Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Vita vya upande wa Gaza vimepata umaarufu kwa vile ni vya wazi na athari zake zinaoneshwa kwa ulimwengu mzima, lakini kumbe vita vinavyoendelea kimya kimya kule ukingo wa Magharibi na Mashariki ya Jerusalem ni vikubwa zaidi.
Eneo hilo miaka michache iliyopita lilikuwa ni ardhi kubwa iliyoshikana na yote ikijulikana kama maeneo ya Wapalestina. Miji yake maarufu ambayo wengi watakuwa wanaikumbuka ni kama vile Ramallah, Jeusalem, Jeriko, Jenin na kuendelea.
Katika uporaji ambao umefanyika na unaendelea kila siku maeneo hayo yate, yamechongwa kwa vizuizi vya kuta na madaraja kiasi kwamba familia kadhaa haziwezi tena kutembeleana bila kupata ruhusa za askari wa Israel.
Utenganishwaji huo haujakoma katu, kila baada ya muda mfupi familia zilizobaki hupokea nyaraka za kuwataka wahame ili kupisha ujenzi wa makaazi mapya ya familia za Kiyahudi.
Familia zinazokaidi amri hizo kwa hoja hapo ni kwao au hawana pa kwenda hupewa tarehe maalum za kuja kuvunjwa kwa nguvu majengo yao na kweli huvunjwa na wao kuelekea kwa wenzao kabla nako hawajapewa amri nyengine za kuhama.
Ubaya wa vita vinavyoendelea kingo za Magharibi ni kwamba hutekelezwa kwa namna mbili; kuna amri za kiserikali na amri za walowezi ambao wote wamepewa silaha za moto. Ili kurahisisha kazi zao mara nyingi walowezi hao huvaa sare za jeshi au huambatana na majeshi halisi kutekeleza uporaji wao.
Tangu kutokea kwa shambulio la Hamas ndani ya Israel hapo Oktoba 7 hali imekuwa mbaya zaidi. Kwa mfano, kwenye kijiji cha Qusra familia za Kipalestina zimekuwa zikivamiwa kwenye majumba na mashamba yao ya zaituni na kuuliwa.
Familia moja ya kijiji hicho baada ya kushambuliwa bila sababu na watoto wao kuuliwa walikwenda kufuata maiti kwenye hospitali moja nje ya kijiji. Safari hiyo tofauti na kawaida ya misafara yoo ambapo hupeperusha bendera za taifa la Palestina, waliamua kutoweka bendera. Pamoja na hivyo walowezi waliwafahamu na kuwashambulia na kuua wana familila wengine.
Wapalestina wa maeneo hayo wanasema mikasa ya aina hiyo ni endelevu bila ya msaada wowote na kwamba kila siku wanazidi kuminywa kwenye maeneo finyu yasiyo na huduma nzuri na mwishowe kupoteza ardhi zao kabisa.
BBC: