KERO Uovu unaoendelea Kivinje Sekondari pamoja na dhuluma ya Afisa Elimu Sekondari Kilwa kwa Walimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari gani wanaJamiiForums?

Mimi ni mdau wa jamvi la JamiiForums nikitokea Kilwa Kivinje Mkoa wa Lindi. Nina mambo mawili ninataka kuyafichua kwa leo.

Moja, ni kuhusu walimu wa kiume wa shule ya sekondari Kivinje kuendeleza mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike.

Tunashukuru miezi ya nyuma kidogo mliandika kuripoti vitendo hivi na tuliona Serikali ikichukua hatua sitahiki kwa muhusika aliyekuwa amempa ujauzito mwanafunzi na kumkatisha kimasomo.

Pamoja na kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikilaaniwa vikali na wadau mbalimbali, bado kuna wimbi kubwa wa walimu wa kiume kuwarubuni watoto wa kike shuleni ili kuwa nao kimapenzi. Taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wanathibitisha kuwa kuna waalimu kadhaa wana hiyo tabia chafu.

Kilichonithibitishia uwepo wa hili jambo ni baada ya mwanangu anayesoma kidato cha nne kunieleza kuwa kuna mwalimu amekuwa akimsumbua kutaka kuwa naye kimapenzi. Niliamua kukutana na muhusika moja kwa moja na alikiri kosa na kuomba msamaha mbele yangu na kuahidi kuacha hiyo tabia mara moja.

Sijataka kutaja jina la huyo mwalimu kwa sababu ya kumfanyia ustaarabu aliouonesha wakati wa mazungumzo yetu. Pia ni kijana mdogo bado anajitafuta, nisingetaka kumpokonya sehemu yake ya kupatia ugali kosa ambalo anaweza akajirekebisha.

Maombi yangu ni kuwa JamiiForums msadie tena kupaza sauti kukemea na kulaani hivi vitendo ili viweze kuisha hapa Kivinje sekondari na kwingineko Tanzania.

Jambo la pili, kuhusu AFISA ELIMU SEKONDARI KILWA na jopo lake kwa ujumla kuwadhulumi walimu wa shule za sekondari haki na sitahiki zao mfano Malipo ya nauli za likizo, malipo ya uhamisho wa vituo vya kazi na malipo ya walimu wanaosimamia UMISETA.

Nikiwa kama mdau wa elimu, ninakutana na walimu mbalimbali na tunasoga kwa sana tu. Ukweli ni kuwa walimu wana manung'uniko ya kudhulumiwa haki na sitahiki zao za msingi na Afisa elimu wao na midomo yao inakuwa bubu kupaza sauti. Nitaelezea kwa kutoa matukio hai kama ifuatavyo.

Moja, mkurugenzi anaidhinisha malipo ya uhamisho na nauli kwa walimu walioenda likizo za malipo, ila malipo hayawafikii walengwa. Yani ni kuwa orodha ya majina ya walimu watakaolipwa nauli inamfikia mkurugenzi. Yeye anaidhinisha malipo na majina ya walimu hao wanaositahili malipo inawekwa hadharani. Lakini malipo hayafanyiki. Walimu wakifuatilia ofisi ya hazina wanapewa majibu kuwa fedha za likizo na uhamisho zimeshatoka na zipo kwa wakuu wa idara. Mfano Februari 2024 na juni 2024 malipo yaliidhinishwa ila walimu hawakupata sitahiki zao.

Mbili ni kuhusu walimu wanaoteuliwa kusimamia watoto katika kambi za michezo UMISETA kulipwa malipo duni. Wanawekwa kambini wilayani siku 7 hafu wanasafiri na wanafunzi kwenda Lindi Mjini na kuwekwa tena kambini siku 7. Baada ya msoto huo wote wanalipwa shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) wakati wenzao wa wilaya nyinginezo walikutana kwenye kambi kuu ya mkoa Lindi Mjini wanalipwa laki saba

Walimu wanashindwa kuhoji maana kwa maana taifa hili kwa sasa linaendeshwa kwa uoga. Anayeonekana kuhoji anatafutiwa visa na kuhamishiwa kwenye shule za vijijini sana ambako ili ufike kilwa mjini unatumia nauli isiyopungua elfu 60 kulingana na jografia ya kilwa ilivyo. Pia wanaoonekana kuhoji wananyimwa fursa za kusimamia mitihani ya taifa.

Ninaomba mpaze sauti ili Afisa elimu Sekondari Kilwa na jopo lake wajirekebishe ili walimu wafanye kazi bila manung'uniko.

Asante, naomba kuwasilisha.
 
Huyu Afisa elimu sekondari wilaya ya kilwa anatumia vibaya nafasi aliyonayo hasa kwenye sitahiki za walimu.

Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kulipa sitahiki za walimu mfano malipo ya uhamisho na likizo. Mkurugenzi anasaini malipo yanapitishwa.

Hazina wanapeleka kila sitahiki ya watumishi kwa idara husika. Idara zingine wanalipa watumishi wao, idara ya elimu msingi wanalipa walimu vizuri. Ila idara ya elimu sekondari inakuwa kigugumizi kila mwaka.

