Uongo wa Historia ya Afrika na Waafrika itajibiwa na muafrika

Uongo wa Historia ya Afrika na Waafrika itajibiwa na muafrika.
........
...Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU iliyokwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM ambacho kinalitafuna taifa leo..
.
mpaka hapa nimecheka mwenyewe
 
Uongo wa Historia ya Afrika na Waafrika itajibiwa na muafrika.

Na: Yericko Nyerere

Binafsi nimejipa utaratibu kuwa vitabu vinavyohusu uafrika na waafri sitavitilia mkazo sana vile vilivyoandikwa na wazungu bali vilivyoandikwa na Waafrika wenyewe! Mfano ukisoma historia ya Mkwawa iliyoandikwa na wazungu wanasema mkwawa alijiua kwakujipiga risasi,

Ukweli wa historia ya kiafrika wazungu waliona aibu kusema walimshindwa Mkwawa, Mkwawa hakujiua bali aliwatoroka wazungu na kuelekea Songea ambapo alifia milima ya Lukumbulu kwakuliwa na Simba baada ya kuugua akiwa milimani peke yake. Nimpongeze kamanda Godwin Mwesiga huyu ni mtafiti wa mambo ya kiafrika na uafrika wetu.

Ni rahisi sana Vijana wa leo kuwadhalau wazee wanaokutana nao barabarani na kuwaona watu wasio na Elimu wakiaminishwa kuwa elimu ilianzia magharibi, Cha ajabu Ahmed Baba (1556-1627) karne ya 16 aliandika vitabu 60.Ni mingoni mwa wasomi wa Phd katika ufalme wa Mali.

Ni vizuri watu tuyasake maarifa kwakutumia maarifa, na kwakutokujua historia yetu Waafrika tumelidhika Bara letu la Afrika na yale machache tunayoyafahmu, tukidhani wazungu ndio wasomi wa mwanzo duniani kumbe wapo waliofanya mapinduzi makubwa katika Africa,ila wamefichwa na historia za kigeni zinazofundishwa mashuleni.

Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......Pamoja na kwamba 1927 Gavana Sir David Cameron kupiga marufuku mtu mweusi kukanyaga mjini (posta ya leo) hasa kwenye sherehe za wazungu ambazo zilikuwa maranyingi zinafanyikia ukumbi wao pale makao makuu ya NBC leo,

Gavana huyu aliwaundia chama cha kuratibu sherehe za weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu mateka wa vita vya kwanza vya dunia toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwakil Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya)huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwakil Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU iliyokwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM ambacho kinalitafuna taifa leo..

Hili ndio chimbuko la AA, TAA, TANU na hii CCM.

SITALALA MPAKA PALE WATAWALA WA AFRIKA MASHARIKI WATAKAPOBADILISHA MAJINA YA MITO, MAZIWA, MILIMA YA WAZUNGU NA KUYAITA MAJINA YA KIKWETU.
 
Mitaala LAZIMA Ibadilishwe. Hatutaki kuwarithisha watoto wetu maneno ya Kilongolongo kama alivyokasema Mr Ebbo. Ondosheni Maneno mbofumbofu.
 
Lakini mwisho wa siku Mapambano ya TANU dhidi ya ukoloni yalifanikiwa chini ya uenyekiti wa Nyerere na ndo hapo dhana ya Nyerere kutajwa kama alfa na omega wa historia ya TZ na sio kwamba hao wengine akina sykes history zao hazpo hapana zpo wazi kabisa
Du pamputi ni binge la tusi kwetu
 
Lakini mwisho wa siku Mapambano ya TANU dhidi ya ukoloni yalifanikiwa chini ya uenyekiti wa Nyerere na ndo hapo dhana ya Nyerere kutajwa kama alfa na omega wa historia ya TZ na sio kwamba hao wengine akina sykes history zao hazpo hapana zpo wazi kabisa
Pamputi,
Tatizo halipo katika kumtaja Mwalimu Nyerere katika historia ya
TANU na harakati za uhuru.

Tatizo lipo katika kumtaja Mwalimu Nyerere peke yake na kuwaacha
wazalendo wenzake waliokuwa katika kupambana na ukoloni kwanza
kabla yake na kisha wakiwa pamoja.

Ukiwa utaielezea historia ya TANU ukidhani unaweza ukaikamilisha bila
ya kuwataja akina Sykes utakuwa imeipunja historia pakubwa sana kiasi
cha kunyofoa nusu karne ya historia ya Tanganyika.

Historia ya Abdul Sykes haikufahamika popote hadi nilipoiandika na kitabu
kuchapwa London mwaka wa 1989 na ilizua tafaruku kubwa katika duru
za ndani ya CCM na kwa baadhi ya wasomi nchini.

