SoC03 Uongozi na viongozi

SoC03 Uongozi na viongozi

Stories of Change - 2023 Competition

Daniel Elisha

New Member
Joined
Feb 1, 2018
Posts
3
Reaction score
0
Uongozi ni mfumo rasmi ulikubaliwa na jamii ili kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii Kwa manufaa ya jamii.
Dhana ya uongozi ni mtambuka , mosi mfumo wa jamii unaweza amua namna ya uongozi uwejene, pili ni mtazamo
wa wananchi huu ya uongozi tatu na mwisho, utashi wa jamii kuhusu uongozi.

Hadithi ya KAMCHAPE, Joka la msimu,Watoto wa Mama ntilie ni miongoni mwa vitabu vichache vinavyoelezea uongozi. Uongozi huanzia ngazi ya familia ambapo makuzi na malezi, hali ya familia kiuchumi, tamaduni pamoja na mila na desturi huchangia aina ya viongozi na uongozi. Kuwa na misingi ya Uongozi na Viongozi ni nguzo katika maendeleo ya Taifa. Tanzania imekosa misingi muhimu ya uongozi na Viongozi.

Athari za kukosa misingi ya Uongozi hupelekea kutokuwajibika pamoja na utamaduni mbovu wakuendekeza makosa yasiorekebishika ambayo hugharimu jamii Kwa namna Moja ama nyingine. Kwa mfamo Ripoti za CAG Kila mwaka Zina dosari na ubadhirifu mkubwa wa fedha lakini jamii imekaa kimya , Ripoti za TAKUKURU pia ni mtindo mmoja kama za CAG. Misingi ya Uongozi ni vyema kama nchi tukaiweka pamoja na misingi ya Viongozi. Leo hii Tanzania Kila anayeingia kwenye siasa huwa malengo makubwa ni maslahi binafsi na si jamii.

Kwa mtazamo wangu ili kuwe na maendeleo endelevu lazima kuwa misingi bora ya Uongozi na Viongozi ili kuweka sura halisi ya matakwa ya jamii. Misingi bora ya Uongozi itakutanisha watu wenye mtazamo tofauti pamoja. Kwa mfano vyama vya siasa ingali Kuna upinzani wa Uongozi lakini dhana ni Moja, yaani misingi ya Taifa.

Hivyo basi bila misingi bora ya Uongozi hakuna kiongozi bora, miaka nenda rudi tutabaki na wimbo huu. Rai yangu kwa jamii tukubali kutengeneza misingi ya Uongozi na Viongozi kwa mara ndio nguzo ya demokrasia, Uongozi imara, uwajibikaji na uzarendo.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom