Uongozi wa Yanga umeweka bayana majukumu ya Haji Manara

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu nafasi ya 'Bugatti' hasa ikizingatiwa Yanga inae Afisa wa Habari, Hassan Bumbuli na Afsa wa Uhamasishaji Antonio Nugaz

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema Manara ataingia kwenye Kitengo cha Uhamasishaji wakiamini atasaidia kuimarisha kitengo hicho kuelekea Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji

"Wakati tunamtangaza Manara pale Serena Hotel hatukusema anakuja kufanya kazi gani hasa, lakini niseme uongozi upo makini na haujakurupuka kumchukua Haji, kuna majukumu yapo na ataenda kuyafanyia kazi hasa kutokana na mabadiliko ya klabu yanayofanywa sasa, kutoka katika mfumo wa sasa na kwenda mfumo mpya na wa kisasa zaidi, hatoingiliana na Nugaz na Bumbuli" alisema Mfikirwa

"Katika mabadiliko ambayo tunayafanya kwa sasa kuna suala la ‘fan base', hapa tunahitaji mtu wa kushawishi mashabiki waingie kwenye mfumo rasmi wa klabu baada ya kukamilika taratibu zote, kuna mashabiki mikoa mbalimbali ambao klabu inawahitaji, lakini lazima washawishike, hapa ndipo panapohitajika watu au mtu mwenye kujua kushawishi, kuna nani zaidi ya Manara?, ili ni eneo ambalo tunaamini atafanya kazi kubwa sana kwa manufaa ya klabu"

Mfikirwa alisisitiza kuwa kila mmoja (Nugaz, Bumbuli na Manara), atafanya kazi yake kwa maendeleo ya klabu na hakutakuwa na mwingiliano.

"Mashabiki wauamini uongozi wao, sisi tupo pale (madarakani) kwa niaba yao, hivyo chochote tutakachokifanya ni kwa faida ya timu hivyo hakuna haja ya kuwa na shaka na ujio wa Manara ndani ya Yanga".

Credit: Yanga Whatsapp Makao Mkuu + Wasafi FM
 
Hapo mtifuano haukwepeki maana mmemkaribisha lopolopo asiyefuata utaratibu, zigo la mavi mnalo hilo..
 
Haji yuko Yanga kunadi biashara za swahiba na mfadhili wake mkuu Ghalib.
 
Nugaz, Bumbuli, Mpili, Haji...Wote hawa hawamfikii Masau Bwire wa Ruvu Shooting.

Nadhani sasa anatafutwa Baba Levo [emoji2957]
 
Na acheze namb 9 ili muondoe ukame wa wafungaj
IMG-20210826-WA0046.jpg
 
Back
Top Bottom