Hapana haja ya kurudia kwani hili hapa barzani tumelizungumza sana na
wachangiaji wengi wemetoa mawazo yao.

Mwalimu Nyerere asingeweza kufanikiwa chochote katika Dar es Salaam
ya miaka ya 1950 bila ya kuungwa mkono na wenyeji aliowakuta katika
siasa.

Mwalimu Nyerere hakuja na chama wala hakuwa na fedha za kuanzisha
chama achilia mbali kuwa na watu wa kumsikiliza.

Chama alikikuta pale New Street kikiwa na viongozi na wanachama na fedha
za kuendesha harakati zilikuwa katika mikono ya John Rupia, Dossa Aziz
na Abdul na Ally Sykes.

Hata TANU ilipoasisiwa kadi za kwanza 1000 zilichapwa na Ally Sykes kutoka
mfukoni kwake na kadi namba moja Ally Sykes alimwandikia Rais wa TANU
Julius Kambarage Nyerere, kadi na namba 2 yake mwenyewe na kadi na. 3
akamwandika kaka yake Abdulwahid Kleist Sykes nk. nk.

Si hilo tu hata usanifu wa kadi ya TANU kuweka mwenge na rangi ya kijani
ilikuwa kazi ya Ally Sykes kwa kudurufu kadi yake ya Tanganyika Legion,
askari wa zamani wa KAR waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Ukipenda kujua habari hizi kwa kirefu msome Judith Listowel, ''The Making
of Tanganyika (Chato and Windus 1965).

Gari ya kwanza ya TANU alitoa Dossa Aziz kusaidia harakati za kudai uhuru.
Abdul Sykes akaishi na Mwalimu Nyerere nyumbani kwake baada ya
Mwalimu kuacha kazi ya kusomesha.

Mzee Rupia akamtafutia Nyerere nyumba Magomeni na hapo ndipo akahama
kwa Abdul Mtaa wa Aggrey na Sikukuu kwenda kwake.

Chuo Cha Kivukoni wamejaribu kuandika historia ya TANU bila ya kuwataja
wenye TANU yao sasa shuhudia leo jinsi walivyokuwa kichekesho katika duru
za utafiti wa kisomi.

Nakuwekea picha iliyopigwa mwaka wa 1933 siku ya ufunguzi wa jengo la AA
New Street, Dar es Salaam.

R0O9cyepr_vtPWmquvovAv1JLLA_pdABYQBEb4aouD8-r4QA5I5Ypu3x_kFLgUjEIkUJFuXXQ_5SMt92mLgjnn3i1oN5Q2i7OEisMAx1GVmyThLNZsQzM6oCxMgJGFvnaENpEmMcTw8G4przL9ZnaPgFpxRuta3Z0CqbOWvlll_7bUrwTcXpxRuqrID1lhtJOmk8pXeP-JZh9r1rBDc7l6Qs1OU7EtO1y979Vn8ippAChJUcp1kFgE5i5YF7EWoskIpnrpCPPGYSR8HyFG5vNq96pNCIAJQitpurjD9LK-GFbbYtSPsgHUTUhbiK1vI4PcLBfiyniejYx6D0mr9ygrYv_Jd8_F0hcUyHkVLjs4cK7CjUMVQUsAA7Pl6Ar8SlDYIrMprd8IlcV3h33IbQpAx8DzlE7jw7pbbXkkoVPcQnpk8_ufyRd0vIidd7xwh2gR3HBz5uft3tlKGwCN4GsuTf_UWHAd9ijor0IicImFSKsq4qSFHGkvnGhPQJIMyWPZm4pdQjKV0uu_wDcWxrb2mRdyHr39kN0_DmC7lY4MTYwaFSs8L24Bao3O8xGLUtb2u-iICjyOAWMFwZbmmRkT0f4cH_7XMH=w876-h657-no
 
Ilikuwa mwaka 1927 ndipo chama cha AA kiliundwa, kikawa kinafanyia shughuli zake nyumbani kwa Rais wa kwanza wa AA Bwana Cecil Matola, na miaka mitatu baadae, yaani 1930 ndipo wakapata jengo toka kwa Gavana Donald Cameron, hapo ndipo picha hii ilipigwa,

Mwaka 1933 Cecil Matola alifariki dunia, na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa AA bwana Klest Sykies mpaka mwaka 1948 chama kilipobadilishwa jina nakuwa TAA, Rais wake wa kwanza wa TAA akawa Daktari Vedasto Kyaruzi, na katibu akawa Abdulwahid Klest Sykies, miaka miwili baadae, Dr Kyaruzi alihamishiwa Kingolwila hivyo nafasi ya urais wa AA ikakaimiwa na Abdulwahid Klest Sykies hadi ilipofika uchaguzi wa 1953 ambao Julius Nyerere alimshinda Abdulwahid Klest Sykies kwakishindo na kuwa Rais wa TAA, Mwaka mmoja baadae TAA ilibadilishwa jina nakuwa TANU................................................................

