KERO Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam umeshindwa kuliongoza jiji

KERO Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam umeshindwa kuliongoza jiji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Katika jambo linalonishangaza ni kuwa mwaka huu 2025 mwezi wa nane Tanzania kama ilivyo Kenya na Uganda tunahost michuano ya CHAN na 2027 tunahost Afcon lakini jiji la Dar es Salaam kila kukicha linaendelea kuwa chafu, vibanda na biashara hole holela zinaongezeka kila kona.

Bodaboda hawana mpangilio kila sehemu wameweka vijiwe. Maji machafu yanatiririshwa ovyo.Baadhi ya mitaa ya Kariakoo kama Sikukuu kuna harufu mbaya sana.

Kwa mwendo naona tunaenda kutia aibu taifa kwa uchafu.

Viongozi wa jiji na mkoa wajitafakari na kama wameshindwa wapishe wengine wenye maono wasafishe na kupanga vizuri jiji la Dar es Salaam ili sisi wa mikoani tusiabike kwa ajili ya jiji la Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom