Uongozi Bora na Uwajibikaji wa Kidemokrasia

Uongozi Bora na Uwajibikaji wa Kidemokrasia

Senior Shonga

New Member
Joined
Jan 23, 2021
Posts
1
Reaction score
0
UONGOZI BORA NA UWAJIBIKAJI WA KIDEMOKRASIA

Kwa maana ya jumla, demokrasia ni nguvu ya wengi katika kufanya maamuzi yanayohusu umma na kuweka usawa wa kisiasa katika matumizi ya nguvu hiyo (International IDEA 2008).

Demokrasia ni lazima iwape wananchi uwezo wa kujieleza na kuwasilisha hoja zao kwa utaratibu mzuri unaowafikia wawakilishi wao. Wazo la msingi ni kuwepo kwa mifumo ya uwajibikaji katika demokrasia, kuhakikisha maafisa wa serikali wanatoa huduma za viwango vya juu kabisa kwa watu, vinginevyo wanawajibishwa ipasavyo ikiwa hawatafanya hivyo.

Maafisa wa Serikali wanapowajibishwa, na misingi ya kidemokrasia inapoheshimiwa na kufuatwa kuna uwezekano mkubwa wa huduma za umma kuboreshwa kwa haraka, kwa wakati muafaka, kwa ubora wa juu au kutekelezwa vizuri zaidi. Mbinu hii inayoongozwa na wananchi wenyewe katika kutathmini uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji wa huduma, imejikita kwenye imani kwamba raia wa nchi husika wapo katika nafasi nzuri ya kutathmini iwapo hali ya kidemokrasia katika nchi yao inafanana na mawazo yao na inakidhi matarajio yao.

Aidha, utaratibu huu umebeba mbinu kadhaa zilizounganishwa zenye lengo moja ambalo ni KULETA MABADILIKO.

Uwajibikaji wa kidemokrasia ni nini?

Kuwawajibisha maafisa wa Serikali ni kitovu cha demokrasia. Uwajibikaji wa kidemokrasia unawapa wananchi na wawakilishi wao nafasi na njia ya kutoa maoni yao na kupatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa maafisa wa kuchaguliwa na wale wasio wa kuchaguliwa, na inapobidi wanashauri hatua za kuchukua kwa maafisa walioshindwa kutekeleza majukumu yao.

Dhana ya uwajibikaji wa kidemokrasia inajumuisha vyote viwili, uwajibikaji wa kisiasa na ule wa kijamii iwe moja kwa moja au kinyume chake au kwa namna yoyote ile iliyo katika msingi mkuu wa kidemokrasia wa nguvu ya wengi katika maamuzi yanayohusu umma.

Uwajibikaji wa kidemokrasia unajumuisha uwezo wa wananchi wa kuelezea matakwa yao ili kushawishi maamuzi, kwa mfano, kupitia michakato ya uchaguzi. Njia nyingine za kidemokrasia ni pamoja na maandamano, habari za kiuchunguzi, mikakati ya kibunge, midahalo ya umma au kura za maoni. Uwajibikaji wa kidemokrasia pia unahusu mbinu ambazo sio za moja kwa moja, kama vile mfumo wa kuchunguzana na kurekebishana pamoja na taratibu nyingine zinazotumika kwenye taasisi moja moja ili kushawishi uendeshaji wa nchi.

Mifano ya mbinu hizo ni usikilizaji wa kesi katika kamati za kibunge, maswali yanayoulizwa na vyama vya siasa vya upinzani pamoja na mapitio au uchunguzi unaofanywa na ofisi ya uchunguzi wa malalamiko ya wananchi au taasisi kuu za ukaguzi wa hesabu za seikali, n.k. Uwajibikaji siyo sifa inayoishia kwenye demokrasia tu bali uwajibikaji unapokuwa wa kidemokrasia, unasaidia sana kuboresha utendaji wa Serikali.

Uwajibikaji wa kidemokrasia unafanyaje kazi katika utoaji wa huduma za umma?
Kuna uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji huduma pale ambapo wananchi au wawakilishi wao wanahoji au kutoa mrejesho kuhusu huduma za umma halafu watendaji wa kisiasa na watoa huduma ama wayafanyie kazi maoni hayo au wawajibishwe.

Kutokana na dhana hiyo ya msingi, uwajibikaji unabeba uhusiano kati ya watendaji wa aina mbili: Wawajibikaji ni maafisa wa kuchaguliwa na wasio wa kuchaguliwa au watoa huduma wa sekta binafsi wenye mamlaka na wajibu wa kufanya kazi yao na kutoa maelezo na kuhalalisha matendo yao na pia wanaoweza kuwajibishwa kwa matendo yao,mazuri au mabaya.

Wadai haki ni wananchi au taasisi za kisiasa zinazowawakilisha wananchi na zenye haki au mamlaka ya kuangalia/kusimamia utendaji wa wawajibikaji, kuwahoji na kuwahukumu pamoja na kutoa adhabu inapohitajika. Mara nyingi demokrasia hudhaniwa kuwa inapokuwepo basi na mifumo ya uwajibikaji inakuwa inafanya kazi pia. Kwa uhalisia dhana hii ni changamani zaidi. Aina mbalimbali za mivutano, makundi na mazingira halisi huathiri namna huduma zinavyotolewa na jinsi mfumo wa uwajibikaji unavyofanya kazi.

Mara nyingi taratibu hizo huwa hazipo kabisa, hazifai au zinabagua kwa misingi ya utambulisho (kama vile, ubaguzi kwa misingi ya lugha, kabila, dini au jinsia), mwelekeo wa jinsi, umri, kipato, ulemavu au mamlaka.
 
Back
Top Bottom