Uongozi wa Simba SC tafadhali kwa 'Umafia' unaopangwa na Yanga SC kuelekea 'Derby' yetu nao May 8, Wafuatao wasicheze FA Jumamosi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nimepenyezewa za ndani kabisa kutoka kwa Watu wa Yanga SC ( ambao wanajua Mimi ni mwenzao ) kuwa wamezungumza na Wachezaji wa Kagera Sugar tunaocheza nao FA Jumamosi ili 'Wawaumize' Wachezaji wetu Muhimu ( Waandamizi )

Wanaotakiwa 'Kuumizwa' vibaya ili wakose ( waukose ) mtanange wa Simba na Yanga tarehe 8 May, 2021 kwakuwa ni 'Tishio' Kwao na Yanga SC wameshajua kuwa hata 'Wakaroge' wapi wanakufa ( wanafungwa ) tu tena Goli / Bao nyingi ni hawa Wafuatao hapa...

1. Clatous Chama
2. Jose Miquissone
3. Joash Onyango
4. Thadeo Lwanga
5. Bernard Morrison
6. Larry Bwalya
7. Shomary Kapombe
8. Aishi Manula


Hivyo basi GENTAMYCINE nauomba Uongozi wa Simba SC ( hasa kwa Benchi la Ufundi ) Kikosi hiki Kifuatacho hapa ndicho Kicheze Mechi ya FA na Kagera Sugar Jumamosi ijayo ( tarehe 1 May, 2021 )

1. Beno Kakolanya 'Baba Paroko'
2. David Kameta 'Duchu'
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa
6. Jonas Mkude ( Mwanangu )
7. Hassan Dilunga
8. Said Ndemla
9. Meddie Kagere
10. Perfect Chikwende
11. Miraji Athuman

Kwa Kikosi kipana cha Simba SC, aina ya Wachezaji wetu wenye Vipaji binafsi na Morali iliyopo ndani ya Kambi nina uhakika hata kwa Kikosi changu hiki tu hapa Juu Kagera Sugar anafungwa na ukizingatia tunacheza 'Machinjioni' Kwetu kwa Mkapa.

Naomba ANGALIZO langu hili lizingatiwe na Watu wa Simba SC na ningependa pia liwafikie haraka Mtani wangu ( wa Kiha ) Kocha Matola, Msemaji Haji Manara, Mshauri Mkuu wa CEO ( Poti wangu kabisa ) Magori, Meneja ( Mtani wangu wa Kihaya ) Rweymamu na Madame CEO Barbara.

Cbonde Chonde watajwa Wasipangwe.
 
wew utakua ni shabiki wa kagera sugar. Unaogopa mtakula mvua za kutosha.
 
Kwani ao wachezaji wa Simba ambao unaogopa wasiumizwe kwa hujuma hawakuwepo kwenye mechi ya mzunguko wa Kwanza? pamoja na kuwa una u mbumbumbu Ila iyo hoja Ina utoto mwingi.
 
Mechi ya FA na VPL ipi ni muhimu kwa sasa? FA ni muhimu zaidi kwa sababu VPL tunakamilisha ratiba tu,ila FA ni mtoano. Acha wafie uwanjani dhidi ya Kagera sugar. by the way hawawezi kuwapa majeruhi wote
 
Bwalia au chama lazim awepo uwanjani ili team isogee mbele
Wakiumizwa hawa kwa Makusudi ( Kimkakati ) Pasi za Magoli 7 tunayotaka Kuwafunga Yanga SC tarehe 8 May, 2021 atazitoa Mjomba wako au Shangazi yako?
 
upo kama sio mwanaume
 
Huyu gentamycine ni pandikizi la utopolo ndani ya simba! Hujiita pia Al-rounder! Lengo lake ni kuleta mtafaruku. Tumpuuze!! Lengo lake ni kuleta hofu kwa wachezaji, tumpuuze tu! !wa akili ya gentamycine/al-rounder anaamini pia anaweza kumchanganya hata kocha!! Tumpuuze utopolo huyu ambaye kwa siku hizi anajipambanua kama mpenzi wa simba
 
Huwezi kumwona kumwona tena hapa gentamaycine,! Mbinu yake kutaka kuiingiza chaka simba imeangukia pua!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…