Mashabiki na
Wanachama wa
Simba SC tukiwa tunaendelea kuzihesabu siku zilizobaki kuelekea katika "vita' yetu dhidi ya
Yanga SC.. namleta kwenu Jenerari atakaetuongoza siku hiyo.
Huyu Jenenari nani?
Ni
Joseph Marius Omog, ambaye ni Kocha Mkuu wa
Simba SC.
Omog ambaye ana heshima kubwa sana barani Africa, alizaliwa miaka 44 nchini Kameruni.
Omog ana uzoefu gani katika soka?
Ni ngumu sana kumtenganisha
Omog na mpira, kwani tangu akiwa kinda amepiga mpira mwingi sana nchini kwao. Mojawapo ya timu aliyocheza kwa kiwango kikubwa ni Dragon Yaounde. Hakudumu sana dimbani, kabla hajachukua maamuzi magumu ya kusomea ukocha.
Ni "magamba" gani ya ukocha aliyo nayo katika kabati lake?
Ukiuliza wachambuzi wa soka nchini Kameruni, Omog ni nani? Jibu lao hua ni..
"Omog is highly learned man in formal coaching training"
Baadhi ya "magamba" aliyonayo ni;
1. Amesoma
Sports and Physical Education ya katika chuo bora cha soka Africa, kiitwacho Higher Institute of Youth and Sport, kilichopo nchini Kameruni.
2. Ana UEFA license level B, aliyoipata "kwa waojua" nchini Ujerumani mnamo mwaka 1987.
Ni timu gani alizowahi kufundisha?
2001 - 2010... Timu ya Taifa ya Kameruni
2011 - 2013... AC Leopards ya Congo Brazaville
2013 - 2014... Azam FC
2016 - ............ Simba SC
Je kuna mafanikio yoyote aliyowahi kupata kama kocha?
Baadhi ya mafanikio yake ni;
2011 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa FA Cup ya nchini Congo.
2012 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa makombe mawili, ambayo ni CAF Confederation Cup na Congo Premier League.
2013 - Aliiongoza AC Leopards, kutwaa Congo Premier League.
2014 - Aliiongoza Azam FC kutwaa taji lake la kwanza la ligi kuu.
NOTE:
Mwaka 2012
Joseph Marius Omog alikamata namba 2 katika tuzo ya kocha bora barani Africa, nyuma ya Renard Herve.
Huyo ndo
Joseph Marius Omog, Jenerari ambae anaenda kuongoza
Mashabiki na
Wanachama wa
Simba SC duniani katika katika "vita" hiyo.. Naimani tunaenda kushinda asubuhi sana.
KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING.
Neno langu kwa Masau Bwire..
"kilichowakosa JKT Ruvu siku ya jumamosi.. ndicho mtakipata leo.".
cc
Makoye Matale na "wenzake".