Uongo wa karne huu: Mwanamke sura! Tabia inatengenezwa

Uongo wa karne huu: Mwanamke sura! Tabia inatengenezwa

MEKADDISHKEM

Senior Member
Joined
Sep 15, 2016
Posts
148
Reaction score
144
MWANAMKE SURA BANA! TABIA INATENGENEZWA!

Nimekua nikiwasikia watu wengi wakisema, "Uzuri wa mwanamke sio sura wala umbo bali ni tabia". Wengine wameenda mbali kiasi cha kuwaasa vijana wanaojiandaa kuoa ya kwamba wasiangalie sura wala umbo bali waangalie tabia.

Jamani...

Sijui hii dhana watu wameitoa wapi. Mbona Biblia iko straight sana katika hii ishu ya kwamba unapochagua binti wa kumuoa, sura na umbo ni factor ya kuzingatia? Najua nishawashtua watu hapa. Sasa ngoja nikupe facts za kisaikolojia kabla sijaelekea kukupa statistics ya ninachokueleza from the Bible.

Kisaikolojia iko hivi....

1). Sura na umbo la mwanamke linaweza kubadilika kwa asilimia 5 hadi 50 pekee katika maisha yake na vipo vitu huwa havibadiliki kabisa ukifika umri fulani. Hata hivyo, tabia ya mtu inaweza kubadilika kwa asilimia 100 kutoka na kuelekea upande wowote.

Unaijua implication yake hapa? Ni hivi:- Unaweza kumuoa kahaba na akaja kubadilika na kuwa mtakatifu. Lakini kama hupendi wanawake wafupi na ukajilazimisha kumuoa mfupi eti kwa sababu ana tabia nzuri, you are finished!

2). Kiasili ni kwamba, ndani ya sekunde 15 za kwanza mwanaume anaouwezo wa kumtazama mwanamke na kubaini umbo lake (nje ndani) kwa asilimia 95, lakini anaweza kugundua tabia ya mwanamke huyo kwa asilimia 0.05 katika sekunde hizo.

Tunaenda wote? Hii pointi inaonesha kwamba mwanaume huamua nani "anavutia", kwa kuangalia kwanza mwonekano na huamua nani amuoe kwa kuangalia tabia. Kinachofanya mwanaume aendelee kuvutiwa na mwanamke ni mwonekano na kinachofanya ampende ni tabia. Kuvutiwa huwa kunaanza, kisha upendo hufuata (rudia hii sentensi, usije dhani nimekosea).

Did you know kwamba, furaha ya mwanaume inakaa katika mvuto wa mwonekano wa mwanamke na amani ya mwanaume inakaa katika tabia ya mwanamke? Inakuingia? Huwezi kuwa na amani kama huna furaha (rudia mara nne hii sentensi). Umeirudia? Enhee, umegundua nini? Sijaacha watu kweli hapa?

Twende mbele zaidi...

Naomba nikuoneshe statistics za waoaji katika Biblia, ndipo utaelewa umuhimu wa sura na umbo kwa mwanamke "kwa usalama wako". Right?

1). Unakumbuka cha kwanza kilichomvutia Adam alipomuona Eva for the first time? Je, aliangalia tabia? Hapana! Angeijuaje tabia ya mwanamke ambae ndio katoka kumuona sekunde hiyo hiyo? Je, alisema, "Ohoo, Eva wewe unaheshima sana?", ama mwenzangu unepaona aliposema "Wawooo we mwanamke Eva unawathamini ndugu zangu!". Labda mimi Biblia yangu haifanani na yako. Kwani kuna mahali huko kwenye Biblia yako pameandikwa Adam alisema, "Ohoo, Eva unajua kupika vizuri!"? Mi ninachojua ni kwamba Adam alipozinduka na kufumbua macho, alikiona chombo kilichoumbika pembeni, sura ya mvuto, umbo matata, na yaliyomo yakiwa yanaita, ndipo akatamka maneno aliyotamka ya kwamba, ".....huyu atakua mke wangu". Mi sijasema Eva hakua na tabia njema, lakini ndugu yetu Adam alituonesha kitu, au sio?