Afisa Elimu Sekondari Kilwa achunguzwe kwa ubadhilifu huu ikiwezekana atolewe. Tarehe 27/06/2024 malipo yaliidhinishwa na majina ya walimu wanaotakiwa kulipwa yakawekwa hadharani lakini hadi leo malipo hayafanyiki na taarifa kutoka hazina ni kuwa fedha imeshatoka na ipo kwa mkuu wa idara (Afisa elimu)

Huyu Afisa elimu anapiga sana hata fedha kwa ajili ya michezo UMISETA tuhuma ni hizohizo. Walimu wasimamizi wa shughuli hizo za UMISETA wanalalamika kila mwaka. Wakikutana kambini na walimu wa wilaya nyinginezo za mkoa wa Lindi wakilinganisha wanacholipwa na kile ambacho wenzao wanalipwa ni kama mbingu na ardhi.

Mbaya zaidi Walimu wanaogopa kuhoji kwani kuna baadhi yao walihoji na wakajikuta katika bifu kubwa na Huyo afisa elimu. Hivyo wanabaki na vinyongo mioyoni.
 
Tatizo la walimu ni kuchapana majungu, maisha ya kulinganishana, wivu etc ndo maana watu wanawadharau. Yaani hata mwalimu akianzisha mradi wa kuuza barafu shuleni wenzie watampiga majungu tu. Kifupi hii kada ni ya watu maskini coz maskini ni ngumu kupendana.
 
Haya mambo ni matokeo ya ccm na serikali yake.
Usisahau ulishiliki kusimamia chaguzi za ccm na uwizi wa kura. Kaa kwa kutulia
 
Habari gani wanaJamiiForums?

Mimi ni mdau wa jamvi la JamiiForums nikitokea Kilwa Kivinje Mkoa wa Lindi. Nina mambo mawili ninataka kuyafichua kwa leo.

Moja, ni kuhusu walimu wa kiume wa shule ya sekondari Kivinje kuendeleza mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike.

Tunashukuru miezi ya nyuma kidogo mliandika kuripoti vitendo hivi na tuliona Serikali ikichukua hatua sitahiki kwa muhusika aliyekuwa amempa ujauzito mwanafunzi na kumkatisha kimasomo.

Pamoja na kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikilaaniwa vikali na wadau mbalimbali, bado kuna wimbi kubwa wa walimu wa kiume kuwarubuni watoto wa kike shuleni ili kuwa nao kimapenzi. Taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wanathibitisha kuwa kuna waalimu kadhaa wana hiyo tabia chafu.

Kilichonithibitishia uwepo wa hili jambo ni baada ya mwanangu anayesoma kidato cha nne kunieleza kuwa kuna mwalimu amekuwa akimsumbua kutaka kuwa naye kimapenzi. Niliamua kukutana na muhusika moja kwa moja na alikiri kosa na kuomba msamaha mbele yangu na kuahidi kuacha hiyo tabia mara moja.

Sijataka kutaja jina la huyo mwalimu kwa sababu ya kumfanyia ustaarabu aliouonesha wakati wa mazungumzo yetu. Pia ni kijana mdogo bado anajitafuta, nisingetaka kumpokonya sehemu yake ya kupatia ugali kosa ambalo anaweza akajirekebisha.

Maombi yangu ni kuwa JamiiForums msadie tena kupaza sauti kukemea na kulaani hivi vitendo ili viweze kuisha hapa Kivinje sekondari na kwingineko Tanzania.

Jambo la pili, kuhusu AFISA ELIMU SEKONDARI KILWA na jopo lake kwa ujumla kuwadhulumi walimu wa shule za sekondari haki na sitahiki zao mfano Malipo ya nauli za likizo, malipo ya uhamisho wa vituo vya kazi na malipo ya walimu wanaosimamia UMISETA.

Nikiwa kama mdau wa elimu, ninakutana na walimu mbalimbali na tunasoga kwa sana tu. Ukweli ni kuwa walimu wana manung'uniko ya kudhulumiwa haki na sitahiki zao za msingi na Afisa elimu wao na midomo yao inakuwa bubu kupaza sauti. Nitaelezea kwa kutoa matukio hai kama ifuatavyo.

Moja, mkurugenzi anaidhinisha malipo ya uhamisho na nauli kwa walimu walioenda likizo za malipo, ila malipo hayawafikii walengwa. Yani ni kuwa orodha ya majina ya walimu watakaolipwa nauli inamfikia mkurugenzi. Yeye anaidhinisha malipo na majina ya walimu hao wanaositahili malipo inawekwa hadharani. Lakini malipo hayafanyiki. Walimu wakifuatilia ofisi ya hazina wanapewa majibu kuwa fedha za likizo na uhamisho zimeshatoka na zipo kwa wakuu wa idara. Mfano Februari 2024 na juni 2024 malipo yaliidhinishwa ila walimu hawakupata sitahiki zao.

