Uongozi ni dhamana nzito kwa mwenye hofu ya Mungu

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Uongozi sio kitu cha kukimbilia wala kukihangaikia.

Kwa mtu yeyote yule mwenye hofu na Imani kwa Mungu huwa hana tabia ya kukimbilia au kuhangaika kutafuta vyeo kwa sababu anajua kuwa cheo ni dhamana kubwa sio tu kwa Binaadamu mwezako bali Kubwa zaidi kwa Mungu.

Hupaswi kufarahia sana unapo bahatika kupata cheo au kukasirika unapo kosa cheo, maana unaweza ukafurahi sana lakini mwishowe ukaja kulia sana kama sio kuhuzunika.

Mambo yote huwa na mkono wa Mungu kupitia binaadamu hivyo tuwe na tabia ya kushukuru kwa kila jambo.

Viongozi wetu mnao teuliwa katika nafasi mbali mbali msishangilie mkajasihau kuwa cheo ni dhamana lakini kubwa kuliko pia kumbuka uhai maisha yako ya hapa duniani ni kwa muda tu, hivyo fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya taifa lako.
 
Mbowe mbona amekomalia uenyekiti miaka 20 ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…