Uongozi wote wa Manispaa ya Kinondoni kuna haja ya kujitafakari:
- Stand ya daladala Bunju imehamishiwa barabara kuu ya Bagamoyo Manispaa imeshindwa kujenga standi hata ya changarawe. Matokea yake ni ajali na kugongwa kwa wananchi.
- Kata zote Barabara wananchi wanajichangisha wenyewe kulipia Grader, Manispaa inaona sawa. Kwa mfano, Kata ya Bunju ina Miaka Minne manispaa haijawahi kuchonga barabara yoyote. Barabara ya Kilimani Bunju B imebomoka haina mfano Uongozi upo unaona sio tatizo.
- Juzi tumeona wananchi wameweka Bango la kuchonga barabara KWA HISANI YA WANANCHI WENYEWE, Uongozi wa manispaa upo na unaona sio tatizo
- Barabara ya Kutoka Bunju kwenda Mabwe pande pale inapoanzia ina hali mbaya sana, juzi lori kidogo liangukie watu, viongozi wenye dhamana wapo na wanaona.