Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Lisingekuwa Vuguvugu la kumng'oa Mbowe hizi Dakika za Mwisho kwangu mimi ungeniuliza nani anastahili kuwa Mwenyekiti baada ya Mbowe ningesema ni Heche.
Leo nimewasikiliza wote(Lissu&Heche) Hotuba zao walipoingia Ofisini kwa mara ya kwanza,kimsingi ukiwasikiliza vizuri Hotuba ya Heche ndiyo ilitakiwa iwe ya Lissu na ya Lissu iwe ya Heche.
Heche katoa hotuba nzuri sana ya kuvunja Makundi na kutambua Mchango wa Mbowe, Lissu alijitahidi kuongea ila kwasababu ya utulivu mdogo mwishoni alichemsha baada ya kuingiza mambo ya Kampeni tena kwa kuleta majungu na Madongo hasa alipotumia neno Wabangaizaji ambalo lilitonesha Vidonda, tukumbuke neno hili lilitumika sana kama kete ya kuwaunganisha watu wake kipindi cha Kampeni na kuwabagua watu wa Mbowe.
Kwangu mimi naona Heche anaweza kuponya Majeraha na kuwaunganisha wanaCHADEMA kuliko Lissu, hii ni kwasababu Heche ni Homeboy anapendwa na WanaCHADEMA wengi hata katika kundi la Mbowe anao watu wengi na pia kipindi cha Kampeni aliendesha Kampeni za Wastani ambazo hazikujeruhi sana watu na baada ya kushinda ameepuka sana kuendeleza mambo ya Kampeni.
Hii ni tofauti na Lissu ambaye Kampeni zake aliumiza sana watu, alitumia hadaa nyingi ikiwemo kumchafua sana Mbowe hasa kwa tuhuma za rushwa zisizo na ushahidi nk.,Kampeni za Vurugu na Uhuni mwingi akishirikiana na Wakina Pambalu na Mwaipaya, hawa walitengeneza Chuki kubwa sana wanahitajika kufanya kazi ya ziada kurudi kwenye Mioyo ya upande wa pili.
Ni Mtazamo tu Povu linaruhusiwa.