Picha hii na maandiko yamekuwa yakisambaa mtandaoni, yakielezea dhana ya kwamba watu wa zamani walikuwa wakiishi duniani, na kwamba baadhi ya mabaki ya silaha zao kubwa ambazo zilikuwa zinatumika "upanga" yamepatikana.
- Tunachokijua
- Upanga ni silaha yenye makali inayoshikwa mkononi kwa ajili ya kukata, kimuonekano hufanana na kisu ila hutofautiana kwa ukubwa kwa kuwa upanga una umbo kubwa hasa ubapa wake huwa mpana na mrefu na mpini wake ni mkubwa kwa sababu mkono wote unahitaji kushika silaha hii.
Kumekuwepo na picha ya upanga mkubwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii inayodaiwa kuwa ni mabaki ya silaha za watu wa zamani ambao umechimbuliwa Ardhini, upanga huo una umbo kubwa huku ukiwa na muonekano wa kutu ndani ya shimo Tazama hapa, hapa, hapa, hapa na hapa
Je, uhalisia wa Picha hiyo upoje?
JamiiCheck imefatilia uhalisia wa picha hiyo na kubaini kuwa Taarifa hizo Si za kweli kwani Picha hiyo Si halisi bali Imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba(AI)
Aidha, hakuna taarifa za kupatikana kwa upanga wenye ukubwa huo kwenye Vyombo vya kuaminika vya taarifa ambapo kwa picha hiyo ingelikuwa ni Taarifa kubwa ya kidunia na kuandikwa kama moja ya rekodi ya vitu vya kale na kutangazwa duniani lakini hakuna Taarifa hizo.
Vilevile, Katika picha hiyo tumebaini ina ishara kadhaa za kuthibitisha kuwa Siyo picha halisi na kuwa imetengenzwa kwa akili Mnemba.
-Watu wanaoonekana katika picha hiyo sura zao hazipo Sawa, wamegubikwa na giza jeusi kama picha imepigwa gizani wakati picha inaonesha imepigwa kwenye Mwanga ndio maana kuna vivuli.
- Kwenye mazingira hayo hakuna mmea wowote unaoonekana hata kwa mbali licha ya picha kuchukua eneo kubwa la ardhi
-Picha inaonesha kamera ilikuwa karibu na Upanga ndio maana upanga umeonekana kwa karibu lakini watu walio karibu na upanga wameonekana wadogo sana kama wamepigwa picha kutoka mbali na huku nao wapo karibu na Upanga.
Aidha, Picha za aina hiyo za kuonesha Upanga ziko nyingi zenye maumbo tofauti tofauti ambazo zimetengenezwa kwa akili Mnemba(AI) na zote huwa zinasambazwa na madai hayo kuwa ni mabaki ya Silaha za Watu wa kale kitu ambacho Si kweli.