JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Uongozi jumuishi ni moja ya misingi ya utawala bora ikiwa na maana kuwa, kuhusisha watu wa aina zote kwenye jamii kama wazee, vijana, wanawake, wanaume na walemavu kwenye kufaidika na mambo yatokanayo na serikali au uongozi wao.
Pia kuhusishwa kwenye kufanya maamuzi juu ya mambo yahusuyo jamii yao.
Kutofanya hivyo hupelekea utofauti mkubwa kati ya wenye nacho ambao ni wale wanaojumuishwa na wasionacho wale wanaoachwa kwenye mipango ya mambo mbalimbali.
Aidha hupelekea watu kuharibu mambo ya maendeleo kama vile miundombinu ambayo imejengwa bila wao kuhusishwa kwakuwa wanajihisi si sehemu ya mipango hiyo.
Upvote
1