A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha kero hii kupitia jukwaa hili labda Serikali inaweza kuchukua hatua hitajika ili kuweka mazingira salama kwa ajili ya usalama wa afya za Wanafunzi na kutoa mazingira rafiki kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Hali ya usafi katika chuo hiki ni mbaya sana, hiyo ikisababishwa na uchache wa Watumishi wa kufanya usafi, usimamizi mbovu na upatikanaji hafifu wa huduma ya maji.
Hali hii ni mbaya sana hasa katika maliwato (Toilets) kwa kila jengo hususa ni Majengo ya Hostels za Wanachuo, miundombinu mingi ya chooni imelika na chumvi na mingine imeziba kabisa, tunakoelekea kuna siku chemba zitafumuka na kusambaza uchafu kwenye majengo.
Naomba Uongozi wa UDOM upate salamu hizi wajue next time tutaweka wazi kwa kuonesha picha zote jinsi hali ilivyo, ni kichefuchefu sana.