Upande wa Pili wa Hotuba ya kuaga ya Baba wa Taifa ukumbi wa Diamond 1985

Upande wa Pili wa Hotuba ya kuaga ya Baba wa Taifa ukumbi wa Diamond 1985

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
UPANDE WA PILI WA HOTUBA YA MWALIMU YA KUAGA

Kiasi naogopa kufanya uchambuzi wa hii hotuba kwani kuna mambo nadhani Mwalimu Nyerere kasahau au hakupenda watu wayasikie.

Mwalimu hakupokelewa na wazee alipokelewa na Abdul Sykes 1952 tena si New Street kwenye ofisi ya TAA bali nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Wazee walikuwapo siku zote katika siasa za AA na TAA lakini uongozi wa chama kuanzia 1950 ulikuwa chini ya vijana wakiongozwa na Abdul Sykes.

Bahati mbaya Mwalimu huenda alipitiwa kutaja majina hata machache ya hawa wazee ambao wote walikuwa wajumbe wa Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir.

Mikutano yote ya siri ya kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na Nyerere akihudhuria.

Wakati African Association inafungua tawi Tabora Nyerere alikuwapo kwenye mkutano huo na wakati huo haikuwa TAA jina hili lilikuja 1948.

Majina ya viongozi wa tawi hili yanafahamika walikuwa akina Kivuruga na Fundi Muhindi watu maarufu Tabora.
Nyerere alipokuja kuchaguliwa Katibu Hamza Mwapachu alichaguliwa Rais na hii ilikuwa 1946.

Wakati Nyerere anapelekwa kwa Abdul Sykes na Kasella Bantu, Abdul alikuwa Katibu na Kaimu Rais nafasi iliyokuwa imeshikwa na Dr. Vedasto Kyaruzi toka 1950.

Si kweli kuwa TAA ilikuwa "imesinzia kidogo," kwani kuanzia 1950 Dr. Kyaruzi walipochukua uongozi TAA ilifanya mambo makubwa.

Ilipeleka mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Twining 1950 na iliunda Political Subcommitee wajumbe wakiwa Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia.

TAA ilimwajiri Alexander Tobias kama Katibu kuendesha ofisi na akilipwa mshahara.

1950 Abdul Sykes alisafiri hadi Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta na Peter Mbiu Koinange na wazalendo wengine katika uongozi wa KAU kuunganisha nguvu.

1952 TAA ilishughulikia mgogoro wa Ardhi ya Wameru na kusaidia Japhet Kirilo kwenda UNO akiongozana na Earle Seaton.

Hakika hizi si dalili za chama "kilichosinzia kidogo."
Yapo mengi ambayo Mwalimu huenda hakuyajua au kasahau.

Safari ya kwanza ya Nyerere ilikuwa Morogoro akifatana na Zuberi Mtemvu lakini haikuwa na mafanikio.
Safari iliyofuata ilikuwa Lindi, Mtwara na Mikindani.

Safari hii Nyerere alifuatana na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Rajab Diwani.

Safari ya Jimbo la Kusini yaani Southern Province ilikuwa na makubwa sana kwani huko ndiko ilipokuwa ngome ya Kanisa ambalo lilikuwa linapiga vita TANU kichinichini kwa kuwatisha waumini wake kuwa TANU inataka kuleta Vita Vya Maji Maji nyingine dhidi ya Waingereza.

Watu wawili walikuja Dar-es-Salaam, Salum Mpunga na Ali Mnjale walitumwa kuja kueleza tatizo hili kubwa lililokuwa linarudisha nyuma juhudi za ukombozi wa Tanganyika.

Yapo mengi.

PICHA: Maulidi na Abdallah Kivuruga.

PICHA:Clement Mohamed Mtamila Mwenyekiti wa TANU, Julius Nyerere Rais wa TANU nyuma ni Zuberi Mtemvu Katibu wa TANU na Mama Maria aliyekaa.

PICHA: Alexander Tobia General Secretary wa TAA mwajiriwa aliyekuwa kachero wa Special Branch ndani ya TAA.

PICHA: Kushoto: Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti Baraza la Wazee wa TANU, John Rupia Makamu Rais wa TANU na Julius Nyerere Rais wa TANU na nyuma ni vijana wa BANTU Group wahamasishaji na walinzi wa viongozi wa TANU.

1625855916204.png
1625855958868.png
1625855991634.png
1625856023683.png
1625856047623.png
 
Ahsante kwa ufafanuzi...
Smart...
Kuhusu katiba ya TANU ukweli ni kuwa hawakukaa kujadili chochote

Katiba ya TANU ilinakiliwa kutoka katiba ya Convention Peoples Party (CPP) ya Kwame Nkrumah wa Ghana.

Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa kukwepa usumbufu wa Waingereza kwani walijua wangewataabisha kuwataka wabadilishe hiki au kile.

Sasa kwa kuwa Waingereza walikuwa wameikubali katika ya CPP hapakuwa na sababu ya kuikataa katiba ya TANU.

Yapo mengi.
 
Back
Top Bottom