Huyu Afisa elimu sekondari wilaya ya kilwa anatumia vibaya nafasi aliyonayo hasa kwenye sitahiki za walimu.
Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kulipa sitahiki za walimu mfano malipo ya uhamisho na likizo. Mkurugenzi anasaini malipo yanapitishwa.
Hazina wanapeleka kila sitahiki ya watumishi kwa idara husika. Idara zingine wanalipa watumishi wao, idara ya elimu msingi wanalipa walimu vizuri. Ila idara ya elimu sekondari inakuwa kigugumizi kila mwaka.
Afisa Elimu Sekondari Kilwa achunguzwe kwa ubadhilifu huu ikiwezekana atolewe. Tarehe 27/06/2024 malipo yaliidhinishwa na majina ya walimu wanaotakiwa kulipwa yakawekwa hadharani lakini hadi leo malipo hayafanyiki na taarifa kutoka hazina ni kuwa fedha imeshatoka na ipo kwa mkuu wa idara (Afisa elimu)
Huyu Afisa elimu anapiga sana hata fedha kwa ajili ya michezo UMISETA tuhuma ni hizohizo. Walimu wasimamizi wa shughuli hizo za UMISETA wanalalamika kila mwaka. Wakikutana kambini na walimu wa wilaya nyinginezo za mkoa wa Lindi wakilinganisha wanacholipwa na kile ambacho wenzao wanalipwa ni kama mbingu na ardhi.
Mbaya zaidi Walimu wanaogopa kuhoji kwani kuna baadhi yao walihoji na wakajikuta katika bifu kubwa na Huyo afisa elimu. Hivyo wanabaki na vinyongo mioyoni.