Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Nimeshangazwa kama si kugutushwa na sababu ambazo Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizotoa kwa reshuffle ya mwisho wa wiki iliyopita. Sababu kubwa inasemekana viongozi katika ngazi fulani hawaelewani. Hii imenishtua sana!
Nikajiuliza, kwa nini viongozi mahali popote kikazi hawaelewani? Mimi sioni sababu nyingine, ila ile ya maslahi binafsi. Hapa Mama akae chonjo, kikulacho tayari kiko nguoni!
Lakini imekuwaje tumefika hapo?
Mtu Waziri anatoka Magu, Naibu wake anatoka Nangurukuru, sasa watapendanaje kama hawana common denominator? Kula kwa urefu wa kamba yako na maslahi binafsi hapo ndio tatizo.
Mwalimu Nyerere alitufundisha, ilituendelee tunahitaji vitu vinne:
-Watu,
-Ardhi,
-Siasa safi na
-Uongozi bora.
Viwili vya kwanza, yaani watu na ardhi havina matatizo. Tatizo liko katika Siasa Safi - Unifying Ideology na Uongozi Bora.
Hapo chama tawala kiingilie kati, maana viongozi kama hawana umoja na vision inayoeleweka hawataishia kusonyana, mwisho wake ni visu vya mgongoni vinavyoweza kuishia kwenye machafuko kwa wapambe na wananchi.
Sera za umoja na vision kati ya viongozi vinayumba.
Ni mawazo tu.