Uongo uliniponza

Uongo uliniponza

2004boy

Member
Joined
Jul 23, 2024
Posts
53
Reaction score
89
Habarini wakubwa natumai mu wazima.

Kwenye maisha yangu huwa najitahidi sana nisionekane muongo ila hapa ilinibidi nidanganye ili nipate ninachokihitaji.
Nikiwa na miaka 18 nilimpenda binti mmoja nilianza kumfuatilia taratibu nikagundua anapoishi ilikuwa ngumu Sana kutoka nje na nyumbani kwao nikawa namuvizia angalau nimuombe namba tu sikufanikiwa mwisho nikakata tamaa.

Baada ya wiki moja yule binti ilikuwa Kama bahati tulikutana dukani mimi nilikuwa napiga stori na rafiki yangu pale dukani yeye alikuwa kafata simu pale.

Nikaona hii ni kama bahati nikaongea nae nikamuomba namba akanambia hana simu, simu aliyonayo ni ya mama yake. Nilikuwa nampenda mpaka nakosa ujasiri wa kumtongoza live.

Niliachana nae nikaenda nyumbanI ilikuwa najua kabisa simu aliyokuwa nayo ni ya kwake niliumia Sana aliponinyima namba. Sikukata tamaa niliendelea kumfukuzia baada ya siku tatu tulikutana tena, cha ajabu kabla hatujaongea chochote akaniomba simu yangu nikampa baada ya mda kidogo akanirudishia akasema kwamba hii ndo namba yangu.

Nilihisi Kama naota tuliagana pale kila mtu akaenda zake. Nilianza kumtongoza nikawa nachat nae kila siku nikamwona Kama ameshanikubali tayari, ilikuwa haipiti siku bila yeye kunitafuta.

Nikamwomba papuchu akaniuliza kwamba toka uje huku ushawahi kuwa na mpenzi kabla yangu?. Nikafikilia nimjibu jibu gani nikaona nikisema hapana ataniona mshamba wa mapenzi, nikamdanganya kuwa nilishawahi kuwa na mpenzi japo sikuwahi kuwa na mpenzi, kabla yake.
Baada ya kumwambia hivyo tu nikawa namtumia sms hajibu nilijilaumU Sana nilitamanI hiyo mesejI niifute nirudie kuiandika huo ndo ukawa mwisho wetu yule binti.

Alienda shule akawa hapatikani kwenye simu na mimi nilihama Morogoro nikahamia Mwanza ila mpaka leo hii huwa nawasiliana nae ila huwa sizungumzii kuhusu mapenzi.

Lakini Bado nampenda, ila maamuzi nimemwachia yeye mwenyewe akiona ninamfaa ataniambia akinipotezea sawa tu. Lakin haniombagi hata hela ya vocha mpaka nijipendekeze kumpa Mimi mwenyewe.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom