Uongozi wa Yanga uhusike na kulipa gharama zote za kuharibu mechi ya Derby iliyotakiwa kufanyika hivi leo. Uhuni kwenye soka haukubaliki

Ahlan bik

Football ukipenda iite Soccer ni mchezo wa kiungwana sana unaozingatia sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa na shirikisho la mpira duniani kwa maana ya FIFA na shirikisho la mpira katika nchi husika.

Kanuni zipo wazi kabisa na uongozi wa Yanga unafahamu fika kuwa timu ambayo itakuwa ni mgeni inatakiwa iruhusiwe kufanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mechi tena kwa kuzingatia muda ule ule wa mechi.

Simba Sc kwa kulijua hili walifata sheria zote , cha ajabu uongozi wa timu ya Yanga umeamua kufanya uhuni kwa kuweka vikundi vya wahuni wanaodai kuwa ni Makomandoo wa Yanga kwa ajili ya kuulinda uwanja na kupelekea kuzuia timu ya Simba sc isiingie uwanjani kufanya mazoezi.

Wito wangu kwa TFF na Bodi ya Ligi iangalie namna ya kutoa adhabu kali sana kwa uongozi wa timu ya Yanga ili iwe fundisho kwa wahuni wote wanaolenga kuchafua taswira na hadhi ya Ligi kuu ya NBC.

Dunia nzima ilijiandaa leo hii kushuhudia moja kati ya derby kongwe na bora zaidi kutokea katika bara la Africa na dunia nzima. Ila jambo la ajabu na aibu kusikia kuwa mechi hii haitachezwa kutokana na viongozi na uongozi wa timu ya YANGA kufanya uhuni.

Watanzania wengi wamenunua ving'amuzi kwa ajili ya kushuhudia mechi hii , Je nyinyi viongozi wahuni wa Yanga ,mtawalipa nini watanzania waliopoteza pesa zao kwa ajili ya kulipia ada ya ving'amuzi??

Kuna wanachama na mashabiki wenu wamesafiri kutoka mikoa mbalimbali kuja Dar-es-salaam toka juzi kuja kushuhudia moja ya tukio hili la kihistoria ila chakusikitisha wanakuja kuambiwa kuwa mechi haitakuwepo. Je mnawalipa nini hawa wanachama wenu waliopoteza nauli, gharama za malazi na vyakula na kikubwa zaidi muda wao kuja kushudia mechi hii???

Uongozi wa Yanga umefanya makusudi kabisa kwasababu walikuwa na uwezo wa kuwasiliana na wahuni wao waliowaandaa kuharibu mechi kuwa waruhusu msafara wa Simba sc uingie uwanjani.Ila cha ajabu hawakufanya hivyo na ni wazi tukio hili limeonesha dhamira yao ya kuamini imani potofu za kishirikina na pia kuharibu mechi.

Kuna viongozi wa FIFA na CAF pamoja na waandishi wa habari wa kimataifa wamesafiri kutoka mataifa yao kuja kushuhudia mechi hii live ila cha ajabu wanaambiwa kuwa mechi haitafanyika.

TFF na TPBL msipochukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya timu ya YANGA ,tambueni kuwa taifa zima litajua kuwa mnashirikiana na wahalifu hawa wa jangwani kuchafua taswira na hadhi ya moja ya ligi bora zaidi hapa barani Africa.

Wapo mashabiki wa timu hizi mbili walionunua tiketi kwa ajili ya kuingia uwanjani kuishuhudia hii Derby..Je pesa zao mnawarudishia?

Wasimamizi wa uwanja pia wametumia gharama zao kwa ajili ya kuhakikisha mechi hii inachezwa katika mazingira mazuri, Je Yanga mtarudisha gharama zao.?

TFF toeni adhabu kali kwa Yanga unaoongozwa na mwenyekiti wa vilabu barani Africa , Hersi Saidi. ili iwe fundisho kwa wahuni wengine wenye lengo la kuchafua ligi yetu.
1741418412172.png
 
Tupate mwongozo mapema
 
Nlijua tu kuna siku simba itaogopa kuleta timu uwanjani 😂😂😂😂😂 we huku pakome, huku Aziz, kule max kudadadeki hapa mzize alafu katikati khalid wasikimbie mchezo nini ?
 
Thibitisheni kama hao mnaosema waliwazuia Simba ni Yanga
 
Mkuu, kwani ile siku Namungo wamepata kadi nyekundu ya dhuluma walisusia mechi? ,

Sababu za nje ya uwanja hazina uhusiano na kususia mechi
Hili swali kama huna akili timamu huwezi kulijibu. Kuvunjwa Kanuni moja hakuhalalishi kuvunjwa Kanuni nyingine, wasijielekeze vibaya.
 
Nlijua tu kuna siku simba itaogopa kuleta timu uwanjani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we huku pakome, huku Aziz, kule max kudadadeki hapa maize alafu katikati khalid wasikimbie mchezo nini ?
Wee nae sasa hawa walikua wapi pindi wanaondoshwa ktk kabu bingwa?

Uozo mtupu.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Mpira wa Tanzania wa hovyo, simba wajitoe tu kwenye ligi wawaachie ligi yao.Imejaa upangaji matokea,watu fulani kuingilia maamuzi ya uwanjani hovyo kabisa. Safi Simba
Bora useme viongozi wa TFF wajitoe kwenye uongozi kuliko Simba. Kumbe hujajua kwamba Simba ni dude kuuunwaaa
 
Wee nae sasa hawa walikua wapi pindi wanaondoshwa ktk kabu bingwa?

Uozo mtupu.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Kama uozo mbona simba hawataki kuleta timu ? Matokeo mabovu kwenye mpira ni matokeo tu, lakin kwakuwa hatukufuzu haimaanishi Yanga ni wa bovu kivile, kama Yanga mbovu sana njooni, ninyi si mlifuzu njoeni tuwakague mlifuzu vipi
 
Hizi timu za Simba na Yanga zinataka kudumaza soka la Bongo. Tulikuwa tumeshapiga hatua kwenda mbele, naona wanataka kuturudisha nyuma.
 
Msiandike kwa mihemko. Kufuata sheria zote mnamaanisha nini? Je Simba waliwataarifu Yanga muda watakaoenda kufanya mazoezi ili mazingira yaandaliwe? Kwanini waende kwa muda wao wakati sheria wanaijua wao si wenyeji?

Kama Simba hawakutaka kuwasiliana na Yanga ambaye ni mwenyeji, je waliwasiliana na meneja wa uwanja ili aandae mazingira mapema? Barua ya Simba inasema meneja hakuwa na taarifa ya Simba kwenda kufanya mazoezi. Vipi kama meneja wa uwanja alianza kuandaa mazingira kwa ajili ya mechi husika kwa kuwa hana taarifa ya timu kwenda kufanyia mazoezi?

Mnaposema makomando wa Yanga mnamaanisha nini? Yanga ina kikosi cha kijeshi? Kuna kiongozi yeyote wa Yanga alikuwepo kuzuia? Polisi walikuwepo kwenye eneo husika walishindwa kuwadhibiti hao mnaoita makomando wa Yanga? Nafikiri kama kuna kosa limefanyika watakuwa walichukua hatua ili wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria husika.
Wewe nawe kama alivyosema MANARA bado upo kwenye kundi la waliokosa akili
 
Yaani asuse Makolo alafu fidia alipe Yanga? 😂 Akili yako ipo sawa?
 
Back
Top Bottom