Pre GE2025 Uongozi wa CCM chini ya Rais Samia umechokwa na kuwa kituko mpaka wanatumia mabango ya Comedy "Cheka na Samia"?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Aisee hii ni kali , chawa ndio mmechoka mama kiasi hiki mpaka mmemuweka kwenye bango la comedy? Kwahiyo mmekubali kuwa uongozi wake ni kituko mpaka mmefanyia hivi?

Aisee nimelia sana. Nimebubujikwa kwa machozi ya uchungu! Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah nyie ndio wa kumfanyia hivi mama kweli?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

CCM leo mmejitoa mhanga kusema ukweli kuwa mnachoweza ni comedy tu, ila suala la kuongoza serikali limewashinda?

Mama sasa hivi hatoshi, amebaki kutuchekesha tu?


Bango lipo kona ya St. Peter Dar

Afu mwenye bajaji atakua mwana wa Lissu😂😂🤣 alijua kujipitisha muda sahihi, mpaka the Universe is consipiring against CCM.....nazidi kulia kwa huzuni.
 
Kwi Kwi Kwi, uchumi umeporomoka wajanja wanapiga hela, Yeye katundikwa kwenye mabango!
 
My lady,
DR.Samia Suluhu Hassan ni kipenzi cha waTanzania wa makundi yote ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kitaifa na kimataifa, ikiwa ni pamoja na hao wachekeshaji nchini.

Ikikupendeza hata wewe usiache kuweka picha ya Dr.Samia kwenye ile saluni yako, lakini pia na umshauri hata yule bodaboda wako anaekukopeshaga, nae aweke picha ya Dr.Samia, na kwakweli atapata heshima kubwa kwa jamii na atapata wateja wengi zaidi
 
CCM ni mfumo sio mtu hayo yote yanafanywa na mfumo wa utawala Raisi iko pale kwa masirahi ya Chama na deepstate ndo wanapanga la kufanya.......

Lisu ana kazi kubwa kwasababu yeye amejianda kupambana na Samia wakati kuna system ambao hewezi kupoteza mamlaka yoyote wako tayari kwa manipulation zozote ili wa baki na nguvu za pesa na mamlaka hiyo kauli yaka ya no "reforms no election" labda awe tayari kwa kifo mwenyewe ila mass uprising sio rahisi kwa jamii yetu hi.
 
Katafute hela wewe uitunze familia yako, asubuhi yote hii unapoteza muda kupiga picha za mabango ili iweje?

Kwani Comedy siyo sekta ya burudani ambayo inaajiri watu?? Vipi unawadharau akina Will Smith, Bill Cosby, Chris Tucker ?? Wakati ni billionaires?

Ajabu iko wapi Rais ku-bless wachekeshaji wa Tanzania??
 
Nazidi kulia kwa huzuni... kweli mmeona mama anachoweza ni kutuchekesha tu? Hadi wewe Mkuu?
 
Naona mnajitekenya na kujichekesha wenyewe. Mama ndio habari ya Mjini.
Tumejitekenya sisi na bango mmeweka wenyewe? Yaani mnamuona mama kituko kweli? Nimelia sana mpaka nimebubujikwa machozi ya sonona
 
Hii awamu ndio mabango yamezagaa kila kona nchi hii. Yaani kila sehemu unakutana na bango la kusifia.
 
Hao uliowataja kazi yao ni nini?🤣🤣 leo mmefanya mama comedian? Amekuwa kituko? Kutoka raia wa kwanza hadi comedian, ni zaidi ya fezea.... mnazidi kunitia huzuni na kunifanya nilie kwa kugalagala kama Jenista Mhagama
 

'When a clown moves into a palace, he doesn't become a king. The palace turns into a circus'. - Turkish Proverb.​


Hawajakosea kutumia picha waliyotumia.
 
Kwa jinsi ulivyojibubujikwa na machozi mpaka umepotea kwwnye maelezo... nakuelewa, nna uchungu kama wewe
 
Hali ni mbaya sana.
 
Nazidi kulia kwa huzuni... kweli mmeona mama anachoweza ni kutuchekesha tu? Hadi wewe Mkuu?
my lady,
my freiends, ladies and gentleman,

nasisitiza waTanzania wote wazalendo nchini,
kuendelea kushikamana na Rais kipenzi cha waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan, kwa njia mbalimbali sehemu za kazi na majukumu yao.

Ni heshima na uzalendo wa kiwango cha juu kuambatanisha picha za Rais Dr.Samia Suluhu Hasaan, popote ulipo
 
Samia mitano CCM daima
 
Hii nchi imefika sehemu mbaya sana. Kwa wenye akili popote walipo. Ni lazima CCM ilazimishwe tupate Katiba Mpya sasa ili tuondokane na huu upuuzi wa kuabudu watu na kujenga kizazi wa wajinga na machawa.

This country is now a failed state.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…