UPDATE: Mahujaji zaidi ya Elfu Moja wamefariki Makka. Hakuna Mtanzania aliyepoteza Maisha wala kujeruhiwa

UPDATE: Mahujaji zaidi ya Elfu Moja wamefariki Makka. Hakuna Mtanzania aliyepoteza Maisha wala kujeruhiwa

Ndugu zangu Watanzania,

Zaidi ya mahujaji Elfu moja wamepoteza maisha katika mji wa Makka walikokuwa wamekwenda kuhiji kama sehemu ya kutimiza nguzo kuu tano kwa muislamu yeyote yule mwenye uwezo walau mara moja tu katika uhai wake kuweza kufika katika mji huo mtakatifu kwa waislamu .

Vifo hivyo inasemekana vimetokana na kuchochewa na joto kali sana lililokuwa limetokea katika Wiki hii na kufikia nyuzi joto 51 ,kwa wale tuliosoma Geography tunaelewa maana ya joto hili kuwa ni la juu sana na hatari kwa maisha mwanadamu.

Nchi mbalimbali zimeripoti vifo vya watu wake,huku Misri ikiongoza kupoteza watu wake ,ambapo mpaka sasa imepoteza watu 658. Tanzania haijapoteza wala kutokea kifo cha mtanzania yeyote yule wala majeruhi .

Tuendelee kuwaombea wenzetu hao warejee salama kabisa hapa Nchini na kuungana na familia zao.

Chanzo cha habari yangu ni Gazeti la Mwananchi la kiswahili.kwa undani zaidi unaweza jipatia nakala yake au kusoma kupitia mtandaoni na kulipia kulingana na uwezo wako wa kifedha. Lakini pia natamani wenye uwezo wa kifedha mliopo humu jukwaani pia mngekuwa mnachangia Jamii forum pesa kidogo ili kuwatia moyo .ikumbukwe hili ni jukwaa linalotukutanisha maelfu ya watanzania na kujadili masuala mbalimbali kwa uhuru sana.

Kazi iendelee.Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Saudi Arabia: Mahujaji zaidi ya 500 wafariki wakati wa Hija huko Makka
Haya makafara ya wenzetu haya
Juzi walisema wanachinja
 
Kama kweli wanaokufa huko ni mashahidi wa mungu na wanakwenda peponi Moja Kwa Moja, Basi sio jambo la kujivunia Kwa waTanzania kutokufa, inawezekana walioenda huko wengi ni CHAWA ambazo ni mashahidi wa Samia na si Mashahidi wa Mungu
 
Kama kweli wanaokufa huko ni mashahidi wa mungu na wanakwenda peponi Moja Kwa Moja, Basi sio jambo la kujivunia Kwa waTanzania kutokufa, inawezekana walioenda huko wengi ni CHAWA ambazo ni mashahidi wa Samia na si Mashahidi wa Mungu
Uwe na heshima kwa Mheshimiwa Rais.
 
Katika Uislam tunaamini wanaokufa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni mashaheed.

Dua zao zimekubaliwa, hiyo ni one way ticket ya peponi.
Labda pepo ya mabwege, wauza unga kibao tu wanajenga misikiti na kwenda Hija.

Hija ni njia ya Saudi Arabia kuingiza pesa kwa utalii wa kidini.
 
Hii habari kichwa chake hakija kaa sawa. Ilitakiwa isomeke "Mahujaji 1000 wamepata thwawabu ya kufia mahala patakatifu na kwenda peponi moja kwa moja".
Rekebisheni kichwa cha huu uzi.
 
Hii habari kichwa chake hakija kaa sawa. Ilitakiwa isomeke "Mahujaji 1000 wamepata thwawabu ya kufia mahala patakatifu na kwenda peponi moja kwa moja".
Rekebisheni kichwa cha huu uzi.
Uwe na utu ndugu yangu
 
Ndugu zangu waislam watanzania inamaana mmegoma kuipokea neema na thawabu ya kwenda peponi Bureeeee kwenye mabikra wakutosha 😭😭

Au mnamashaka na swawabu hizo
 
Kazi ni kipimo cha utu.Tuendelee kuchapa kazi kujikwamua kiuchumi hasa kipindi hiki ambacho Rais wetu na serikali yake Anaendelea kuweka mazingira wezeshi na mazuri kutuwezesha wananchi kuinuka kiuchumi kwa kila shughuli tuifanyayo..
Mtu ambaye darasani somo la hesabu alikuwa hawezi kupata alama walau hata kumi hawezi kujua ukimwambia huyu mama yako Samia anaharibu uchumi,amekuza ufisadi na wizi wa kila aina,huyo mtu anachojua yy ni kusifu tu,biashara hajawahi fanya na hajui chochote,matatizo ya kibiashara hayajui,yy anajua kimoja tu kusifu basi.kila ukiwaza kwamba Hv huyu binadamu hana hata ka shule kidogo?shilingi yetu iko hoi kabisa asiyejua hesabu anasifu eti nchi imefunguka.mwehu ni mwehu tu.
 
Back
Top Bottom