UPDATE 1: Mfahamu "Jenerari" atakaeongoza "Jeshi" la Simba SC 01.10.2016.

UPDATE 1: Mfahamu "Jenerari" atakaeongoza "Jeshi" la Simba SC 01.10.2016.

Mashabiki na Wanachama wa Simba SC tukiwa tunaendelea kuzihesabu siku zilizobaki kuelekea katika "vita' yetu dhidi ya Yanga SC.. namleta kwenu Jenerari atakaetuongoza siku hiyo.

Huyu Jenenari nani?
Ni Joseph Marius Omog, ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba SC. Omog ambaye ana heshima kubwa sana barani Africa, alizaliwa miaka 44 nchini Kameruni.

Omog ana uzoefu gani katika soka?
Ni ngumu sana kumtenganisha Omog na mpira, kwani tangu akiwa kinda amepiga mpira mwingi sana nchini kwao. Mojawapo ya timu aliyocheza kwa kiwango kikubwa ni Dragon Yaounde. Hakudumu sana dimbani, kabla hajachukua maamuzi magumu ya kusomea ukocha.

Ni "magamba" gani ya ukocha aliyo nayo katika kabati lake?
Ukiuliza wachambuzi wa soka nchini Kameruni, Omog ni nani? Jibu lao hua ni.. "Omog is highly learned man in formal coaching training"
Baadhi ya "magamba" aliyonayo ni;
1. Amesoma Sports and Physical Education ya katika chuo bora cha soka Africa, kiitwacho Higher Institute of Youth and Sport, kilichopo nchini Kameruni.
2. Ana UEFA license level B, aliyoipata "kwa waojua" nchini Ujerumani mnamo mwaka 1987.

Ni timu gani alizowahi kufundisha?
2001 - 2010... Timu ya Taifa ya Kameruni
2011 - 2013... AC Leopards ya Congo Brazaville
2013 - 2014... Azam FC
2016 - ............ Simba SC

Je kuna mafanikio yoyote aliyowahi kupata kama kocha?
Baadhi ya mafanikio yake ni;
2011 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa FA Cup ya nchini Congo.
2012 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa makombe mawili, ambayo ni CAF Confederation Cup na Congo Premier League.
2013 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa Congo Premier League.
2014 - Aliiongoza Azam FC kutwaa taji lake la kwanza la ligi kuu.
NOTE:
Mwaka 2012 Joseph Marius Omog alikamata namba 2 katika tuzo ya kocha bora barani Africa, nyuma ya Renard Herve.

Huyo ndo Joseph Marius Omog, Jenerari ambae anaenda kuongoza Mashabiki na Wanachama wa Simba SC duniani katika katika "vita" hiyo.. Naimani tunaenda kushinda asubuhi sana.

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING.
Neno langu kwa Masau Bwire.. "kilichowakosa JKT Ruvu siku ya jumamosi.. ndicho mtakipata leo.".

cc Makoye Matale na "wenzake".
Hapo natia shaka. Umesema kuwa Omog ana miaka 44 i.e. born (1972), halafu alipata UEFA License B nchini Ujerumani mwaka 1987? Ina maana hata kwa umri wa "formal education" yeye alikuwa akisomea ukocha tu? Kwanza kocha mzuri asingekuja huku TZ.
 
Hapo natia shaka. Umesema kuwa Omog ana miaka 44 i.e. born (1972), halafu alipata UEFA License B nchini Ujerumani mwaka 1987? Ina maana hata kwa umri wa "formal education" yeye alikuwa akisomea ukocha tu? Kwanza kocha mzuri asingekuja huku TZ.


Mkuu sio Mimi naliyosema hayo.. ni wakameruni wenyewe wamesema hayo.. katika link hii Profile - Marius Omog, Flag Bearer of Cameroonian Coaches

Alafu unapata wapi uthubutu wa kusema kocha aliyehukua kombe la shirikisho barani Africa, makombe ya ligi mawili mfululizo katika ligi ngumu barani Africa nchini Congo na kombe la ligi kuu TZ si mzuri? Au kwa kua anafundisha Simba SC.. umenistaajabisha.
 
Hapo natia shaka. Umesema kuwa Omog ana miaka 44 i.e. born (1972), halafu alipata UEFA License B nchini Ujerumani mwaka 1987? Ina maana hata kwa umri wa "formal education" yeye alikuwa akisomea ukocha tu? Kwanza kocha mzuri asingekuja huku TZ.
sembo hii habari uliyoitunga imekushushia sana hadhi ,Omog alipata leseni ya UEFA akiwa na miaka 15 ?

James7 hii story imetengenezwa na asilimia kubwa ni uongo mtupu.Ndugu zetu Wamchangani wamezoea kudanganywa na viongozi wao na wao wameshakuwa mabingwa wa uongo
 
Nina imani na cocha wetu JOSEPH MARIUS OMOG kwani ni cocha aliefanikia katika ufundishaji barani Africa
 
Nina imani na cocha wetu JOSEPH MARIUS OMOG kwani ni cocha aliefanikia katika ufundishaji barani Africa

Mkuu.. Omog kawavuruga sana hawaamini wanachokiona. Sasa wanatafuta kila njia kumfanya aonekane si lolote si chochote.

Tuna Imani na Joseph Marius Omog.
 
Hapo ndo mnapoharibu nyie watu.. Ila najua ndio propaganda za viongozi wenu ili wapige pesa... Simba nguvu zao na akili yao c kuchukua mataji, wala Kutengeneza mafanikio ya kudumu, wao wakiifunga yanga bhaaaaasi yatosha, hapo ndo unaona tofauti ya Yanga na Mikia,.. Ila hii ni kutokana na mikia kutaka sifa Kuwa wameifunga club Kubwa kwao huku yanga wakiichukulia kama mechi ya kawaida sana. Mikia inatamani siku moja iwe kama Yanga, huku Yanga ikitamani siku moja iwe kama Mazembe.
 
Back
Top Bottom