe kwa Kisukuma na watu wake wanaongea Kiarabu ?
Allah anaeleweka kwa lugha zote, ndio maana tunamuomba na kumsoma. Lakini lugha sio kikwazo kama ukiamua kujifunza, na ukianalgalia lugha ya Kiarabu ni tofauti na lugha nyinginezo bali husemwa lugha hii ni ya watu wote na ushahidi uko wazi, ukisoma Historia ya fani za Kiarabu utakuta wasomi wa kubwa wa lugha hii Ulimwenguni kote si Waarabu kiasalia, lakini tafuta lugha nyingine hilo hulikuti. Tukiongelea katika mlango huo hakuna lugha kuishinda Kiarabu.
Kujua Kiarabu ni lazima kama ukitaka kujua Dini hii, sababu imekuja kwa lugha ya Kiarabu. Lakini hakuna aliye zaliwa anajua, hata wewe Leo hii umezaliwa hujui kusoma Wala kuandika lakini umesomeshwa na ukajua. Sasa kwanini hili hulisemi ? Leo hii ulienda Saudia utakuta Waafrika wanawasomesha Waarabu Kiarabu,maana yake nini ? Hii ni elimu Haina wenyewe ukitaka kujua unajua ukizembea ni wewe na uzembe wako.
Hajashindwa kufanya hivyo, bali angetaka sote tumuamini tunge kumaini kama ilivyo nukuliwa hivyo katika Qur'aan, ila amefanya haya na kuweka hali wezekano za kujua ambayo wewe unayadai ukitaka. Mola wetu hapendi watu wazembe.
Kama "Allah" huyo ni Mungu wa binadamu wote, Alishindwaje kuleta Quran hiyo katika lugha zote au Quran hiyo kuweza kufanyiwa tasfiri ili kila mtu aelewe maandiko hayo kiurahisi.
"Allah" huyo, Anajua kabisa watu wapo kwa lugha tofauti lakini Quran hiyo ninyi waislamu mnadai, Haiwezi kufanyiwa tafsiri kwa lugha nyingine tofauti na kiarabu.
Huyo "Allah" kama alitaka tuijue Quran kwa lugha ya kiarabu, Alishindwaje kutuumba binadamu wote ulimwenguni kote, Tuzungumze kwa Kiarabu tu?
Ili iwe rahisi mafundisho yake ya Quran hiyo kueleweka kwa watu wote ulimwengu mzima?