A
Anonymous
Guest
Habari gani wanaJamiiForums?
Mimi ni mdau wa jamvi la JamiiForums nikitokea Kilwa Kivinje Mkoa wa Lindi. Nina mambo mawili ninataka kuyafichua kwa leo.
Moja, ni kuhusu walimu wa kiume wa shule ya sekondari Kivinje kuendeleza mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike.
Tunashukuru miezi ya nyuma kidogo mliandika kuripoti vitendo hivi na tuliona Serikali ikichukua hatua sitahiki kwa muhusika aliyekuwa amempa ujauzito mwanafunzi na kumkatisha kimasomo.
Pamoja na kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikilaaniwa vikali na wadau mbalimbali, bado kuna wimbi kubwa wa walimu wa kiume kuwarubuni watoto wa kike shuleni ili kuwa nao kimapenzi. Taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wanathibitisha kuwa kuna waalimu kadhaa wana hiyo tabia chafu.
Kilichonithibitishia uwepo wa hili jambo ni baada ya mwanangu anayesoma kidato cha nne kunieleza kuwa kuna mwalimu amekuwa akimsumbua kutaka kuwa naye kimapenzi. Niliamua kukutana na muhusika moja kwa moja na alikiri kosa na kuomba msamaha mbele yangu na kuahidi kuacha hiyo tabia mara moja.
Sijataka kutaja jina la huyo mwalimu kwa sababu ya kumfanyia ustaarabu aliouonesha wakati wa mazungumzo yetu. Pia ni kijana mdogo bado anajitafuta, nisingetaka kumpokonya sehemu yake ya kupatia ugali kosa ambalo anaweza akajirekebisha.
Maombi yangu ni kuwa JamiiForums msadie tena kupaza sauti kukemea na kulaani hivi vitendo ili viweze kuisha hapa Kivinje sekondari na kwingineko Tanzania.
Jambo la pili, kuhusu AFISA ELIMU SEKONDARI KILWA na jopo lake kwa ujumla kuwadhulumi walimu wa shule za sekondari haki na sitahiki zao mfano Malipo ya nauli za likizo, malipo ya uhamisho wa vituo vya kazi na malipo ya walimu wanaosimamia UMISETA.
Nikiwa kama mdau wa elimu, ninakutana na walimu mbalimbali na tunasoga kwa sana tu. Ukweli ni kuwa walimu wana manung'uniko ya kudhulumiwa haki na sitahiki zao za msingi na Afisa elimu wao na midomo yao inakuwa bubu kupaza sauti. Nitaelezea kwa kutoa matukio hai kama ifuatavyo.
Moja, mkurugenzi anaidhinisha malipo ya uhamisho na nauli kwa walimu walioenda likizo za malipo, ila malipo hayawafikii walengwa. Yani ni kuwa orodha ya majina ya walimu watakaolipwa nauli inamfikia mkurugenzi. Yeye anaidhinisha malipo na majina ya walimu hao wanaositahili malipo inawekwa hadharani. Lakini malipo hayafanyiki. Walimu wakifuatilia ofisi ya hazina wanapewa majibu kuwa fedha za likizo na uhamisho zimeshatoka na zipo kwa wakuu wa idara. Mfano Februari 2024 na juni 2024 malipo yaliidhinishwa ila walimu hawakupata sitahiki zao.
Mbili ni kuhusu walimu wanaoteuliwa kusimamia watoto katika kambi za michezo UMISETA kulipwa malipo duni. Wanawekwa kambini wilayani siku 7 hafu wanasafiri na wanafunzi kwenda Lindi Mjini na kuwekwa tena kambini siku 7. Baada ya msoto huo wote wanalipwa shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) wakati wenzao wa wilaya nyinginezo walikutana kwenye kambi kuu ya mkoa Lindi Mjini wanalipwa laki saba
Walimu wanashindwa kuhoji maana kwa maana taifa hili kwa sasa linaendeshwa kwa uoga. Anayeonekana kuhoji anatafutiwa visa na kuhamishiwa kwenye shule za vijijini sana ambako ili ufike kilwa mjini unatumia nauli isiyopungua elfu 60 kulingana na jografia ya kilwa ilivyo. Pia wanaoonekana kuhoji wananyimwa fursa za kusimamia mitihani ya taifa.
Ninaomba mpaze sauti ili Afisa elimu Sekondari Kilwa na jopo lake wajirekebishe ili walimu wafanye kazi bila manung'uniko.
Asante, naomba kuwasilisha.