KITABU cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi sasa kinapatikana naeneo yafuatayo kwa Dar.

1. Duka la House of Wisdom lilipo Posta Mtaa wa Samora Jengo la NHC ghorofa ya Kwanza.

2. Dar es Salaam Bookshop lipo Posta mtaa wa Makunganya karibu na Klab ya starehe Bilz,

3. Imalaseko Supermarket iliyopo Posta mtaa wa Pamba mkabala na ATCL.

Bei kwa jumla ni 25,000/= na rejareja ni 30,000/=

Kwa waliopo nje ya Tanzania unaweza kununua nakala laini katika mtandao wa Amazon product ASIN B01GPXFDB6
Kwa mawasiliano zaidi piga simu.

+255759349954, +255715737332, +255655668204

Hivi historia hasa ya tanzania tunaipata wapi?

20151219_124737.jpg
 
Akisema haya Mohamed Said mnakataa, mnamuita mdini, akisema Yericko eti tumetoka mbali bullshit.
Yule analazimishaga hoja! aungwe mkono kwa nguvu! na kuona yeye ndiyo mjanja tuuu! msomi aliyetukuka! kuumbee!
 
KITABU cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi sasa kinapatikana naeneo yafuatayo kwa Dar.

1. Duka la House of Wisdom lilipo Posta Mtaa wa Samora Jengo la NHC ghorofa ya Kwanza.

2. Dar es Salaam Bookshop lipo Posta mtaa wa Makunganya karibu na Klab ya starehe Bilz,

3. Imalaseko Supermarket iliyopo Posta mtaa wa Pamba mkabala na ATCL.

Bei kwa jumla ni 25,000/= na rejareja ni 30,000/=
Mbona umetaja wa Dar es salaam tu, huko mikoani kwani hawajui kusoma? Dharau hizi? hata jimbo lako umelisahau! Ubaguzi tu na Matumizi mabaya ya wana darisalama, unawatumia tu km ngazi ya kupanda kwenye kilelel cha mafanikio imeniudhi sana hiii.

Duka la........ duka laa.......... duka laaa mfyuuuxxxc
 
Kinachochekesha, ni kujaribu kuandika
inayoitwa Historia kwa kunakili maandishi ya wengine kwa kuyapunguza na kurekebisha yaendane na matakwa yako.

Historia ni utafiti, na kuhojiana na walioidiriki. Sio kukaa ndani na Laptop kuunganisha maandishi.

Kuandika na kwenda kuchapisha mwenyewe kwamba hiki ni kitabu cha Historia ya nchi!

Asilani hakiwezi kuwa marejeo ya kutegemewa labda iwe kwa kutafuta pesa za kuuza nakala.
 
Tofautisha kuona tu kwa macho na kuugundua.
Kugundua kitu ni pamoja na kuugundua asili yake.
Nadhani inajieleza wazi wazi. Ni vizuri kupata historia ya Afrika toka kwa waafrika wenyewe. Lakini si kila kitu kitakuwa sahihi. Historia iliyoandikwa na wazungu ina mapungufu mengi sana. Lakini yapo machache yaliyo sahihi. Hoja zipingwe kwa hoja mbadala.

Kwa mfano, kusema mzungu fulani alikuwa binadamu wa kwanza kuliona ziwa fulani ni upuuzi. Kupinga hilo, inapasa kuonyesha kuwa wenyeji walikuwa wakiishi na kutumia ziwa hilo miaka mingi kabla wazungu hawajafika !
 
Kama Mkwawa alikufa peke yake porini kwa kuliwa na simba, ina maana lile fuvu lake ambalo tuliambiwa kuwa lilipelekwa Germany ni "fake"? Kwa hiyo watalii wanaoenda Iringa kuliangalia "fuvu" la Mkwawa wanatapeliwa!
Mbona hoja ya fuvu haijibu
 
Nimepapenda sn kwenye historia ya TANU,ila hapo kwa mkwawa napata shida kukuamin? Vipi lile fuvu pale kalenga? Kwa mujibu wa wale watoa historia mkwawa baada ya kuuwawa alitembezwa kalenga yote,ipamba,iringa,hadi ubena ili kucreate fear kwa wote wahehe na wabena na ndo ukawa mwisho wa vita.
Yaap!!!,hata mimi napata ukakasi kwenye ishu ya fuvu.
 
Back
Top Bottom