GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Uongozi wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca, Fadlu David ambaye inaelezwa atatua nchini Ijumaa sambamba na wasaidizi wake.
Kocha huyo ambaye amethibitisha ujio wake Tanzania baada ya kutumia ukurasa wake mtandao wa kijamii ‘Instagram’ kuwaaga viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu aliyokuwa akiifundisha.
“Ulikuwa ni wakati mzuri, msimu mzuri, wachezaji bora, wafanyakazi wenzangu tulikuwa na benchi bora bila kuwasahau mashabiki,” Ni ujumbe wa kocha huyo akiwaaga."
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwananchi kuwa kocha huyo anakuja na wasaidizi wake sambamba na meneja wa timu hiyo.
Chanzo: mwananchi_official
OMBI LANGU KUU GENTAMYCINE kwa Uongozi wa Simba SC
Tafadhali kama mmeamua aje Kocha Mgeni na Benchi lake zima basi hakikisheni akina Mgunda na Matola hawawi karibu na Timu kwani hawa Wawili ni Watanzania wenzangu ila kwa Majungu nadhani wameshapata tayari Degree na Masters wanasubiria tu Doctorate yao sasa.
Na kama mtaamua Kocha Mgunda awe Msaidizi wake kutoka kwa Wazawa ( Watanzania ) tafadhali mwambieni kabisa Mgunda kuwa huyu Kocha ni Bosi wake na amuheshimu na aachane na tabia yake ya Kupigisha Shoti Wachezaji hasa Wazawa ili Kuigawa na Kuidhoofisha Timu kusudi arejeshwe Kuikoa Timu.
Ila kama pia mtaamua kuachana na huyu Kocha Mgeni basi nauomba Uongozi wa Simba SC umuamini Kocha Mgunda na Matola wawape Timu kwa Msimu huu Mmoja, ila hakikisheni mnawapa Stahiki zao zote kama ambavyo huwa mnawapa Wageni na mngempa Mgeni ajae ili Watulie na wasiwe na Majungu ya 10%.
Yangu ni haya tu ila Asanteni sana Uongozi wote wa Simba SC na kwa Tajiri kwa huu Udhamini wa Kiufundi wa sasa.