Mzalendo05
New Member
- Nov 30, 2024
- 1
- 0
Moja kwa moja niende kwenye mada inayohusu vyuo vingi lakini hasa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT), ambapo limetoka tangazo linalowataka wanafunzi kulipa asilimia 50 ya ada ili kuruhusiwa kufanya Test 1.
Kwa kuwa mhula umeanza hivi karibuni na tunafahamu vipato vinatofautiana, baadhi ya wanafunzi hulipa ada kwa awamu ndogo ndogo. Tunaomba ruhusa rasmi kwamba kuelekea msimu wa Test 1, mwanafunzi awe amelipa angalau robo ya ada ya mhula. Kuelekea Test 2 na mitihani ya mwisho (UE), awe amefikia asilimia 50.
Sio kila mwanafunzi ana mzazi mwenye uwezo mkubwa. Wapo wasiokuwa na boom, na wapo ambao boom linatosheleza mahitaji muhimu kama kodi, chakula, na mavazi. Tunaomba Serikali ya Mama Samia kupitia wakuu wa vyuo Tanzania, ambao ni walezi wa ndoto za Watanzania, waone namna ya kushughulikia changamoto hizi.
Tunaomba wanafunzi waruhusiwe kulipa robo kwa robo ya ada, mradi ifikapo msimu wa UE wawe wamemaliza ada. Hii ni nafuu kwa familia zenye kipato kidogo zinazojitahidi kufanikisha ndoto za watoto wao.
Nawasilisha kwa imani kuwa wahusika watachukua hatua ya kusaidia wanafunzi kufanikisha ndoto zao. Kulipa asilimia 50 kwa mkupuo ni changamoto kwa wenye kipato cha chini.
Mungu ibariki Tanzania.