2). Unamfahamu aliendika kitabu cha Esta? Kwa taarifa yako alieandika ni Roho Mtakatifu kupitia uvuvio wake. Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini Esta alisifiwa sana kwa uzuri wa sura na umbo kuliko tabia yake? Sijasema Esta hakua na tabia njema, ila nataka uone kwamba, kumbe Roho Mtakatifu anajua kuwa wanaume wameumbiwa kutopuuza ishu ya sura na umbo. Unajua kwa nini nakwambia hivyo? Si unajua Esta alikua amewekwa kwa misheni maalumu ya kuolewa ili awaokoe Waisraeli dhidi ya hila za Hamani? Sasa unadhani Esta angekua mbaya wa sura na umbo, Mfalme Ahasuero angevutikaje kuoa? Tafadhali usikubali kukaririshwa atii!

3). Hivi unazikumbuka skendo za Ibrahim na mtoto wake Isaka? Ibrahim alikua fundi wa kuchagua, asikwambie mtu na akamrithisha hadi mwanae Isaka. Mke wa Ibrahim (Sara) alikua mzuri wa sura na umbo kwa kiasi ambacho kila alipoingia alikua anatikisa. Mke wa Isaka ndio usiseme, alikua mzuri kwa kiwango ambacho habari zake zilisambaa nchi nzima. Kasome Biblia yako. Hivi unataka uniambie wewe ni wa kiroho sana kushinda Ibrahim na Isaka kiasi kwamba unatuzuga kwamba eti suala la kuoa sio la kuangalia sura wala umbo? Ahaaa, bana, hebu acha kutufanyia kanyaboya wenzio, heeee!

4). Umeshawahi kuifuatilia habari ya jamaa yetu Mfalme Daudi namna alivyotegwa kwa mwanamama Abigaili? Karudie hii habari utaona namna ambavyo sura na umbo la Abigail lilivyomchanganya Daudi hadi akaghairi kwenda kufanya timbwili alilopanga. Kwa taarifa yako, maamuzi ya Daudi kumuoa Abigaili hakuyafanya eti baada ya mumewe kufariki, bali aliyafanya siku ile ile aliyomuona. Sasa utaniambiaje kwamba eti usiangalie sura wakati makamanda wa Yesu kama akina Daudi hawakucheza mbali na hicho kigezo?

Nimekuchanganya?

Pooooleeeee bana. Actually, ningeendelea kukuletea statistics nyingi zaidi ila nafasi inakaba. Wapo wengi mie nimewafuatilia, hakuna alieoa kizembe, bali wote walioa "vifaa vya hatari". Kama unabisha kaangalie vigezo alivyokua anatumia Mfalme Suleman kupata wake zake, utapenda! Kamcheki Boaz jinsi alivyompima Ruthi, utanipa tano! Ila najua umenipata-pata japo kidogo, au sio? Basi, mwayego, hebu tufunge na pointi hizi hapa:-

1). Kijana wa kiume:- Kama unaona mie nakushauri hakikisha unajitwalia mke mwenye vigezo vyote viwili. Mvuto wa sura na umbo pamoja na tabia. You know what? Sura na umbo ni kazi yako kujichagulia, ishu ya tabia na ya mbele ndipo atakusaidia Roho Mtakatifu kujua zaidi. Kushikilia "swaga" za kwamba, ohoo, siangaliii sura na umbo bali naangalia tabia, shauri yako nakwambia!

Achana na makelele ya kwamba ohoo maumbo ya wanawake huwa yanabadilika huko mbele. Eboo, Sasa kama huwa yanabadilika ndio ubebe mradi yeyote? Hebu tafuta kitu ile roho inapenda, ambacho Roho mtakatifu anakupa amani nacho, then hayo mambo ya kubadilika, sijui nini na nini, ni mbele kwa mbele! Shida ni kwamba kuna watu wamezidi mno kuwatisha vijana wetu kuhusu hizi ndoa, wakati ishu yenyewe ni simpo kinoma!

2). Mabinti:- Nikisema uzuri wa sura na umbo wala usiwaze. Uzuri wa mtu umo machoni pa anaemtazama. So, wewe mweusi unaweza kuwa mbaya machoni pa anaependa weupe, but ukikutana na wanaopenda weusi, wewe ni mrembo balaaa! Asikutishe mtu na vigezo vya jumla!

3). Kina mama:- Binti ambae hujaolewa endelea kujiweka sopu-sopu, maana mwonekano wako una umuhimu sana katika kuonekana kwako. Mwanamke ulieolewa, wewe ndio kabisaaaa. Hebu jitahidi kumaintain usopu-sopu, maana mvuto wako ndio furaha ya mumeo.

