KERO Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Igawilo – Mbeya boresheni huduma kwa wateja

KERO Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Igawilo – Mbeya boresheni huduma kwa wateja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi baadhi ya wananchi tuna malalamiko kuhusu hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Igawilo, zipo changamoto mbalimbali zinazoathiri upatikanaji wa huduma bora za afya kwa leo nitazitaja mbili tu.

Kwanza kabla ya yote kuna huduma zisizoridhisha kwa baadhi ya Watumishi, nimeshuhudia matumizi ya lugha isiyo ya staha kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa afya, hao watumishi wachache ni wakali kama pilipili.

Jambo lingine gharama kubwa za dawa, kwanza bei ni kubwa tofauti na vituo au hospitali nyingine za Serikali, licha ya kwamba mwenye uhitaji analipa kwa Namba ya Malipo lakini gharama zao ni kubwa ukilinganisha na wenzao.

Wanaweka utaratibu ambao mgonjwa au mwenye uhitaji ananunua mahitaji ya matibabu katika duka linalohusishwa na hospitali hiyo, ole wako ujaribu kwenda nje, watakufokea, watakasirika na wanaweza hata wasikubali kuchukua dawa zako.

Yote hayo siyo kwamba yanafanywa na hospitali yote bali baadhi ya Watumishi kiasi kwamba najiuliza dawa zao ni bora zaidi ya nyingine zote? Kwanini hawataki tununue nje ya kituo chao ambacho wao wanauza bei kubwa zaidi?

Unalazimishwa kununua dawa ndani ya hospitali, na ukinunua nje wanakudharau au wanakataa kuzitumia.
 
Back
Top Bottom