SI KWELI Upanga wa aina hii ulitumika na watu wa zamani

SI KWELI Upanga wa aina hii ulitumika na watu wa zamani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Picha hii na maandiko yamekuwa yakisambaa mtandaoni, yakielezea dhana ya kwamba watu wa zamani walikuwa wakiishi duniani, na kwamba baadhi ya mabaki ya silaha zao kubwa ambazo zilikuwa zinatumika "upanga" yamepatikana.
1731699525623.jpg

 
Tunachokijua
Upanga ni silaha yenye makali inayoshikwa mkononi kwa ajili ya kukata, kimuonekano hufanana na kisu ila hutofautiana kwa ukubwa kwa kuwa upanga una umbo kubwa hasa ubapa wake huwa mpana na mrefu na mpini wake ni mkubwa kwa sababu mkono wote unahitaji kushika silaha hii.
images

Kumekuwepo na picha ya upanga mkubwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii inayodaiwa kuwa ni mabaki ya silaha za watu wa zamani ambao umechimbuliwa Ardhini, upanga huo una umbo kubwa huku ukiwa na muonekano wa kutu ndani ya shimo Tazama hapa, hapa, hapa, hapa na hapa

Je, uhalisia wa Picha hiyo upoje?

JamiiCheck imefatilia uhalisia wa picha hiyo na kubaini kuwa Taarifa hizo Si za kweli kwani Picha hiyo Si halisi bali Imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba(AI)

Aidha, hakuna taarifa za kupatikana kwa upanga wenye ukubwa huo kwenye Vyombo vya kuaminika vya taarifa ambapo kwa picha hiyo ingelikuwa ni Taarifa kubwa ya kidunia na kuandikwa kama moja ya rekodi ya vitu vya kale na kutangazwa duniani lakini hakuna Taarifa hizo.

Vilevile, Katika picha hiyo tumebaini ina ishara kadhaa za kuthibitisha kuwa Siyo picha halisi na kuwa imetengenzwa kwa akili Mnemba.

-Watu wanaoonekana katika picha hiyo sura zao hazipo Sawa, wamegubikwa na giza jeusi kama picha imepigwa gizani wakati picha inaonesha imepigwa kwenye Mwanga ndio maana kuna vivuli.

- Kwenye mazingira hayo hakuna mmea wowote unaoonekana hata kwa mbali licha ya picha kuchukua eneo kubwa la ardhi

-Picha inaonesha kamera ilikuwa karibu na Upanga ndio maana upanga umeonekana kwa karibu lakini watu walio karibu na upanga wameonekana wadogo sana kama wamepigwa picha kutoka mbali na huku nao wapo karibu na Upanga.

Aidha, Picha za aina hiyo za kuonesha Upanga ziko nyingi zenye maumbo tofauti tofauti ambazo zimetengenezwa kwa akili Mnemba(AI) na zote huwa zinasambazwa na madai hayo kuwa ni mabaki ya Silaha za Watu wa kale kitu ambacho Si kweli.​

1731750674471-png.3153650

6728368a19a2b.webp

images

GcQo8KSWEAAwlFE

Waliitwa MAJITU (Giants) na kwa mujibu wa Biblia ni Uzao uliopatikana baada ya Malaika walioasi (Fallen angels)kuzaana na binti wana wa Binadamu. (Soma kitabu cha Enock sura ya 6 - 12.)
Kwa hiyo huo upanga wa size hiyo yawezekana ulikuwepo kweli zama hizo ?? 🤔 🤔
 
Picha hii na maandiko yamekuwa yakisambaa mtandaoni, yakielezea dhana ya kwamba watu wa zamani walikuwa wakiishi duniani, na kwamba baadhi ya mabaki ya silaha zao kubwa ambazo zilikuwa zinatumika "upanga" yamepatikana.
Kuwa makini na kila unachokiona mtandanoni. siku hizi kumekuwepo na utitiri wa picha na video ambazo ni AI generated watu wanatafuta followers, comments n.k.
 
Kuwa makini na kila unachokio

kuwa makini na kila unachokiona mtandanoni. siku hizi kumekuwepo na utitiri wa picha na video ambazo ni AI generated watu wanatafuta followers, comments n.k.
Yeah upo sahihi kabisa mkuu.. Dunia inaenda kasi sana kwa teknologia..
 
Ingekuwa ni kweli hata CNN pamoja na media nyingine reliable ingekuwa breaking news, kwenye Google au Wikipedia au Guinness book of records ungekuwa unakuta vitu vya hii.

Hizi images hutengenezwa kwa agenda(cheap agenda) maalum na watu cheap na wasio makini, mtu yoyote mwenye kutafakari anajua fika kutenganisha mbivu na mbichi.
Kweli media kama hizo CNN na platform nyinginezo wangetoa tamko kuhusu hilo.. ✍️ ✍️
 
Tafsiri ya wanefili ni “watu wakubwa”.. yaani watu wenye maumbo makubwa. Hivyo wanefili walikuwa ni watu wenye miili makubwa sana..

Na biblia inaendelea kusema kuwa walikuwa ni WATU HODARI na WENYE SIFA. Maana yake walikuwa ni watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili na vile vile walikuwa ni watu wenye sifa (maaana yake maarufu na wanaojulikana sana).

Hivyo hawakuwa tu wakubwa kama tembo halafu hawana akili, hapana! Walikuwa wakubwa na vile vile walikuwa na uwezo mkubwa wa kiakili, ambao

View attachment 3153424 uliwafanya wawe maarufu.
Kwa maana hiyo hata zana zao kama hizo ziliendana na miili yao
Du ndio kama huo mnefili pichani?
 
Back
Top Bottom