Uongozi ni kama mali ya Familia

Uongozi ni kama mali ya Familia

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Wengi wetu Huwa tunaamini kwamba ukishachaguliwa au kuteuliwa kuwa Kiongozi basi nafasi hiyo ni yako milele, jambo ambalo tunakosea sana unapopewa nafasi haimaanishi kuwa wewe ni bora kuliko wote waliobaki na unavyoondolewa haimaanishi kwamba umefanya vibaya sana na ndio maana tunasema Uongozi ni kama mali ya familia mwanafamilia yeyote anahaki ya kusimamia ikiwa anavigezo.

Kwanza nimpongeze Mhe Rais Kwa kufanya teuzi za Wakuu wapya wa Wilaya na Makatibu Tawala katika maeneo mbalimbali, hakika hii ni hatua kubwa katika uongozi.

Nanyi kwenu ndugu viongozi ambao mmeachia ngazi kupisha wengine tunawashukuru sana Kwa uongozi wenu uliotukuka hakika mmefanya kazi kubwa katika kuliendeleza Taifa letu mpaka hapo ambapo umefika wakati wa kuwaachia wengine waendeleze mlipoishia Hii ni keki ya Taifa lazima kila mmoja aonje utamu wake na kujua uchungu uko wapi Nini kifanyike Ili utamu uendelee Kwa watanzania kupeana nafasi au zamu ni jambo la kawaida katika uongozi.

Na ndio maana hata katika familia kama kila kitu Kiko sawa huwezi kuwa mtoto peke yako lazima watazaliwa wengine hiyo haimaanishi kwamba hawakupend au utimizi majukumu yako kama mtoto. Pongezi za dhati kwenu ndugu viongozi ambao ndio mmepata dhamana hii Rais Samia Suluhu Hassan amewaamini ni wajibu wenu Nanyi kumuaminisha kuwa mnaweza katika nafasi mlizopewa.
 
Back
Top Bottom