4). Wanaume mliooa:- Tabia ya mwanamke ni matokeo ya inputs zako kwake, lakini sura na umbo lake ni inputs za Mungu kwake. Mungu hakushikii bunduki kuoa, so, kupata kifaa bomba ni ni umakini wa mwanzoni ila kuendelea kufurahia ndoa ni inputs unazofanya. Ndio maana kwenye tabia, mke unaweza kuona alikua anakutii lakini sasa hakutii tena ama kawa mkorofi. Lakini mkeo kama ni mrefu wa futi tano, atabaki kuwa mrefu wa kimo hicho iwe atazaa ama hatazaa. Msitake niseme mengi, nyie watu wazima bana! Tehee! Tehee!

Kwa herini.....

kutoka kwa
[HASHTAG]#SmartMind[/HASHTAG]

Albert Nyaluke Sangaj
 
unanikumbusha enzi napiga gambe, nikifika hata simsalimii, naagiza ya kwanza, ya pili, ya tatu, naanza kumuangalia kwa nyuma akisepa, ya nne namuuliza kinywaji anachotumia ya tano, namkaribisha mezani nampa maneno na mi ahadi kibao, anapiga mbili tatu, ya sita, nakumbuka kesho natakiwa niwahi kazini, nalipa, namlipia kisha nasepa, na yeye huyoo anaenda kwenye meza ya mlevi mwingine
 
unanikumbusha enzi napiga gambe, nikifika hata simsalimii, naagiza ya kwanza, ya pili, ya tatu, naanza kumuangalia kwa nyuma akisepa, ya nne namuuliza kinywaji anachotumia ya tano, namkaribisha mezani nampa maneno na mi ahadi kibao, anapiga mbili tatu, ya sita, nakumbuka kesho natakiwa niwahi kazini, nalipa, namlipia kisha nasepa, na yeye huyoo anaenda kwenye meza ya mlevi mwingine
Siku hizi umeacha? If yes, Nipatie maujanja uliyotumia ili na mie niache
 
Siku hizi umeacha? If yes, Nipatie maujanja uliyotumia ili na mie niache
sijui kama nimeacha ama nimepumzika, ila nina miaka miwili na nusu sasa situmii.....pia nilianza kitambo kidogo nikiwa darasa la tatu...hivyo nina kila sababu ya kujipumzisha
 
sijui kama nimeacha ama nimepumzika, ila nina miaka miwili na nusu sasa situmii.....pia nilianza kitambo kidogo nikiwa darasa la tatu...hivyo nina kila sababu ya kujipumzisha

siku nilipoacha nilienda kumzika mzee mmoja hivi huko bush, sasa kuna shehe alikuwa akitoa mawaidha, utadhani kalipwa aniseme mimi, kila analosema linanihusu, aidha nimesha fanya si chini ya mara 1000 ama ndio nilikuwa na mpango nikitoka mazishini nikafanye, nikaona isiwe tabu huyu shekhe maneno yake ngoja niyafanyie kazi, pale pale, nikaacha, nahii, nikaacha nanihii, nikaacha na nanihii pia, na hivi naelekea masjid..ila nanihii ndo siwezi acha aisee
 
Hongera zake mme wangu kwa kuchagua mke mwenye sura nzuri umbo zuri na tabia nzuri. Daaah mme wangu ana bahati sana ..
 
Weka picha acha longolongo
Hongera zake mme wangu kwa kuchagua mke mwenye sura nzuri umbo zuri na tabia nzuri. Daaah mme wangu ana bahati sana ..
nakusaidia.
drawn-baby-animal-marker-eyebrow-12.jpg
 
sijui kama nimeacha ama nimepumzika, ila nina miaka miwili na nusu sasa situmii.....pia nilianza kitambo kidogo nikiwa darasa la tatu...hivyo nina kila sababu ya kujipumzisha
aiseee darasa LA 3 ¿??? makubwa haya
 
siku nilipoacha nilienda kumzika mzee mmoja hivi huko bush, sasa kuna shehe alikuwa akitoa mawaidha, utadhani kalipwa aniseme mimi, kila analosema linanihusu, aidha nimesha fanya si chini ya mara 1000 ama ndio nilikuwa na mpango nikitoka mazishini nikafanye, nikaona isiwe tabu huyu shekhe maneno yake ngoja niyafanyie kazi, pale pale, nikaacha, nahii, nikaacha nanihii, nikaacha na nanihii pia, na hivi naelekea masjid..ila nanihii ndo siwezi acha aisee
hahaaaa sio wewe tu ..hiyo nanihii hata yule shekhe pia hawezi kuiacha...acha kabisa usifnye mchezo na naniii
 
Fact.
Mwonekano kwanza, tabia tutajua jinsi ya kufix [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom