HOST NOT FOUND
JF-Expert Member
- Dec 30, 2023
- 1,192
- 3,486
Tuambiane ukweli:
Leo, watu wengi wanataka kuwa viongozi si kwa sababu ya kuwahudumia wengine, bali kwa sababu ya madaraka, heshima, na ulaji.
Lakini uongozi wa kweli haupimwi kwa vyeo wala makofi ya hadhara. Unapimwa kwa kiasi gani uko tayari kusema ukweli hata kama utachukiwa, kutengwa au kupoteza kila kitu.
Viongozi wa kweli huwa wachache kwa sababu kubeba dhamira ni kazi nzito kuliko kubeba cheo. Cheo kinaweza kukuficha, lakini dhamira inaweza kukuumbua.
Na kama jamii, tusipobadilika, tutaendelea kupigiwa makofi na wanaotutafuna kimyakimya.
Swali langu kwa kila anayesoma huu ujumbe ni moja tu:
Je, wewe ni mfuasi wa viongozi wa cheo au wa viongozi wa ukweli? Na kama siku moja utapewa nafasi ya kuongoza, utalinda kiti au utatetea watu
Tafakari. Jibu kwa moyo. Si kwa mazoea