Azoge Ze Blind Baga
JF-Expert Member
- Mar 8, 2019
- 442
- 1,655
Kama mada inavyonieleza
Kuna hiki kitendo cha dailysis pale Bugando hospital mambo ni ovyo sana
Kwanza wahudumu hasa wa kike kwenye kile kitengo hawana kauli nzuri kwa wagonjwa wanaokuja kusafisha damu
Suala la kuwatoa wagonjwa kwenye mfumo baada ya kumaliza matibabu nalo ni kero wahudumu wanarushiana mpira nani awatoe wagonjwa kwenye mfumo hali inayoleta kero na usumbufu mwingi kwa wagonjwa.
Machine za kusafisha damu zimeunganishwa na mfumo wa maji ila tangu jumanne mfumo unasumbua hivyo mashine zinasimama kufanya kazi hali inayopelekea huduma kuchelewa
Mfano siku ya jumanne ya tar 24/12/2024 mfumo wa kusambaza maji kwenye machine ulizingua mashine zikaacha kufanya kazi na kusababisha wagonjwa kuchelewa kupata huduma.
Hospitali inakusanya hela nyingi kupitia wagonjwa wa figo lakini huduma zao zimekua mbovu na za ovyo sana
Kila wakati mashine za kusafisha damu zinaharibika hali inayopelekea kuwa na foleni kubwa na kuchelewesha kutoa huduma kwa wagonjwa.
Mkurugenzi wa Hospital ya Bugando na timu yake ijitathimini juu ya changamoto nyingi zilizopo kwenye kitengo cha Dailysis.
Hela mnachukua lakini huduma zenu ni mbovu na haziridhishi mbona mnafanya kazi kwa mazoea na mnaleta mazoea kwa afya ya mtu.
Waziri wa Afya fuatilia kero hii kwenye kitengo cha Figo pale Bugando.