Mbili ni kuhusu walimu wanaoteuliwa kusimamia watoto katika kambi za michezo UMISETA kulipwa malipo duni. Wanawekwa kambini wilayani siku 7 hafu wanasafiri na wanafunzi kwenda Lindi Mjini na kuwekwa tena kambini siku 7. Baada ya msoto huo wote wanalipwa shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) wakati wenzao wa wilaya nyinginezo walikutana kwenye kambi kuu ya mkoa Lindi Mjini wanalipwa laki saba

Walimu wanashindwa kuhoji maana kwa maana taifa hili kwa sasa linaendeshwa kwa uoga. Anayeonekana kuhoji anatafutiwa visa na kuhamishiwa kwenye shule za vijijini sana ambako ili ufike kilwa mjini unatumia nauli isiyopungua elfu 60 kulingana na jografia ya kilwa ilivyo. Pia wanaoonekana kuhoji wananyimwa fursa za kusimamia mitihani ya taifa.

Ninaomba mpaze sauti ili Afisa elimu Sekondari Kilwa na jopo lake wajirekebishe ili walimu wafanye kazi bila manung'uniko.

Asante, naomba kuwasilisha.
Walimu wamekuwa wakijihusisha na mapenzi na wanafunzi wao toka enzi. Sijui hii tabia wataiacha lini?
 
Huyu Afisa elimu sekondari wilaya ya kilwa anatumia vibaya nafasi aliyonayo hasa kwenye sitahiki za walimu.

Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kulipa sitahiki za walimu mfano malipo ya uhamisho na likizo. Mkurugenzi anasaini malipo yanapitishwa.

Hazina wanapeleka kila sitahiki ya watumishi kwa idara husika. Idara zingine wanalipa watumishi wao, idara ya elimu msingi wanalipa walimu vizuri. Ila idara ya elimu sekondari inakuwa kigugumizi kila mwaka.

Afisa Elimu Sekondari Kilwa achunguzwe kwa ubadhilifu huu ikiwezekana atolewe. Tarehe 27/06/2024 malipo yaliidhinishwa na majina ya walimu wanaotakiwa kulipwa yakawekwa hadharani lakini hadi leo malipo hayafanyiki na taarifa kutoka hazina ni kuwa fedha imeshatoka na ipo kwa mkuu wa idara (Afisa elimu)

Huyu Afisa elimu anapiga sana hata fedha kwa ajili ya michezo UMISETA tuhuma ni hizohizo. Walimu wasimamizi wa shughuli hizo za UMISETA wanalalamika kila mwaka. Wakikutana kambini na walimu wa wilaya nyinginezo za mkoa wa Lindi wakilinganisha wanacholipwa na kile ambacho wenzao wanalipwa ni kama mbingu na ardhi.

Mbaya zaidi Walimu wanaogopa kuhoji kwani kuna baadhi yao walihoji na wakajikuta katika bifu kubwa na Huyo afisa elimu. Hivyo wanabaki na vinyongo mioyoni.
Huyo afisa elimu anaonekana kuwa ni mnyanyasaji. Kuna kundi la WhatsApp nimeona watu wakimlalamikia kuhusu dhuluma anazowafanyia.
 
Kwa kesi ya mapenzi kati za walimu na wanafunzi wadau mbalimbali wa elimu na haki za watoto wangefanya namna kuona linathibitiwa.

Ila hao walimu watu wazima wasomi kabisa wanaoogopa kupambania haki zao sina neno la kutia hapo. Labda mamlaka husika iwaonee huruma wachunguze ukweli wa mambo ukoje ili kila mtu ale chakula chake na huyo kamba iliyomzidi waipunguze kidogo
 
Kwani pesa za watuishi siku hizi zinalipwa mikononi?nacho fahamu uwa Inaandaliwa barua ya kuomba kiasi fulani cha malipo ikiambatanishwa na paylist ya wausika na akaunti namba zao za benki. Muhasibu elimu iwe msingi au sekondari uandaa hati ya malipo kutoka kwenye bajeti ya idara ya elimu kwa kifungu usika kisha uandaliwa cheque kwenda benki ikiwa na orodha ya walipwaji akaunti zao za benki na kiasi cha malipo kwa kila mmoja. Sasa afisa elimu pesa anaichukuaje?
 
Umenisikitisha sana kuacha kumuwajibisha huyo ticha anayetaka kukuchapia binti yako,mngetengeneza mtego kupata ushahidi ili akome,
Kama wewe umelea ufirauni hutakiwi kulaumu wengine kushindwa kutimiza wajibu wao
 
Kwa maelezo yalitolewa ni aidha Afisa anakaa na check muda mrefu japo sijui ukomo wa check unakuwa ni muda gani? Au kuna maujanja yanafanyika ambayo hayajafahamikq bado.
 
Umenisikitisha sana kuacha kumuwajibisha huyo ticha anayetaka kukuchapia binti yako,mngetengeneza mtego kupata ushahidi ili akome,
Kama wewe umelea ufirauni hutakiwi kulaumu wengine kushindwa kutimiza wajibu wao
Au mwamba alishikiwa kitu kidogo akapoa😂
Kama kweli aliamua kumsamehe bure kabisa ili tu asimharibie kazi yake. Huyo mzazi ni mbinguni moja kwa moja maana huo utakatifu ni level zingine
 
Back
Top Bottom