Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Zaidi ya mahujaji Elfu moja wamepoteza maisha katika mji wa Makka walikokuwa wamekwenda kuhiji kama sehemu ya kutimiza nguzo kuu tano kwa muislamu yeyote yule mwenye uwezo walau mara moja tu katika uhai wake kuweza kufika katika mji huo mtakatifu kwa waislamu .
Vifo hivyo inasemekana vimetokana na kuchochewa na joto kali sana lililokuwa limetokea katika Wiki hii na kufikia nyuzi joto 51 ,kwa wale tuliosoma Geography tunaelewa maana ya joto hili kuwa ni la juu sana na hatari kwa maisha mwanadamu.
Nchi mbalimbali zimeripoti vifo vya watu wake,huku Misri ikiongoza kupoteza watu wake ,ambapo mpaka sasa imepoteza watu 658. Tanzania haijapoteza wala kutokea kifo cha mtanzania yeyote yule wala majeruhi .
Tuendelee kuwaombea wenzetu hao warejee salama kabisa hapa Nchini na kuungana na familia zao.
Chanzo cha habari yangu ni Gazeti la Mwananchi la kiswahili.kwa undani zaidi unaweza jipatia nakala yake au kusoma kupitia mtandaoni na kulipia kulingana na uwezo wako wa kifedha. Lakini pia natamani wenye uwezo wa kifedha mliopo humu jukwaani pia mngekuwa mnachangia Jamii forum pesa kidogo ili kuwatia moyo .ikumbukwe hili ni jukwaa linalotukutanisha maelfu ya watanzania na kujadili masuala mbalimbali kwa uhuru sana.
Kazi iendelee.Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
PIA SOMA
- Saudi Arabia: Mahujaji zaidi ya 500 wafariki wakati wa Hija huko Makka