Uongo wa wachungaji wa Kanisa

Uongo wa wachungaji wa Kanisa

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Habari za muda huu Wana JF

Kuna kipindi nilikuwa Arusha baada ya mihangaiko ya maisha Kuna siku moja, nilikuwa matembezi ili niujue mji wa Arusha vzuri ilikuwa Mara ya Kwanza kufika.

Wakati nipo kwenye mizunguko nilipita mitaa flani siikumbuki vizuri jina lake.kuna kanisa la walokole mchungaji anahubiri,nilipenda Yale mahubiri yake yakanivutia ikabidi niingie ndani kanisani siunajua kanisani hakuna kiingilio.

Ulivyofika muda wa sadaka nikatoa, kumbe lile kanisa Wana utaratibu wao ibada ikikaribia kuisha wageni wote mnaenda mbele kujitambulisha, nakumbuka tulikuwa Kama 2 hivi Mimi na mama wa makamo Fulani.
baada ya kujitambulisha ikafika muda wa kuombewa ili.. tumpokee Yesu.

Mchungaji alianza na Mimi akaanza kuniombea uk mkono ameweka kichwani baada ya muda nikahisi Kama nasukumwa vile nidondoke kila nikijitahidi anazidi kunipush ili nidondoke nakumbuka nilijikaza kila akinipush sidondoki nipo tu akaniangalia kwa jicho Fulani hivi afu akaendlea kuombea mwingine badae ibada iliisha tukaondoka.

Wakati tunaondoka Kuna kijana alinifuata umri tunafanana baada ya story akaniambia niliona pale mchungaji alivyokuwa anakupush afu umekaza tu hata udondoki, Yani pale ukijifanya Kama unadondoka mwisho wa ibada anakuita ukiwa peke yako anakupa hela ata Mimi wakati ni mgeni nakuja alishawahi kufanya hivo.Nilishangaa Sana kumbe Wachungaji wengi ni waongo.

Sikuenda Tena kwenye lile kanisa
 
Haya makanisa mtihani lipi kanisa niliwahi kusali mchungaji badala kuhubili neno yeye ni mipisho wa kwa waumini, asisikie kitu full mipisho.
 
Kuna waliolipwa pesa nyingi ili kujifanya kama misukule iliyofufuka. Ila nasikia ni mazoezi makali.
 
Biashara za watu hizo. Mm nikiona mchungaji maubuli yake yamefocus kwenye utajiri, kupata kazi, kuwa mtawala, kufanikiwa kibiashara na anataka had akuombee yeye huyo kwangu naona ni tapeli tu. Naitaji mchungaji anafundisha mtu kujua neno la Mungu kweli, kujua mambo ya kiroho na kujua jinsi ya kujiombea mwenyewe
 
Biblia ni kitabu cha Maandiko Matakatifu kilichotimia kiukweli kwa 100%.

Tatizo Watu wa siku hizi ni wabishi sana.

Soma Biblia upate maarifa ujue tunaishi nyakati zipi na jinsi ilivyotabiriwa kuhusu Manabii wa uwongo.

CHUKUA HII [emoji116]

MATHAYO 24.

2WAKORINTHO.
11:14-15.

MATHAYO 7:16-21.

1YOHANA 4:1-5.

DANIEL 7.

UFUNUO WA YOHANA 12:14-17.
 
S

Shukran
 
Hawa full uongo .utasikia utapokea nyumba.utapokea gari yeye mwenyewe anatembea kwa miguu si apokee yeye ujinga huu.wananikera sana.utapokea bila kufanya kazi
 
Habari za muda huu Wana JF

Kuna kipindi nilikuwa Arusha baada ya mihangaiko ya maisha Kuna siku moja, nilikuwa matembezi ili niujue mji wa Arusha vzuri ilikuwa Mara ya Kwanza kufika.

Wakati nipo kwenye mizunguko nilipita mitaa flani siikumbuki vizuri jina lake.kuna kanisa la walokole mchungaji anahubiri,nilipenda Yale mahubiri yake yakanivutia ikabidi niingie ndani kanisani siunajua kanisani hakuna kiingilio.

Ulivyofika muda wa sadaka nikatoa, kumbe lile kanisa Wana utaratibu wao ibada ikikaribia kuisha wageni wote mnaenda mbele kujitambulisha, nakumbuka tulikuwa Kama 2 hivi Mimi na mama wa makamo Fulani.
baada ya kujitambulisha ikafika muda wa kuombewa ili.. tumpokee Yesu.

Mchungaji alianza na Mimi akaanza kuniombea uk mkono ameweka kichwani baada ya muda nikahisi Kama nasukumwa vile nidondoke kila nikijitahidi anazidi kunipush ili nidondoke nakumbuka nilijikaza kila akinipush sidondoki nipo tu akaniangalia kwa jicho Fulani hivi afu akaendlea kuombea mwingine badae ibada iliisha tukaondoka.

Wakati tunaondoka Kuna kijana alinifuata umri tunafanana baada ya story akaniambia niliona pale mchungaji alivyokuwa anakupush afu umekaza tu hata udondoki, Yani pale ukijifanya Kama unadondoka mwisho wa ibada anakuita ukiwa peke yako anakupa hela ata Mimi wakati ni mgeni nakuja alishawahi kufanya hivo.Nilishangaa Sana kumbe Wachungaji wengi ni waongo.

Sikuenda Tena kwenye lile kanisa
Bro makanisa Mengi yamejaa majizi na majambazi,kanisa linatumika kutakqtisha pesa tu,
Kuna fisadi la kiasia lilifukuzwa Kenya kipindi Cha Moi,katika kashfa ya goldenberg,
Likahamia Zimbabwe,huko likakutana na majizi Mengine yaliyopo serikalini,
Yanafsnya ufisadi wa kutisha wa dhahabu,
Kuna mtu ni balozi wa Zimbabwe kwenye bara la ulaya na ni mpwa wa Raisi,anaitwa Uebert angel,vile vile ni pastor anakanisa lake,huyu na Hilo fisadi la kiasia kutoka Kenya,wanafanya umafia wa kutisha,
Aljazeera wamerusha documentary,inaitwa "Gold mafia"
Ukiicheki hii kitu utagundua wizi wa kutisha kwenye makanisa,huyo Uebert angel,jumapili ni pastor anhubiri na kutoa "Pepo"jumatatu yupo ofcn anafisadi nchi yake.
 
Hii haifai kabsa hawa ndo wale mitume wa uongo anyway liko wapi ilo kanisa mchungaj ana gawa pesa [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom