Update: Muuguzi mlevi aliyetuhumiwa kumbaka mjamzito wodini aachiwa huru

Update: Muuguzi mlevi aliyetuhumiwa kumbaka mjamzito wodini aachiwa huru

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Screenshot 2023-06-13 at 12-20-53 EastAfricaRadio on Twitter.png


..........................................................................................
TABORA: Muuguzi daraja la pili, Rayson Duwe aliyetuhumiwa kumbaka Mjamzito wa Wiki 32 aliyekuwa amelazwavkatika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge, ameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilayani humo, baada ya upande wa Mashitaka kushindwa kuthibitisha tuhuma za kumchoma Dawa ya usingizi kisha kumbaka Mjamzito huyo

Aidha, Ushahidi ulitofautiana baada ya Shahidi wa Kwanza ambaye ni Mjamzito kusema alibakwa Juni 10, 2023, Saa 5 Usiku, ikiwa ni Siku ya 2 baada ya kufika Hospitalini hapo wakati Mshtakiwa akimhudumia, Shahidi wa Pili ambaye ni Muuguzi alidai tukio lilikuwa Juni 9, 2023, Saa 2 Usiku, na Shahidi wa 3 alidai tukio lilikuwa saa 4 Usiku Juni 9, 2023, ambapo katika Mashahidi wote hakuna aliyeweza kuthibitisha kama Muuguzi huyo ni kweli alimbaka Mgonjwa

Hata hivyo, Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa Mtumishi huyo aliyekuwa zamu siku hiyo, eneo la mapokezi ya Wagonjwa wa Nje, (OPD) na aliingia kazini akiwa amelewa. Pia Mtuhumiwa alikutwa na bomba la Sindano na dawa za Usingizi huku taarifa ya Kitabibu ikithibitisha kuwa alimwingilia Mgonjwa huyo

........................................................................................................................................................

Rayson Agnelusi Duwe ambaye ni muuguzi msaidizi daraja II (ANO) katika hospitali ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mama mgonjwa mwenye ujauzito wa miezi tisa baada ya kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema tukio hilo lilitokea Juni 9. 2023 majira saa mbili usiku.

Kamanda Abwao amesema muuguzi huyo ambaye aliingia kazini akiwa amelewa pombe alitenda kosa hilo wakati alipopangiwa zamu ya usiku ya kuhudumu wagonjwa wa nje (OPD) ndipo alipotoka na kwenda chumba cha wagonjwa wa ndani na kumbaka mama huyo mwenye ujauzito wa karibu kujifungua ambaye alikuwa anaendelea na matibabu ya ugojwa wa malaria.

Muuguzi huyo alikutwa akiwa na bomba la sindano pamoja na dawa za usingizi huku taarifa ya kitabibu ikidhibitisha kuwa alimwingilia mgonjwa huyo.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakani mapema hii leo June 13,2023 kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya upelelezi kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
 
#HABARI Rayson Agnelusi Duwe ambaye ni muuguzi msaidizi daraja II (ANO) katika hospitali ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mama mgojwa mwenye ujauzito wa miezi tisa baada ya kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema tukio hilo lilitokea Juni 9. 2023 majira saa mbili usiku

Kamanda Abwao amesema muuguzi huyo ambaye aliingia kazini akiwa amelewa pombe alitenda kosa hilo wakati alipopangiwa zamu ya usiku ya kuhudumu wagonjwa wa nje (OPD) ndipo alipotoka na kwenda chumba cha wagonjwa wa ndani na kumbaka mama huyo mwenye ujauzito wa karibu kujifungua ambaye alikuwa anaendelea na matibabu ya ugojwa wa malaria.

Muuguzi huyo alikutwa akiwa na bomba la sindano pamoja na dawa za usingizi huku taarifa ya kitabibu ikidhibitisha kuwa alimwingilia mgonjwa huyo.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakani mapema hii leo June 13,2023 kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya upelelezi kukamilika #EastAfricaTV
 
Tabora mbona Kuna watumishi wa afya wapuuzi kiasi hiki? Sakata la manesi kuchanachana mapacha na kunyofoa viungo, sakata la mabishano kati ya nesi na mtu wa maabara kuhusu vifaavya malaria vilivyoisha muda, Leo tena muuguzi Kabaka mgonjwa tena mjamzito.
Kuna shida gani huko?
 
Back
Top Bottom